"Mwisho wa enzi"; Je, upi mustakabali wa Ronaldo?

Muda wa kusoma: Dakika 4

Kufuatia chapisho la utata kwenye mitandao ya kijamii, inaonekana kwamba Cristiano Ronaldo anapanga kuondoka Al-Nasr ya Saudi Arabia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 40 alijiunga na Al-Nasr Januari 2023 na mkataba wake na klabu hiyo unamalizika mwezi ujao.

Ronaldo aliifungia timu yake bao la kwanza katika kichapo cha 3-2 dhidi ya Al-Hilal, ambacho kiliisaidia kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Ligi ya Saudia. Lilikuwa bao la 800 kwa Ronaldo kwa klabu.

Baada ya kupoteza, Ronaldo aliandika kwenye X-Net: "Enzi hii imekwisha. Hadithi? Bado inaandikwa. Asanteni wote."

Swali sasa ni nini kitatokea kwa nyota huyo wa zamani wa Real Madrid na Manchester United na je atakuwepo kwenye michuano ya Klabu Bingwa Duniani mwezi ujao?

Pia unaweza kusoma

"Majadiliano ya Kombe la Dunia la Klabu"

Wiki iliyopita, Rais wa FIFA Gianni Infantino aliibua uwezekano wa Ronaldo kushiriki Kombe la Dunia la Vilabu kufuatia Al-Nasr kushindwa kufuzu kwa mashindano hayo.

"Ronaldo anaweza kuchezea moja ya timu katika Kombe la Dunia la Vilabu," Infantino aliambia kituo cha YouTube.

"Kuna majadiliano na vilabu kadhaa, kwa hivyo ikiwa klabu inaangalia hili sasa na ina nia ya kumsajili Ronaldo , nani anayejua?"

Michuano ya kombe la dunia la vilabu itakayofanyika nchini Marekani majira ya kiangazi ni mtihani mzito kwa FIFA. Ni toleo la kwanza la michuano hiyo kushirikisha timu 32.

Hata hivyo, idadi kubwa ya tiketi za mechi hizo hazijauzwa, ikiwa ni pamoja na mechi ya ufunguzi kati ya Inter Miami, ambayo ina Lionel Messi, na Al Ahly.

"Ronaldo anaweza kuchezea moja ya timu katika Kombe la Dunia la Vilabu," Infantino aliambia kituo cha YouTube.

"Kuna majadiliano na vilabu kadhaa, kwa hivyo ikiwa klabu inaangalia hili sasa na ina nia ya kumsajili Ronaldo ... nani anayejua?"

Michuano ya kombe la dunia la vilabu itakayofanyika nchini Marekani majira ya kiangazi ni mtihani mzito kwa FIFA. Ni toleo la kwanza la michuano hiyo kushirikisha timu 32.

Hata hivyo, idadi kubwa ya tiketi za mechi hizo hazijauzwa, ikiwa ni pamoja na mechi ya ufunguzi kati ya Inter Miami, ambayo ina Lionel Messi, na Al Ahly.

Ni timu gani inaweza kumsajili Ronaldo?

Timu chache duniani zinaweza kumudu mshahara wa Ronaldo. Alikua mwanasoka anayelipwa pesa nyingi zaidi katika historia alipojiunga na Al-Nasr miaka miwili iliyopita. Ronaldo anaripotiwa kuingiza takriban euro milioni 200 kwa mwaka.

Bila shaka, kuna uwezekano pia kwamba Ronaldo atasaini mkataba wa muda mfupi na klabu ya kucheza Kombe la Dunia la Klabu na kisha kuamua juu ya mustakabali wake.

Gazeti la Uhispania la Marca liliripoti wiki iliyopita kuwa klabu moja ya Brazil ilitoa ofa ya kumsajili Ronaldo.

Botafogo wanaoshiriki Kombe la Dunia la Vilabu, wanadaiwa kufanya mawasiliano na mshambuliaji huyo.

"Unatakiwa kusubiri zawadi tu wakati wa Krismasi, lakini akija huwezi kumkatalia nyota wa aina hiyo. Sijui chochote, nilijibu swali tu," alisema Renato Pavia, kocha wa timu hiyo.

"Lakini kama nilivyosema, makocha daima wanataka bora na Ronaldo ni mashine ya kupachika mabao hata katika umri huu. Katika timu inayounda fursa baada ya fursa, hiyo inafanya kazi vizuri."

Uwezekano wa uhamisho na sheria zilizobadilishwa

Dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi la Uingereza linaanza Juni 16 hadi Septemba 1. Hata hivyo, dirisha maalum litafunguliwa kwa timu zinazoshiriki Kombe la Dunia la Klabu kuanzia Juni 1 hadi 10.

FIFA imeunda haki hii maalum kwa timu katika Kombe la Dunia la Vilabu ili c

Kombe la Dunia la Klabu linaanza lini?

Michuano hiyo ambayo itaandaliwa na viwanja 12 kote Marekani, itaanza Juni 12. Jumla ya mechi 63 zitafanyika, huku fainali ikipangwa Julai 13 kwenye Uwanja wa MetLife

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla