Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ndege za Marekani zapelekwa kuwalinda wanajeshi Syria
Ndege za jeshi la Marekani zimepelekwa mji wa Hassakeh nchini Syria kuwalinda wanajeshi maalum wa Marekani walio mjini humo kutoka kwa mashambulizi ya angani ya Syria.
Makao makuu ya jeshi la Marekani yanasema kuwa ndege za Syria zilikuwa zikiondoka wakati ndege za Marekani zilipowasili.
Watu katika mji wa Kaskazini Masharikia wa Syria wanasema kuwa ndege za serikali zilishambuliwa mitaa yenye wakurdi kwa muda wa siku mbili zilizopita ambapo maelfu ya watu wanaripotiwa kuyakimbia makwao.
Hassakeh ni mji unaodhibitiwa na wapiganaji wa kurdi wa YPG.