Tetesi za soka Ulaya Jumamosi: Juventus yamtaka Zirkzee yamkataa Rashford

Chanzo cha picha, Getty Images
Juventus wamekataa nafasi ya kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na England Marcus Rashford, 27, lakini badala yake wanamtaka mshambuliaji mwenzake wa Mashetani Wekundu Joshua Zirkzee, 23, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Uholanzi. (Sun),
Manchester City huenda ikatafuta kuanzisha kipengele cha kutolewa cha Martin Zubimendi cha pauni milioni 50 na kiungo huyo wa kati wa Uhispania na Real Sociedad, 25, ili kuziba pengo la jeraha la Rodri mwenye umri wa miaka 28. (Football Insider)
Manchester City, Liverpool, Real Madrid na Paris St-Germain zote zinafikiria iwapo watamnunua kiungo wa kati wa Bayern Munich na Ujerumani Jamal Musiala, 21, ambaye thamani yake ni karibu £150m Januari. (Caught Offside)
Meneja Ruben Amorim ana matumaini Manchester United inaweza kumsajili fowadi wa PSG na Ufaransa Randal Kolo Muani, 26, Januari licha ya ushindani kutoka kwa Chelsea, Tottenham na Arsenal. (TeamTalks)

Chanzo cha picha, Getty Images
Wolves haitakaribisha ofa kwa fowadi wao wa Brazil Matheus Cunha, 25, mwezi Januari, huku Arsenal na Manchester United zikimwania. (Mirror)
Juventus wanatafuta dili la pauni milioni 20 kumsaini beki wa kati wa England Fikayo Tomori, 27, kutoka AC Milan. (La Gazzetta dello Sport)
Manchester City watakuwa na nia ya kumnunua mwezi Januari James McAtee, 22, huku Nottingham Forest, West Ham na Brentford, pamoja na Bayer Leverkusen na Fiorentina, zote zikiwa na nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa England chini ya miaka 21. (Telegraph – Subscription Required)
Mshambulizi wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 27, anaweza kukubaliana mkataba wa awali na Fiorentina mwezi Januari, huku Newcastle na West Ham pia wakimtaka. (TeamTalks)
Liverpool wako tayari kumuuza mlinda lango wa Jamhuri ya Ireland Caoimhin Kelleher, 26, kwa bei ifaayo msimu ujao, huku Newcastle wakifuatilia hali yake. (TeamTalks)

Chanzo cha picha, Getty Images
Winga wa Galatasaray na Ivory Coast Wilfried Zaha, 32, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Lyon, anaweza kulengwa na vilabu vya Ligi Kuu ya Soka. (Mail)
Miguel Almiron ataondoka Newcastle mwezi Januari huku vilabu vya Ligi ya Premia, MLS na Saudi Arabia zikiwa na nia ya kumnunua kiungo huyo wa kati wa Paraguay mwenye umri wa miaka 30. (Football Insider)
Manchester United inamtazama Royal Antwerp na mchezaji wa kimataifa wa Ubelgiji chini ya umri wa miaka 21, Senne Lammens, 22, wanapotathmini chaguo lao la muda mrefu la golikipa. (Telegraph – Subscription Required)
Timu ya La Liga, Leganes ina nia ya kumtuma mshambuliaji wa Ivory Coast anayecheza kwa mkopo Sebastien Haller, 30, kurudi Borussia Dortmund mwezi Januari. (Marca, in Spanish).
Imetafsiriwa na Seif Abdalla












