Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Trump kuzuru Mexico licha ya msimamo mkali
Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amekubali mwaliko wa kumtembelea rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, Jumatano.
Afisi ya rais huyo imesema mipango ya kufanyika kwa mazungumzo ya faraghani baina ya wawili hao inakaribia kukamilishwa.
Mkutano huo utafanyika muda mfupi kabla ya Bw Trump kutoa hotuba kuhusu uhamiaji nchini Marekani.
Kwenye kampeni, Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama "wahalifu" na "wabakaji".
Ameahidi kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji hao kuingia nchini humo iwapo atachaguliwa kuwa rais.
Rais Pena Nieto pia ametoa mwaliko kwa mgombea urais wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton.