Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Man Utd yasitisha mpango wake wa kumnunua Baleba – Tetesi za soka Ulaya Jumamosi
Manchester United haitaendelea na mpango wa kumnunua Carlos Baleba, mlinda mlango wa Manchester City Ederson anafikiria mustakabali wake na Newcastle wanataka kukamilisha dili la kumnunua Yoane Wissa wa Brentford.
Manchester United haitaendelea na mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Cameroon Carlos Baleba, 21, msimu huu wa joto, huku thamani ya Brighton ya pauni milioni 115 ikionekana kuwa juu sana. (Athletic - subscription required)
Kipa wa Manchester City Ederson, 31, anafikiria mustakabali wake katika klabu hiyo na uwezekano wa kwenda Galatasaray. Iwapo mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil ataondoka, City itataka kumsajili mchezaji wa Paris St-Germain Gianluigi Donnarumma, 26, huku nyota huyo wa Italia akipatikana. (Guardian)
Newcastle wako tayari kuendelea na harakati za kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa Brentford na DR Congo Yoane Wissa, 28. (Sky Sports)
Newcastle pia wameanza tena harakati za kutaka kumnunua mshambuliaji wa Paris St-Germain na Ureno Goncalo Ramos, 24, huku wakitafuta washambuliaji wawili msimu huu. (Mail)
Klabu ya Saudi Pro League, Al-Nassr iko mbioni kukamilisha dili la £25.8m kumsajili winga wa Ufaransa Kingsley Coman kutoka Bayern Munich. (Talksport)
Nottingham Forest wana nia ya kumsajili beki wa pembeni Rico Lewis, 20, huku Manchester City wakiwa tayari kumruhusu mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza kuondoka kwa malipo ya zaidi ya £30m. (Mail)
Kiungo wa kati wa Juventus na Argentina Nicolas Gonzalez, 27, anafuatilia uhamisho wa euro 30m (£26m) kwenda Atletico Madrid msimu huu wa joto. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)
Wolves wanakaribia kumsajili Verona na beki wa pembeni wa Cameroon Jackson Tchatchoua, 23. (Athletic - subscription required)
Sunderland wamekubali dili la kumsajili beki wa Paris St-Germain na Ufaransa Nordi Mukiele, 27, kwa pauni milioni 9.5 pamoja na nyongeza za pauni milioni 2.5. (Northern Echo)