Kitu kisicho cha kawaida chapatikana katika ufuo wa bahari wa Japan

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kitu kisicho cha kawaida chapatikana katika ufuo wa bahari wa Japan

Kitu kisicho cha kawaida chenye umbo la mvingo kicholisombwa na maji kwenye ufuo wa bahari huko Japan, likiwashangaza wenyeji na kuzua uvumi ulioenea, limeondolewa, kulingana na vyombo vya habari vya ndani.

Picha zilionyesha mashine nzito ya kunyanyua ikichukua tufe kubwa.

Maafisa wa eneo la Hamamatsu walisema kuwa itahifadhiwa "kwa muda fulani" kisha "kutupwa".

Lakini wengi pia wamehoji kwa nini maafisa wa Japan hawajajitokeza na kusema wazi ni nini.

Kitu hichokisicho cha kawaida - kilichopewa jina la "yai la Godzilla", "boya la kuhama" na "kutoka anga za juu" - kulianza mapema wiki hii baada ya polisi wa eneo hilo kuwaarifu walipoona kitu kisicho cha kawaida kwenye ufuo.

Polisi, na hata kikosi cha mabomu, walitumwa kuangalia kitu hicho.

Kugunduliwa kwa chuma kikubwa cha mviringo kinachofanana na mpira wa miguu katika mji wa pwani ya Japan wa Hamamatsu, takriban kilomita 200 kusini magharibi mwa Tokyo, kumezua wimbi kubwa la uvumi.

Mamlaka za mitaa, polisi na kikosi cha mabomu walitumwa kwenye ufukwe wa Enshuhama kuchunguza kitu hicho kisichojulikana.

Wamegundua tu kwamba chuma hicho cha mvirongo hakina lolote ndani yake na hakina tishio lolote, huku wengine wakishuku kuwa inaweza kuwa aina ya boya.

Wenyeji waliovutiwa tayari wamekuja na majina machache ya kuupatia mpira huo kama vile "yai la Godzilla" , "mooring buoy" na kitu cha "anga ya nje".

Kisichojulikana

Televisheni ya umma ya Japani NHK ilionyesha picha za maafisa wawili kwenye ufuo wa Enshuhama wakitazama tufe la chuma lenye kutu, ambalo kipenyo chake ni takriban mita 1.5.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wakuu walizingira mahali hapo, ingawa wanakataza kuwa mpira huo unaweza kusababisha hatari.

Ni Jirani mmoja ambaye alitoa taarifa kwa polisi mara ya kwanza baada ya kuona kitu hiki kisicho cha kawaida kwenye ufuo wa pwani.

Mamlaka ilizingira eneo hilo na kufanya uchunguzi wa X-ray, ingawa haya hayakuonyesha mengi, kando na kuthibitisha kwamba kitu hicho hakina hatari yoyote.

Mwanariadha ambaye alikuwa akikimbia ufukweni alikiri kwa vyombo vya habari vya ndani kwamba alishangazwa na kitu hicho alichodai kwamba ulikuwa katika eneo hilo kwa muda.

"Nilijaribu kusukuma lakini haikusogea," aliambia NHK.

Mamlaka za mitaa zilionyesha kuwa watakiondoa kitu hicho hivi karibuni.

Mgogoro wa kisiasa

Maelezo ya video, Mpira mkubwa wa ajabu uliopatikana kwenye ufuo wa bahari kusini magharibi mwa Tokyo

Ugunduzi kama huo mara chache huibua mashaka katika nyakati za kawaida, lakini umekuja wakati ambapo kuna wasiwasi juu ya vitu visivyojulikana kufuatia kudunguliwa kwa puto linaloshukiwa kuwa la kijasusi la China na Marekani mapema mwezi huu.

Jumatano iliyopita, Japan iliiarifu China kuhusu kutoridhika kwake kutokana na tuhuma za kugundua puto za uchunguzi kwenye anga yake angalau mara tatu tangu 2019.

Ilikuwa ni tuhuma ya kwanza ya aina yake kutoka Tokyo dhidi ya Beijing, ambayo ilikanusha kutekeleza majukumu ya kijasusi.

Mawaziri wa ulinzi wa nchi hizo mbili walikutana Jumatano katika mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu ya usalama wa nchi hizo mbili katika kipindi cha miaka minne.

Pande zote mbili zilikubali kufanya kazi ili kupata nambari ya simu ya mawasiliano