Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Daniel Khalife: Mshukiwa wa ugaidi alitorokaje jela?
Maelezo ya kutoroka kwa Daniel Khalife yanazua maswali mazito kuhusu kile kilichotokea kuhusu usalama katika HMP Wandsworth.
Wizara ya Sheria haina uwezekano mkubwa wa kuthibitisha hadharani maelezo yote.
Ikiwa kutoroka kulihusisha kutumia mwanya au mbinu mahsusi ya usalama, jambo la mwisho ambalo wakuu wa gereza wanahitaji ni kuhakikisha wafungwa wengine hawapati wazo sawa.
Lakini kile tunachojua kuhusu tukio hili linawasumbua sana.
Gereza la kihistoria
HMP Wandsworth ni gereza la Kitengo B kusini-magharibi mwa London
Gereza la Wandsworth ni mojawapo ya magereza maarufu nchini Uingereza - na ya kutisha - ya Victoria. Sio mahali pazuri kuishi kwa siku, achana na miezi au miaka.
Vitengo vya gereza hilo zamani likiitwa Heathfield and Trinity vina vipaza sauti viwili.
Majiko yamewekawa katikati ya vipaza sautu hivi, kwenye barabara ya kufikia gari ambalo liko kaaribu na eneo kuu la usalama na lango.
Hilo si jambo la kawaida kuwapata , kwani wanahitaji kupokea bidhaa kila siku - na wakuu wa usalama wanahitaji kupunguza mwendo wa magari.
Tunaweza kuona kutoka kwenye picha za satelaiti kwamba majiko ya gereza hilo pia yako karibu na kontena za taka za viwandani - kwa hivyo litakuwa eneo lenye msongamano mkubwa wa magari kila siku - na kila harakati huongeza kazi nyingi kwa walinzi wa usalama wa gereza.
Magari ya mizigo yanayofika Wandsworth kwanza yanapitia lango la usafirishaji wa umma, kisha yasimame kwenye "kifunga hewa" kabla ya lango la pili.
Hilo ndilo eneo la kwanza ambapo kunaweza kuwa na ukaguzi wa kina wa usalama.
Timu za usalama zimefunzwa kusaka maeneo ya chini ya gari lenye vioo na wanapaswa kuangalia sehemu ya juu ya gari na, bila shaka, ndani yake pia.
Safu ya pili
Mara tu ukaguzi huo unapokamilika, magari husogea kupitia lango la pili, ndani ya kuta za gereza, zikiwa na alama ya chungwa kwenye mchoro wetu, na kisha kusimama tena.
Eneo hili hunapaswa kuwa chini ya uangalizi wa mara kwa mara na hakuna mtu anayepaswa kuingia bila ruhusa na kusindikizwa.
Ni wakati tu lango la tatu linapofunguliwa, kati ya eneo lisilo na uchafu na uzio wa ndani, ndipo magari hatimaye hufika maeneo ya gereza ambapo yanaweza kufikiwa na wafungwa.
Lakini hata katika eneo hilo magari hayawezi kuzunguka kwa uhuru - kuna milango zaidi ya usalama zaidi ya kizuizi cha jikoni.
Hiyo ina maana magari ya kubebea mizigo au malori yanaweza kwenda tu kadri yanavyoruhusiwa ili kupunguza hatari ya kusafirisha bidhaa zisizo halali ndani - au kuwasafirisha wafungwa nje.
Hatua hizo zote za usalama na ukaguzi hufanyika baada ya magari kuondoka. Nimetazama hili ikitokea zaidi ya mara moja jela na utaratibu huu huchukua muda.
Kwa hivyo tukibadili utaratibu huo, tunaweza kusema kwa uhakika kwamba Bw Khalife aliweza kukwepa kugunduliwa kwa angalau matukio mawili maalum kwani gari alimojificha lilipitia safu mbili na milango mitatu.
Jambo moja ambalo polisi wanalichunguza kwa sasa ni iwapo wanaweza kujua ni muda gani Khalife alikuwa amejificha chini ya lori kabla ya kuondoka.
Mapungufu zaidi
Lakini mapungufu yanayodaiwa hayaishii kwa ukaguzi wa gari.
Bw Khalife na lori waliondoka saa 7.32 asubuhi - na hakutangazwa na wakuu wa magereza kwa dakika 20 zaidi. Dakika nyingine 25 zilipita kabla ya polisi kuitwa.
Walifanikiwa kulifuatilia lori hilo na kulisimamisha saa 8.37 asubuhi zaidi ya maili tatu. Kufikia wakati huo, Bw Khalife alikuwa ameondoka muda mrefu - akiwa amevaa kama mpishi.
Kamanda Dominic Murphy, mkuu wa kukabiliana na ugaidi katika Scotland Yard, amesema kuwa Bw Khalife lazima awe amepanga kutoroka kwake - na kutokana na mafunzo yake ya kijeshi alikuwa na ujuzi - na ujuzi ambao ungemsaidia kutoroka.
Ian Acheson, mkuu wa zamani wa usalama huko Wandsworth na mkuu wa kitaifa wa magereza , anasema kutoroka ni kushindwa kwa huduma ya magereza kutokana na idadi ya ukiukaji wa taratibu za usalama.
Waziri wa sheria wa Uingereza Alex Chalk amethibitisha kuwa kamba zilipatikana chini ya gari hilo. Hii inaibua maswali kadhaa:
- Je, Bw Khalife alipataje kitu chenye nguvu cha kutosha kushika uzito wake?
- Alihitaji kujifunga chini kwa muda gani?
- Je, alikuwa chini ya gari kwa muda gani bila kutambuliwa kabla ya kuondoka?
- Je, kulikuwa na aina fulani ya muundo maalum wa magari ambayo Bw Khalife alitumia kujificha?
- Je, hii sasa inaleta hatari ya kutoroka zaidi kwa wafungwa wengine?
Maswali hayo yatapelekea kufanyika kwa uchunguzi ili kujua kama alikuwa na usaidizi - pengine kutoka ndani ya gereza.
Kazi ya jikoni "Plum".
Bw Khalife pia alikuwa katika hali isiyo ya kawaida ya kuwa mfungwa anayesubiri kusikilizwa kwa makosa makubwa - lakini pia, kama Mkuu wa zamani wa gereza John Podmore alivyoiambia BBC .
Maafisa wa magereza huchagua kwa uangalifu sana ni nani anafaaa kufanya kazi za jikoni kwa sababu zimejaa visu na vifaa vingine hatari.
Kwa sababu ya kazi yao ya usafirishaji wa chakula , wao pia wanauwezekano wa kutoroka.
Kwa kawaida, wafungwa waliochaguliwa kufanya kazi jikoni huwa wana rekodi ya kuaminika.
Kwa hivyo kwa nini mtu anayekabiliwa na mashtaka ya ugaidi alifanya kazi jikoni? Hilo ni moja tu ya maswali ambayo Bw Chaki anataka klijibiwe.
Amewaambia wabunge alitaka kujua ni nani alikuwa akisimamia jiko na lango - na ni itifaki gani za usalama walikuwa wakifuata.
Waziri wa sheria aliomba ripoti ya awali ifikapo mwisho wa wiki - na ameahidi kutakuwa na uchunguzi huru zaidi.