Man City wawazima Man U nyumbani Old Trafford

Kevin De Bruyne alifunGa bao la kwanza la Man City dakika ya 15

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15

Pep Guardiola aliibuka mshindi katika mechi ya kwanza ya lingi kuu nchini Uingezea katika mechi iliyochezwa kati ya Manchester United na Manchester City nyumbani kwa Man U huko Old Trafford.

Kevin De Bruyne alifunga bao la kwanza la Man City dakika ya 15 alipovamia ngome ya Manchester United na kumpata mlinzi Daley akiwa usingizini.

Raia huyo wa ubelgiji pia alitoa mchango mkubwa katika bao la pili na Man City, baada ya kumpa pasi safi Kelechi Iheanacho ambaye aliutumbukiza mpira wavuni bila kuchelewa.

Iheanacho, mshambuliaji raia wa Nigeria mwenye umri wa miaka 19, alisema anafuraha sana kwa kuipa klabu yake bao la ushindi, na kuongeza imani yake mbele ya meneja Pep Guardiola.

Jose Maurinho na Pep Guardiola

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Jose Maurinho na Pep Guardiola