Tetesi za soka Ulaya: Bayern kutoa £43m kumsajili Bruno wa United

Chanzo cha picha, Getty Images
Bayern Munich wako tayari kutoa takribani euro milioni 50 (£43m) kwa Manchester United ili kumsajili kiungo wa Ureno na nahodha wa klabu Bruno Fernandes, 31. (Fichajes)
Winga wa Ghana Antoine Semenyo, 25, anapendelea kuhamia Liverpool badala ya Manchester City au Manchester United iwapo ataondoka Bournemouth mwezi Januari. (Guardian)
Chelsea wanapanga kutafuta wanunuzi wa mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, kwa kuwa hatabaki Bayern Munich zaidi ya kipindi chake cha mkopo. (CaughtOffside)
Kipa wa Denmark Filip Jorgensen, 23, anataka kuondoka Chelsea baada ya kukata tamaa na nafasi yake kama kipa wa pili, ingawa klabu italazimika kuidhinisha kuondoka kwake kwani ana mkataba hadi 2031. (Teamtalk)
Liverpool wamearifiwa juu ya uwezekano mkubwa kwamba beki wa Inter Milan na Italia Alessandro Bastoni, 26, anaweza kuwa tayari kuhamia Anfield mwaka 2026. (Teamtalk)
Hata hivyo, Barcelona pia wanamvizia Bastoni, pamoja na beki wa Manchester City na Croatia Josko Gvardiol, 23. (Mundo Deportivo)

Chanzo cha picha, Getty Images
Aston Villa wanaendelea kumfuatilia kipa wa Barcelona na Ujerumani Andre ter Stegen, 33, ambaye anataka muda wa kucheza mara kwa mara kabla ya Kombe la Dunia la mwaka ujao. (Mundo Deportivo)
Winga wa Athletic Club na Hispania Nico Williams, 23, ambaye anavivutia vilabu vya Liverpool, Arsenal na Chelsea, anataka kujiunga na Real Madrid. (Football Transfers)
Arsenal wamewasiliana na wawakilishi wa kiungo wa Lille Ayyoub Bouaddi kuhusu uhamisho wa Januari wa euro milioni 45 (£39.4m), huku Manchester City, Manchester United na Liverpool pia wakimvizia kiungo huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 18. (Mirror)
Beki wa kulia wa Leeds United Jayden Bogle, 25, anasakwa na Everton baada ya maskauti wao kuvutiwa na kiwango chake kwenye Ligi Kuu msimu huu. (Football Insider)
AC Milan wanafuatilia mpango wa kumchukua kwa mkopo mshambuliaji wa Arsenal Gabriel Jesus, 28, huku Mbrazil huyo akihangaika kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara. (Gianluigi Longari)















