Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Samsung: Kiwanda chetu hakina madhara ya kikemikali
Kampuni ya kielektroniki ya Samsung ya Korea Kusini, imekanusha taarifa zilizotolewa na familia ambazo zinataka fidia ya madhara ya viwanda.
Kundi la wafanyakazi limesema watu 76 wamefariki kutokana na kemikali za kiwanda ambacho kinatengeneza bidhaa za samsung.
Baadhi ya kesi zilimalizika lakini nyingine zinachelewa kutokana na mamlaka Kutaka kujua ni kemikali gani zimesababisha ugonjwa na vifo.
Samsung imesema kufichua taarifa kama hizo ni kutoa siri za kibiashara.
Imekanusha kuzuia taarifa kinyume na sheria.