Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Uganda ilivyokabiliana na milipiko iliyopita ya ugonjwa wa Ebola
Na Ambia Hirsi
Uganda imekumbwa na mlipuko wa Ebola mara nne tangu virusi hivyo kugunduliwa kwa mara ya kwanza. Hata hivyo, ikilinganishwa na Afrika Magharibi, taifa hilo la Afrika Mashariki limeonyesha uwezo mkubwa katika na haraka kudhibiti ugonjwa huo.
Mwaka 2000 na 2001, karibu watu 425 nchini Uganda waliambukizwa, miaka minne baadaye watu 149 waliambukizwa virusi hivyo. Katika miaka iliyofuata, milipuko mingine miwili ilirekodiwa nchini Uganda lakini jumla ya watu walioambukizwa virusi hivyo ilikuwa zaidi ya 30.
Kwa wafanyikazi wengi wa afya ya umma nchini Uganda, kukabiliana na milipuko ya magonjwa sio jambo geni.
Hii ni kwa sababu nchi imekuwa katika njia za kujitayarisha na kujibu kwa muda mrefu na mfumo wake wa milipuko ya magonjwa umekuwa ukiwekwa kwenye mizani mara kwa mara kwa miaka kadhaa sasa.
Uganda imekumbwa na milipuko minne ya Ugonjwa wa Ebola (EVD) katika miaka ya 2,000, 2014, 2017 na 2018.
Kufikia wakati Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilipotangaza COVID-19 kuwa janga la kimataifa mnamo Machi 11, 2020, Uganda ilikuwa imedhibiti ugonjwa wa Ebola katika wilaya ya Kasese kwenye mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kuashiria Uganda, nchi ilikuwa bado katika hali ya tahadhari kwa kutarajia maji kutokea kutoka DRC ambako EVD ilikuwa bado inaendelea.
Tayari Rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni amesema hakuna haja ya kuweka vikwazo katika maeneo hatarishi ya Ebola katika eneo la kati kwa sababu ugonjwa huo unaosababishwa na virusi hautokei hewani.
Mlipuko mkubwa zaidi na mbaya zaidi ulikuwa wa mwaka 2000 ambao ulisababisha vifo vya watu 224 na wengine 425 kuambukizwa virusi vya ugonjwa wa Ebola.
Katikati kipindi hicho Uganda pia hiyo pia ilikuwa inakabiliwa na milipuko ya magonjwa mengine kama Marburg, Homa ya Crimean Congo Hemorrhagic, Homa ya Manjano, Rift Valley Fever, Avian Influenza na surua miongoni mwa mengine kulingana na ripoti ya ya mwaka 2020 ya Shirika la Afya Duniani.
"Maambukizi ya awali wakati mwingine huwa vigumu kutambuliwa na huchukua miezi kadhaa kabla ya kubainishwa. Hali hiyo ilisababisha msururu kutokea kwa msururu wa maambukizi kutokea," alisema Trevor Shoemaker, mtaalamu wa virusi anayefanya kazi katika Taasisi ya Utafiti wa Virusi vya Uganda katika mradi wa pamoja na Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Marekani.
Waganda wanafahamu Ebola
Kwa sababu Uganda tayari ina uzoefu na milipuko mikubwa ya Ebola, watu walio na na taarifa za kutosha na inashirikiana na vituo vya matibabu. "Tofauti na baadhi ya jumuiya au tamaduni za Afrika Magharibi, Uganda iko wazi sana kwa kuwa wanataka kuripoti kesi za (Ebola) na sio kuzificha," Shoemaker alisema.
"Waganda wanawasilisha ripoti kuhusu watu wanaowashuku wana dalili za Ebola kwa sababu wanataka kuzuia."Shoemaker alisema. Maafisa wa afya walikuwa hawana matatizo ya kutambua wagonjwa na wale waliokuwa wakitafuta matibabu."
Katika nchi ambazo zimewahi kupambana kudhibiti Ebola, imani katika mfumo wa afya iko chini. Hili si jambo la kushangaza kwa sababu mlipuko wa Ebola inaweza kulemaza miundombinu ya afya ya mataifa husika.
Kwa mfano wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone kuanzia 1991 hadi 2002, maelfu ya watu wakiwemo madaktari na wauguzi walikimbia nchi.
"Kuna wafanyakazi wachache sana wa ndani wenye mafunzo. Hawawezi kushughulikia ipasavyo mgogoro huu," alisema Katja Ment, mratibu wa Afrika wa shirika la misaada, Madaktari wa Ujerumani, walikuwa wakisaidia hospitali nchini Sierra Leone, mojawapo ya nchi zilizoathirika zaidi. kutokana na janga hilo.
Ebola ya Sudan
Uganda ina uzoefu katika kukabiliana na ugonjwa wa Ebola na mlipuko ya wa ebola ya Sudan, na hatua muhimu kuelekea udhibiti wake. Mlipuko huu wa sasa ni wa kwanza wa ugonjwa wa Ebola uliosababishwa na virusi vya Sudan nchini Uganda tangu 2012.
Kulingana na ainisho ya Kimataifa ya Magonjwa ya Virusi vya Filovirus (ICD-11) iliyotolewa Mei 2019, ugonjwa wa Ebola sasa umeainishwa kulingana na virusi vinavyosababisha.
Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Sudan unaitwa milipuko ya Ugonjwa wa Virusi vya Sudan (SVD).
Kabla ya Mei 2019 virusi vyote vinavyosababisha ugonjwa wa Ebola viliwekwa pamoja.
Kulingana na matokeo ya vipimo vya maabara, mlipuko wa sasa wa ebola nci Uganda unasababishwa na virusi vya Sudan.
Virusi vya Sudan viliripotiwa kwa mara ya kwanza kusini mwa Sudan mnamo Juni 1976, tangu wakati huo virusi hivyo vimeibuka mara kwa mara na hadi sasa, milipuko saba iliyosababishwa na SUDV imeripotiwa, minne nchini Uganda na mitatu nchini Sudan.
Makadirio ya uwiano wa vifo vya kesi za SVD umetofautiana kutoka 41% hadi 100% katika milipuko iliyopita.
Kuzuia maambukizi
Ebola ni mojawapo ya virusi hatari zaidi ulimwenguni lakini haiambukizwi kupitia hewa, hivyo basi huwezi kuambukizwa Ebola kama homa ya kawaida.Madaktari wanasema kuepuka Ebola ni rahisi sana iwapo mtu atafuata tahadhari hizi muhimu zaidi:
1. Sabuni na maji
Nawa mikono kila baada ya shughuli yeyote kwa kutumia sabuni na maji safi- na utumie taulo kujikausha.Hili huwa jambo gumu kwa wanaoishi kwenye makazi duni, na walio vijijini ambako aghalabu maji safi hayapatikani moja kwa moja- lakini ni mbinu iliyothibitishwa ya kuua virusi vya Ebola.
2. Hakuna kugusana
Iwapo unashuku kuwa mtu ana Ebola, usimguse.Inaokena kuwa si maadili mema unapoona unaowapenda wakihisi uchungu na unataka kuwakumbatia na kuwahudumia, lakini maji maji ya kimwili- mkojo na kinyesi, matapishi, kamasi, mate, machozi, na mbegu za kiume na majimaji ya uke- vyote huweza kueneza Ebola.
Dalili za mtu aliyeugua ni joto mwilini, maumivu kwa misuli na viungo, vidonda kooni, kuumwa na kichwa, na uchovu- kufuatiwa na kichefuchefu, kutapika, na kuharisha, ambapo mtu huweza kutoa damu pia.
3. Epuka miili ya wafu
Iwapo unadhani mtu amefariki baada ya kuugua Ebola, usiguse mwili wao, hata kama ni mila au desturi ya maziko.
4. Usile nyama ya porini
Epuka kuwinda, kugusa, au kula nyama ya porini, kwa mfano popo, nyani na sokwe, kwani wanasayansi wanaamini kuwa hiyo ndiyo chanzo cha maambukizi kwa binadamu.