Trump kuzuru Mexico licha ya msimamo mkali

Trump

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha, Kwenye kampeni, Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama "wahalifu" na "wabakaji"

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump, amekubali mwaliko wa kumtembelea rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, Jumatano.

Afisi ya rais huyo imesema mipango ya kufanyika kwa mazungumzo ya faraghani baina ya wawili hao inakaribia kukamilishwa.

Mkutano huo utafanyika muda mfupi kabla ya Bw Trump kutoa hotuba kuhusu uhamiaji nchini Marekani.

Kwenye kampeni, Bw Trump amewaeleza wahamiaji wa Mexico wanaoingia Marekani kama "wahalifu" na "wabakaji".

Ameahidi kujenga ukuta kuwazuia wahamiaji hao kuingia nchini humo iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Mexico

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Trump pia ametishia kuzuia raia wa Mexico walio Marekani wasitume pesa nyumbani

Rais Pena Nieto pia ametoa mwaliko kwa mgombea urais wa chama cha Democratic Bi Hillary Clinton.