Je, hatua kubwa za binadamu kwenda anga za mbali zitafaulu?

Kuna mpangilio mpya unaoibuka katika anga za mbali – kinyang’anyiro baina ya Marekani na Uchina. Lakini kutokana na uvumbuzi wa anga za mbali kuwa ghali, hata mataifa haya yenye nguvu zaidi duniani hayataweza kufanya uvumbuzi huo peke yao.

 Changamoto kubwa za kiufundi na za gharama zimekuwa zikitajwa kukwamisha malengo na si tu la watu kuishi na kufanya kazi katika sayari nyinyine, labda kwa miaka kumi - lakini katika dunia iliyogawanyika ambamo utashi wa kimataifa ni haba, je yanaweza kutekelezeka?.

 Kurejea kwa Nasa mwezini kumeanza kwa mpango wake unaofahamika kama Artemis. Safari zaketatu za kwanza zimefanikiwa kuanzishwa. Ndege hii isiyokuwa na rubani ilipima kwamba roke kwamba roketi na teknolojia zinafanya kazi.

Safari ya pili itawachukua binadamu mbali zaidi katika anga za mbali kuliko walivyowahi kwenda kabla na safari ya tatu itawaweka katika itawapeleka wataalamu wa anga za mbali hadi kwenye mwezi kwa wiki, ambako watafanya majaribi. Lengo la muda mrefu ni kuutumia mwezi kama kituo cha kuruka kuifikia sayari ya Mars.

Lakini mpango huo unakadiriwa kugarimu dola bilioni 93 (£76bn), kiasi ambacho ni mzogo mzito kwa walipa kodi wa Marekani, ambao tayari wanakabiliwa na mbinyo wa kiuchumi.

China imefanikiwa operesheni yake kikamilifu katika kituo cha anga za mbali cha Tiangong, katika uzio kwa muda uliopangwa.

Mpango wa China wa anga za mabali ulipeleka vyombo vyake katika Mwezi na karika sayari ya Mars .

Inapanga kuanzisha utafiti unaojiongoza katika kituo chake cha angaza mbali Mwezini ifikapo 2025 na halafu wana anga wake watue kwenye sakafu ya mwezi 2030.

Kuwaweka wataalamu wa anga za mbali katika Mwezi ni jambo ambalo tayari limefanyika kabla lakini hatua inayofuata, ya kuelekea Mars, ni ngumu zaidi.

Kihistoria mataifa yenye nguvu zaidi duniani yamekuwa yakionyeshana ubabe katika uelewwa wa juu ya dunia . Marekani na Urusi zilishindania utawala katika anga za mbali katika miaka ya 1950 na 1960.

Urusi ilimuweka mtu wa kwanza katika uzio (obit) kwa mara ya kwanza . Na Wamarekani wakamuwezesha mtu wa kwanza kutua katika anga za mbali na kupandisha bendera yao katika Mwezi miaka michache baadaye.

Katika miaka ya 1970 enzi bora ya ushirikiano ilianzishwa na kuweza kufanikisha kujengwa kwa kituo cha Kimataifa cha anga za mbali (ISS), kilichoanza utendaji katika mwaka 1998.

Pamoja na nchi washirika nyingine 13, nchi hizo zenye mamlaka zaidi duniani zilijenga kile ambacho kwa sasa ni jengo kubwa zaidi katika anga za mbali. Halimilikiwi na taifa lolote, na kila taifa linategemea jingine kufanya kazi yake katika anga za mbali.

 Wanaanga wa marekani n awa Usovieti walisalimiana kwa mikono katika uzio(obit), na hivyo kutoa fursa ya enzi bora katika ushirikiano katika anga za mbali baina ya mataifa hayo yenye nguvu.

Ilikuwa ni ishara ya kile ambacho binadamu wanaweza kufanikisha iwapo nchi zitaweka kano tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.

 Lakini uhalisia kilikuwa ni kitu ambacho ni tofauti. Marekani iliizuia China kuwa mshirika katika ISS, kwahiyo Wachina walikwenda peke yao.

 Hivi karibuni, katika kipindi cha wiki za uvamizi wa Ukraine, mataifa yaliacha kufanya kazi na Urusi. Safari mbili za ushirikiano za kuelekea katika Mwezi baina ya shirika la anga za mbali la Ulaya (ESA) na Urusi zimesitishwa, sawa na mradi wa wa pamoja wa Mars Rover ambao lengo lake lilikuwa ni kutafuta dalili za maisha katika sayari nyekundu.

Bado kazi ya utafiti wa sakafu ya mwezi na ushirikiano unaendelea katika kituo cha anga za mbali cha kimataifa, ambako mataifa ya Magharibi yanapaswa kufanya kazi na Urusi katika uzio.

Lakini kile kilichotokea wakati mmoja katika ISS kinamalizika mwaka 2030?

Marekani na Ulaya bado hata zinapata mafunzo katika kituo cha Urusi cha anga za mbali cha HQ, katika Star City.

Juliana Suess, mchambuzi wa sera ya anga za mbali na mshauri katika taasisi ya Royal United Services mjini London anasema Urusi ni nchi mshirika mwenye machache ya kusaidia kuliko ilivyowahi kufanya awali kwasababu ya kupitwa na wakati kwa teknolojia yake.

Alielezea uwezekano wa taifa hilo kuwa la kwanza kuondoka katika anga za mbali.

Kufeli kwa Urusi kunakuja wakati ambapo mpango wa Uchina wa anga za mbali ukiendelea kukua kwa kasi. Katika kipindi cha miaka kumi iliyopita imeweza kutuma maroketi zaidi ya 200, hata kama matumizi ya kifedha ya Marekani katika anga za mbali yanaifanya Uchina kuonekana badoni ndogo katika anga hizo.

Nchi sabini na mbili kwa sasa zina mipango yao ya kibinafsi ya anga za mbali kwasababu haziwezi kuacha nyuma katika kile ambacho sasa kimekuwa ni mashindano ya teknolojia ya anga za mbali.

Mabilionea wanaotaka uwepo wa binadamu katika anga za mbali

Anga za mbali ni sehemu muhimu kwa ajili ya maisha yetu ya kila siku . Tunahitaji kutegemea setilati kwa ajili ya utabiri wa hali ya hewa , mawasiliano, usafirishaji wa pesa za benki, bila kusahau kuwa anga za mbali ni nyenzo muhimu katika upelelezi wa mataifa .

Na shughuli zinaendelea kuwa nyingi hapa. Katika mwaka mwaka 2021 setilaiti takriban 5,000 zilitumwa katika anga za mbali. Ulirudi nyuma miaka 20, setilaiti 800 zilitumwa huko kila mwaka.

Anga za mbali ni biashara ghali na ngumu kiufundi . hakuna nchi mmoja inayoweza kuifanya peke yake. Ushirika mpya unaundwa, huku ukiwemo ule wa mabilionea wanaojiunga katika biashara hii.

Kampuni ya Elon Musk , SpaceX, tayari inawapeleka wasafiri katika uzio. Mjasiriamali bilionea anashusha gharama kwa kutumia roketi zinazoweza kutumika tena. Jeff Bezos anataka kujenga kituo cha kibiashara cha kimataifa cha anga za mbali katika uzio, atakachokiita, Orbital Reef.

Mtaalamu wa anga za mbali wa kwanza nchini Uingereza,Helen Sharman, ambaye alikuwa katika safari ya kuelekea kituo cha anga za mbali cha Usovieti - Mir katika mwaka 1991, anaamini kwamba uhasama wa sasa wa kimataifa unaweza kugubikwa na kuingia kwa sekta binafsi katika anga za mbali.

Matarajio ya faida ya na uvumbuzi wa kisayansi vinachochea ushirikiano. Makampuni ya kibinafsi yanaweza kusaidia kuleta ushirikiano mpya lakini ni lazima yaheshimu sheria za nchi zao.

Wakati nchi zilipoyawekea makampuni ya Urusi vikwazo katika mwaka 2022 , makampuni yalilazimika kuvunja mikataba na Urusi.

 Dr Josef Aschbacher, ambaye ni mkuu wa Shirika la anga za mbali la Ulaya , ameazimia kuendelea kuiweka Ulaya katika kinyang’anyiro kipya cha anga za mbali. Hivbi karibuni aliowezesha kuongezwa kwa ufadhili wa pauni bilioni 2 ($2.4bn) , licha ya uhaba wa fedha unaozikabili serikali za Ulaya.

 "Anga za mbali ni moja ya sekta ambazo zinapanuka kwa kasi kubwa na za haraka zaidi sasa kuliko ilivyokuwa katika miongo michache iliyopita. Hatuwezi kuipoteza ," aliiambia BBC. "Tunaihitaji kusema kweli.

Itakuwa ni nchi zinazoongoza uvumbuzi wa siku zijazo. Lakini changamoto zitayalazimisha mataifa kujumuika kwa pamoja kama kikundi kimoja au "shirikisho" la nchi kushirikishana taarifa na kushindana na mashirikisho mengine.

Shirika la anga za mbali la Ulaya limefanikiwa kufanya hili kwa miaka mingi.

Sheria mpya kwa ajili ya anga za mbali

Lakini kile kinachoweza kurudisha nyuma mafanikio makubwa yajayo katika sayari nyingine ni sheria za kimataifa zinazoongoza anga za mbali.

Mkataba bora wa anga za mbali unaofahamika kama " Outer Space Treaty" haujafanyiwa marekebisho tangu uliposainiwa katika mwaka 1967, wakati nchi 31, ikiwemo Marekani na Muungano wa Usovieti zilipoahidi kutokuwa na silaha za nyuklia katika anga za mbali.

Sheria mpya za kudhibiti wa unyonyaji wa kibiashara wa mwezi, Mars na anga nyingine za mbali zilianzishwa mwaka 1979 na Umoja wa Mataifa lakini, Uchina, Marekani na urusi zilikataa kuisaini.

Josef Aschbacher wa ESA anaamini kuwa kinyang’anyiro kipya cha anga za mbali kitazuiwa hadi mkataba mpya wa anga za mbali utakapokamilishwa.