Je, Marekani kuishambulia tena Iran?

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Donald Trump
Muda wa kusoma: Dakika 3

Iran haikuwa katika ajenda katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO huko The Hague, Uholanzi. Lakini karibu mijadala yote katika mikutano ya waandishi wa habari ilihusu Iran.

Pembeni, mijadala mikali pia ilifanyika kuhusu uhalali wa mashambulizi ya Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.

Rais wa Marekani Donald Trump amependelea kuwasilisha shambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran kwa washirika wake wa NATO kama mafanikio ya kihistoria.

Amesisitiza mara kwa mara kwamba ameweza kushughulikia moja ya kero kuu za nchi wanachama wa NATO katika Mashariki ya Kati kwa pigo moja.

Ingawa mashaka yaliibuka kuhusu msingi wa kisheria wa shambulio la Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran, Katibu Mkuu wa NATO Mark Rutte na viongozi wengine kadhaa wa nchi wanachama wa muungano huo waliunga mkono hatua hiyo ya Marekani.

Kinyume chake, Uturuki mwanachama wa NATO ilichukulia hatua ya Marekani kuwa kinyume na sheria za kimataifa. Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Kaya Kallas pia alisema hana uhakika kwamba shambulio la Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran ni kwa mujibu wa sheria za kimataifa.

Kando na kile Marekani ilifanya na mpango wa nyuklia wa Iran, wengi walitaka kuona mipango ya Donald Trump kwa mustakabali wa Iran.

Yaliyojitokeza katika hotuba za wajumbe wa Marekani na majadiliano katika mikutano ya kando ya NATO zaidi au kidogo yalifichua mipango ya Marekani kuhusu Iran

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kwanza, Marekani inapenda mazungumzo yaendelee. Donald Trump alisema kuwa wajumbe wa Iran na Marekani watakutana wiki ijayo.

Iran bado haijajibu kauli hii. Mahali na wakati halisi wa mazungumzo pia haijulikani. Bila shaka, Bw. Trump amesema kuwa mazungumzo hayo yatakuwa ya moja kwa moja na bila ya kuingiliwa na nchi ya tatu.

Kwa maneno mengine, njia ya mazungumzo, ambayo katika miaka ya hivi karibuni ilifanywa kupitia njia ya waamuzi wa Uropa au Omani, inabadilika.

Pili, kwa mtazamo wa Marekani, udharura wa mpango wa nyuklia wa Iran umeondolewa. Kwa hiyo, Marekani haina haraka ya kufikia hitimisho la mazungumzo hayo, kwa sababu kulingana na Bw. Trump, vituo vya nyuklia vya Iran vimeharibiwa kabisa.

Tatu, Marekani inaendelea kutumia sera ya shinikizo la juu, tu kwa mabadiliko ambayo haisisitizi tena kusimamisha uuzaji wa mafuta ya Iran kwa China.

Na nne, na muhimu zaidi, chaguo la kijeshi bado liko kwenye meza. Bw.Trump amesema iwapo Iran inataka kuanza tena kurutubisha madini ya uranium, Marekani haitasita kushambulia tena vituo vya nyuklia vya Iran.

Marekani inaendelea kutumia mbinu zile zile za awali, mchanganyiko wa mazungumzo na shinikizo la juu zaidi na uwezekano wa kutumia chaguo la kijeshi, chaguo ambalo sasa imetumia na inaamini limekuwa na ufanisi.