Jinsi wanasesere wa 'Labubu' walivyokuwa maarufu ulimwenguni

Muda wa kusoma: Dakika 5

Iwe unadhani ni wa kupendeza, wabaya au wa ajabu tu, kuna uwezekano kwamba umesikia kuhusu wanasesere wenye manyoya ambao wamekuwa maarufu ulimwenguni, Labubu.

Akiwa ametengenezwa kama mnyama, kiumbe huyo anayefanana na kibwengo kutoka kwa mtengenezaji wa vinyago vya China, Pop Mart sasa ananunuliwa kwa urahisi.

Na si haba zimeonakana na watu mashuhuri: Rihanna, Dua Lipa, Kim Kardashian na Lisa wa Blackpink. Watu wa kawaida wanapenda sana, kutoka Shanghai hadi London, foleni ndefu za kunyakua mwanasesere zimegonga vichwa vya habari, wakati mwingine huingia kwenye mzozo.

Kuvutia kwa ulimwengu na Labubu kumekaribia mara tatu faida ya Pop Mart katika mwaka uliopita na kulingana na wengine, hata ilitia nguvu Wachina, ambayo imeharibiwa na janga la uhusiano mbaya na Magharibi.

Kwa hiyo, tulifikaje hapa?

Unaweza kusoma

Labubu ni nini hasa?

Ni swali ambalo bado linawasumbua wengi na hata wale wanaojua jibu hawana uhakika kabisa wanaweza kuelezea.

Labubu ni mhusika wa kubuniwa na chapa. Neno lenyewe halimaanishi chochote. Ni jina la mhusika katika mfululizo wa vinyago vya "The Monsters" iliyoundwa na msanii mzaliwa wa Hong Kong Kasing Lung.

Vinyago vilivyotengenezwa kwa plastiki,masikio yenye ncha, macho makubwa na tabasamu linaloonesha meno tisa.

Watu walio na mitazamo tofauti mitandaoni wameshindwa kueleza kama ni vya kupendeza au vya ajabu.

Kulingana na tovuti rasmi ya muuzaji rejareja, Labubu "ni mwenye moyo mkunjufu na daima anataka kusaidia, lakini mara nyingi kwa bahati mbaya huwa kinyume chake".

Wanasesere wa Labubu wameonekana katika mfululizo kadhaa wa "The Monsters", kama vile "Big into Energy", "Have a Seat", "Exciting Macaron" na "Fall in Wild".

Nani anauza Labubu?

Sehemu kubwa ya mauzo ya Pop Mart yalikuwa yanaitwa 'blind box' ambapo wateja waligundua tu kile walichokuwa wamenunua walipofungua kifurushi.

Pop Mart ilianzisha mfululizo wa kwanza wa mauzo mwaka wa 2016, wakiuza wanasesere wa Molly, sanamu zinazofanana na za watoto zilizoundwa na msanii wa Hong Kong Kenny Wong.

Lakini mauzo ya Labubu ndiyo yaliyochochea ukuaji wa Pop Mart na mnamo Desemba 2020, ilianza kuuza hisa kwenye Soko la Hisa la Hong Kong. Hisa hizo zimepanda kwa zaidi ya 500% katika kipindi cha mwaka uliopita.

Pop Mart yenyewe sasa imekuwa muuzaji mkuu. Inaendesha zaidi ya mashine 2,000 za kuuza, au "roboshops", kote ulimwenguni.

Na sasa unaweza kununua wanasesere wa Labubu katika maduka, au mtandaoni, katika zaidi ya nchi 30, kutoka Marekani na Uingereza hadi Australia na Singapore, ingawa wengi wao wamesitisha mauzo hivi karibuni kutokana na mahitaji makubwa.

Mauzo kutoka nje ya China Bara yalichangia karibu 40% ya mapato yake yote mnamo 2024.

Ishara ya jinsi Labubu imekuwa maarufu, maafisa wa forodha wa China walisema wiki hii kwamba wamekamata zaidi ya wanasesere 70,000 bandia katika siku za hivi karibuni.

Mahitaji hayakuongezeka mara moja. Kwa kweli ilichukua miaka michache kwa vibwengo hao kuingia kwenye mkondo wa mauzo.

Je, Labubu ilipataje umaarufu duniani?

Kabla ya ulimwengu kugundua Labubu, umaarufu wake ulikuwa wa China pekee.

Labubu ilianza kuibuka baada ya janga la corona mwishoni mwa 2022, kulingana na Ashley Dudarenok, mwanzilishi wa kampuni ya utafiti inayolenga ChoZan.

Mitandao ya Kichina, ambao ni mikubwa na yenye ushindani, bidhaa nyingi umaarufu wake haushiki uwanda wa kimataifa. Lakini huyu alifanya na umaarufu wake ukaenea haraka katika nchi jirani ya Kusini Mashariki mwa Asia.

Fiona, anayeishi Canada, anasema alisikia habari za Labubu kwa mara ya kwanza kutoka kwa marafiki wa Ufilipino mwaka wa 2023.

Ndipo alipoanza kuzinunua, anasema anaziona kuwa za kupendeza, lakini umaarufu wake unaoongezeka ni mvuto mkubwa: "Kadiri inavyozidi kupata umaarufu ndivyo uhitaji unavyoongezeka.

"Mume wangu haelewi ni kwa nini mimi, mtu aliye na umri wa miaka 30, ninapenda sana kitu kama hiki."

Umaarufu wa Labubu uliongezeka mnamo Aprili 2024, wakati nyota wa K-pop mzaliwa wa Thailand Lisa alipoanza kutuma picha kwenye Instagram akiwa na wanasesere mbalimbali wa Labubu. Na kisha, watu wengine mashuhuri ulimwenguni waligeuza wanasesere kuwa jambo la kimataifa mwaka huu.

Mwimbaji Rihanna alipigwa picha akiwa na Labubu iliyowekwa kwenye begi lake la Louis Vuitton mwezi Februari.

Mshawishi wa mtandaoni, Kim Kardashian alionesha wanasesere wake 10 wa Labubu katika mtandao wa Instagram mwezi wa Aprili.

Na mwezi Mei, nahodha wa zamani wa soka wa Uingereza Sir David Beckham pia aliweka picha Instagram ay picha ya Labubu, aliyopewa na binti yake.

Sasa wanasesere wako kila mahali, mara kwa mara wanaonekana sio mtandaoni tu bali pia kwa marafiki, wafanyakazi wenza au wapita njia.

Beijing hakika imefurahishwa na matokeo. Shirika la habari la serikali Xinhua linasema Labubu "inaonyesha mvuto wa ubunifu, ubora na utamaduni wa Kichina katika lugha ambayo ulimwengu unaweza kuelewa", huku ikimpa kila mtu fursa ya kuiona "China tulivu".

Labubu inaendelea kuongeza wafuasi kwenye mitandao ya kijamii huku mamilioni ya watu wakitazama wamiliki wapya wakibatilisha ununuaji.

Mojawapo ya video maarufu zaidi, iliyochapishwa mnamo Desemba, inaonesha wahudumu wa usalama wa uwanja wa ndege wa Marekani wakijibanza wakizunguka sanduku la Labubu la msafiri ambalo halijafunguliwa ili kujua ni mwanasesere yupi aliye ndani.