Roger Federer kustaafu:Nguli wa Uswizi wa tenisi ambaye alifikia kilele cha mchezo huo

"Lazima ujiulize kama amnatoka sayari moja."

Katika kipindi cha miaka 20 iliyopita hakuwa Novak Djokovic pekee ambaye alijiuliza ikiwa Roger Federer alikuwa ameumbwa na kushushwa kwenye Uwanja wa tenis na miungu ya tenisi.

Uwezo wake ni mkubwa zaidi katika mchezo.

Federer, ambaye ametangaza kustaafu baadaye mwezi huu, pia alikuwa mmoja kati ya wachache ambao wanaweza kukuvutia na kuushika moyo wako, huku akionekana kufikia ubora stahiki.

Wengine wanaweza kuwa wameshinda mataji zaidi lakini kwa wengi Federer alikuwa anacheza katika ubora wake, gwiji huyo wa Uswizi amepata mashabiki wengi tofauti na mtu yeyote kabla yake.

Ustadi wa Federer mwenye umri wa miaka 41 ulipatikana kwenye viwanja vya tenis katika Kituo cha Kitaifa cha Tenisi cha Uswizi huko Basel.

Kama kijana alikuwa na talanta ya hali ya juu lakini alijulikana kwa hasira yake. Inasemekana alipewa adhabu ya kusafisha vyoo baada ya kurusha racket ( kifaa cha kupigia mpira wa tenis) akiwa na umri wa miaka 16.

Inaweza kuwa kumbukumbu ya mbali kwa sasa lakini tabia ya Federer ya hasira mbaya iliendelea hadi miaka yake ya mwanzoni ya kazi yake.

"Ilinichukua kama miaka miwili kuupata moto na barafu," alisema mwaka 2018. "Moto wa kushinda lakini baridi ya barafu ili kufunika hasara na makosa mabaya. Kisha kazi yangu ilipaa katika hali isiyotarajiwa."

Kwa kweli, Federer alipogundua hali hiyo uchezaji wake si tu ulimfikisha mbali, lakini pia uliendelea kupaa zaidi hadi kutoboa anga ya sayari nyingine.

Baada ya kutengeneza jina akiwa na miaka 19 kwa kumfunga Pete Sampras huko Wimbledon mwaka wa 2001 na mwaka mmoja baada ya kifo cha kocha wake wa mwanzo katika ajali ya gari, Federer alishinda rekodi yake ya kwanza ya rekodi ya mataji nane ya SW19 mwaka wa 2003 na alilia wakati wa mahojiano yake baada ya mechi na Sue Barker.

Katika miaka minne iliyofuata alishinda Grand Slam 11 kati ya 16 zilizopatikana katika kipindi mchezo huo ulionekana mara chache.

Mtindo aliouoneshwa kwenye sweta lisilo na cola iliyopambwa kwa dhahabu alilokuwa akivaa uwanjani, sasa limehalalishwa kikamilifu

Slam zingine nane zingetokea miaka 11 ijayo lakini hadithi ya Federer, na umaarufu wake, vimechangia kushuka kwa kiwango kikubwa pia.

La kwanza lilikuja mwaka wa 2008 alipopigwa na Rafael Nadal katika fainali ya Wimbledon kwa seti tano ambazo zinachukuliwa kama moja ya mashindano makubwa zaidi ya tenisi ya wakati wote.

Miezi sita baadaye wakati Mhispania huyo alipomfunga tena katika michuano ya Australian Open, Mswizi huyo aliangua kilio. “Mungu hii inaniumiza,” alisema. Gwiji huyo alilazimika kuweka wazi yaliyo katika nafsi yake..

Lakini Juni 2009, Federer alifanikiwa kurudi katika ushindi tena wakati huu alitoa machozi ya furaha baada ya kujibu hasara ya awali kwa kushinda taji la kwanza la French Open lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu.

Hiyo ilikamilisha ushindi wa Grand Slam, ambayo ni wachezaji watano pekee waliokuwa wamepata hapo awali ingawa Nadal na Djokovic waliifikia kuanzia hapo.

Mafanikio mengine matatu yalifuata haraka, ikiwa ni pamoja na ushindi dhidi ya Andy Murray wenye hisia kali huko Wimbledon mwaka wa 2012, lakini kwa miaka mitano baadaye ilionekana kana kwamba matokeo ya Grand Slam ya Federer yangesalia katika umri wa miaka 17, kama dalili za kwanza za majeraha makubwa zilianza kuingia katika kazi yake.

Kilichofuata, ingawa, kilikuwa kipindi cha pili cha dhahabu kwa Federer kifupi lakini hakikuwa na maajabu

Akiwa na umri wa miaka 35, na baada ya miezi sita nje na jeraha la goti, alishinda Australian Open 2017 Nadal, bila shaka, mpinzani aliyekuwa akileta amsisimko mwingine katika seti tano.

Baada ya ushindi wa mbele Federer alipiga kelele kwa kutoamini, wakati ulimwengu ukifurahia pambano lingine kati ya wapinzani wakubwa waliogeuka marafiki.

Ushindi wake wa nane katika wa All England, na wa sita nchini Australia, ulikuja miezi 12 iliyofuata.

Urithi wa Federer bila shaka utafungamana na ule wa Nadal na Djokovic, ambao walimtoa mcheza tenis huyu wa Uswizi kileleni mwa mchezo kwa upande wa wanaume na kufanya kuwa mchezo wa watu watatu wanaoshindana kiuwezo.

Federer aliweka kiwango hicho kwenye Grand Slams 20 lakini, huku akijitahidi kujiweka sawa katika misimu mitatu iliyopita, alikabiliana kwanza na Mhispania huyo na kisha Mserbiana kisha kupita idadi yake kuu.

Katika yote hayo, hata hivyo, Federer amekuwa namba moja kwa mashabiki na pia wadhamini.

Anakaa pamoja na Lionel Messi, Cristiano Ronaldo, LeBron James na Tom Brady katika orodha ya wanamichezo tajiri zaidi duniani.

Federer na nguli mwingine wa tenisi Serena Williams, ambaye pia alitangaza kustaafu mwezi uliopita, sio tu wamefanya vizuri katika mchezo huo bali Wameivuka mafanikio yao.

Popote alipoenda, Federer amekuwa akishangiliwa na watazamaji, na zaidi ni huko Wimbledon mwaka huu alipopokea mapokezi makubwa zaidi kati ya wahusika wakongwe kama sehemu ya sherehe za miaka 100 za uwanja wa tenis wa Wimbledon.

Hiyo ndio maisha yake marefu, vizazi viwili havikumbuki mazingira ya michezo bila yeye.

Salamu za heshima zenye hisia kufuatia kustaafu kwa Federer zimetoka kwa Nadal na mbali zaidi, ikiwa na kaulimbiu ya kawaida isemayo "tenisi haitakuwa sawa tena". Mswizi huyo ataonekana tena kwenye ziara yake, katika Kombe la Ryder Cup-style Laver Cup baadaye mwezi huu mashindano aliyosaidia kuyaunda. Ikizingatiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu acheze mara ya mwisho, ni kiwango gani ataweza kufikia hakijafahamika. Mashabiki wa tenisi watashuka London, hata kama kusema jambo moja tu; "Asante Roger, kwa kumbukumbu."