Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kimeta ni nini na ni ugonjwa wa kutisha kiasi gani?
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeripoti Jumatatu kuwa nchi tano za Afrika Mashariki na Kusini zinakabiliwa na milipuko ya ugonjwa wa bakteria wa kimeta (anthrax).
Zaidi ya visa 1,100 vya maambukizi, visa 37 vilivyothibitishwa na vifo 20 vimerekodiwa katika miezi ya hivi karibuni nchini Kenya, Malawi, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
WHO linasema kuwa ugonjwa huo unaenea katika nchi hizo, na milipuko ya msimu inatokea kila mwaka.
Kati ya nchi hizo tano, Zambia imeshuhudia mlipuko mkubwa zaidi wa ugonjwa huo, huku majimbo tisa kati ya 10 yakiathirika. Kufikia Novemba 20, Zambia ilikuwa imeripoti watu 684 walioshukiwa kupatwa na bakteria wa kimeta , 25 walithibitishwa kuambukizwa na kulikuwa na vifo vinne vilivyotokana na ugonjwa huo , WHO imesema.
Je, kimeta hufanya nini kwa wanadamu
Ugonjwa huo hupata jina lake kutoka anthrakis, neno la Kigiriki linalomaanisha makaa ya mawe, kwa sababu ugonjwa huo unaweza kusababisha ngozi kuwa na vidonda vyeusi.
Kimeta huwaathiri wanyama wa mifugo, lakini binadamu pia wanaweza kuambukizwa wakati wanapokutana moja kwa moja na wanyama walioambukizwa au hutumia bidhaa za wanyama walio bakteria
Husababishwa na Bacillus anthracis na kwa kiasi kikubwa huishi kama seli zinazohusika na uzazi za mimea (spores) ambazo hujificha kwenye udongo kwa miaka na hubadilika na kuwa hatari kwa mnyama zinapoingia kwenye mwili wa mnyama kupitia jeraha.
Je ni dalili zipi tatu za kimeta?
Ugonjwa wa kimeta unaweza kujitokeza kwa bnjia mojawapo kati ya hizi tatu linasema WHO:
- Kimeta cha ngozi - ambapo maambukizi ni hufanyika wakati unapokatwa ngozi - ni ya kawaida na maambukizi haya ni ya hatari ya chini ulilinganisha maambukizi yote matatu. Huanza kama matuta yaliyoinuliwa kwenye ngozi na huifanya ngozi kung’aa na kisha vidonda visivyo na maumivu na kuifanya sehemu ya ngozi kuwa nyeusi. Baadhi ya watu hupatwa na maumivu ya kichwa, maumivu ya misuli, homa, na kutapika
- Kimeta cha utumbo husababisha dalili za awali sawa na anazopata mtu aliyekula chakula chenye sumu ya chakula, lakini ugonjwa unaweza kuwa mbaya zaidi na kusababisha maumivu makali ya tumbo, kutapika damu na kuhara kali
- Kimeta cha pulmonary ni ni aina mbaya zaidi zaidi na mwanzoni kuwa na dalili ya homa au mafua ya kawaida, lakini homa inaweza kuendelea na kuwa kali kiasi cha kumfanya mtu ashindwe kupumua na hata kupata mshitukowa moyo
Unaweza pia kutazama:
Ugonjwa wa kimeta ni hatari kiasi gani?
Watu wanaougua ugonjwa huu wanahitaji kulazwa hospitalini. Watu wanaobainika kuwa wana uwezekano wa kupata maambukizi ya ugonjwa huu wanaweza kupewa matibabu ya prophylactic. Kimeta hutibiwa vyema na dawa za antibiotiki hasa Penisilini, lakini matibabu yanahitaji kuanza mara baada ya maambukizi.
Bila matibabu, hadi 20% ya watu wenye kimeta cha ngozi hufariki, kulingana na Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) nchini Marekani. Hata hivyo, kwa matibabu sahihi, karibu wagonjwa wote wenye kimeta hicho hupona.
Kimetacha utumbo – ambacho humpata mtu anapokula nyama mbichi au isiyopikwa - mara nyingi ni kibaya. Bila matibabu, zaidi ya nusu ya wagonjwa walio na aina hii ya ugonjwa hufariki.
Hata hivyo, kwa matibabu sahihi, asilimia 60 ya wagonjwa huweza kuhusurika inasema CDC.
Kimeta kinachoambukizwa kwa njia ya hewa au Inhalation anthrax hukuliwa kuwa aina mbaya zaidi ya ugonjwa, ambayo husababishwa na kuvuta hewa yenye seli za mimea zinazohusika na uzazi ( spores) . Bila matibabu, karibu kila wakati ni mbaya, lakini iwapo matibabu yatatolewa kwa haraka , karibu 55% ya wagonjwa hunusurika, CDC inasema.
kimeta kinaweza kugeuzwa vipi kuwa silaha?
Inawezekana kugeuza kimeta kuwa silaha kama kimeta cha spores(spores anthrax) hupatikana kwa urahisi katika mazingira asilia, kinaweza kuzalishwa katika maabara, na kinaweza kudumu kwa muda mrefu katika mazingira ya kawaida, inasema CDC.
Kinahitaji tu upatikanaji wa vifaa vya kisasa vya teknolojia ya kibaiolojia na chanzo cha asili cha bakteria ya kimeta kuanza mchakato wa kulima.
Kimeta kinaweza kusambazwa bila mtu yeyote kujua. Seli za kometa ambazo haziwezi kuonekana kwa macho zinaweza kuwekwa katika poda, dawa, chakula na maji, na ni vigumu kuziona, kunusa au kuonja.
Katika shambulio la mwaka 2001, kimeta kilitumwa kwa wanasiasa wa Marekani na ofisi za vyombo vya habari siku chache baada ya mashambulizi ya Septemba 11.
End of Unaweza pia kusoma:
Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Lizzy Masinga