Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Picha za kipekee za mazishi ya Papa Francis
Umati mkubwa ulikusanyika katika Jiji la Vatican tangu asubuhi kwa ajili ya mazishi ya Papa Francis, yaliyohudhuriwa na viongozi karibu kutoka kote duniani
Inakadiriwa watu 250,000 walikusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro na mitaa ya karibu kuona msafara wa mazishi.
Walinzi wa Uswisi wakiwa wamevaa sare zao zenye mistari ya njano, bluu na nyekundu wanafuatilia kwa karibu matukio Vatican. Mara nyingi wanajulikana kama "jeshi dogo zaidi duniani", kikosi hiki chenye watu 135 kimekuwa kikimlinda Papa kwa karne tano.
Papa Francis alieleza wazi matakwa yake kuhusu mazishi anayotaka katika wasia wake, akisema: "Kaburi liwe ardhini; bila mapambo maalum, likiwa na maandishi haya tu: Franciscus."
Kuna takriban Wakatoliki bilioni 1.4 duniani kote, wengi wao wakiwa bara la Amerika ingawa idadi ya watu wanaoongezeka kwa kasi zaidi katika Kanisa hilo barani Afrika. Wengi wao walikusanyika mbele ya runinga siku ya Jumamosi kutazama matukio Vatican.
Mara tu mazishi kumalizika, dekani wa Chuo cha Makadinali ana hadi siku 20 kuwaita makadinali Vatican kuanza mchakato wa kumchagua Papa mwingine mpya. Pia, kipindi cha maombolezo cha siku tisa, kinachojulikana kama Novemdiales, kinaaza.