Ramadhan: Nchi gani zina mfungo mrefu au mfupi zaidi duniani?

Ramadhan

Zaidi ya Waislamu milioni moja wameanza mfungo duniani kote wiki hii, ambapo watatumia mfungo huo wa mwezi mzima katika mwezi huu wa Ramadhani.

Swaumu inayoanzia alfajiri na kumalizika baada ya kuzama kwa jua kila siku hufanywa kwa masaa 12 hadi 18 popote pale duniani, lakini inategemea mtu anaishi sehemu gani ya dunia.

Waislamu wengi duniani wanaamini kuwa mfungo wa Ramadhani ni miongoni mwa nguzo tano kuu za dini ya Kiislamu, tangu zama za Mtume Muhammad (SAW) zaidi ya miaka 1,400 iliyopita.

Wakati wa kufunga, kula, kunywa au chochote kinachohusiana na kujamiiana kati ya mwanamume na mwanamke huepukwa kuanzia wakati wa alfajir mpaka kuzama kwa jua.

Kwa nini Ramadhani huanza kwa nyakati tofauti?

Kuna kupungua kwa siku 10 hadi 14 katika kila mwaka ikilinganishwa na wakati ambapo mfungo ulianza kwa mwaka uliopita.

Hii inatokana na jinsi kalenda ya Kiislamu ilivyo na miezi inayoishia kati ya siku 29 na 30.

Miezi yote miwili haina siku 28 kama ilivyo mwezi Februari katika kalenda ya Gregori, au siku 31 kama mwezi Desemba.

Mwaka huu, mfungo ulianza katika nchi kama vile Saudi Arabia na Nigeria mnamo Alhamisi, Machi 23.

Kwa sababu kalenda ya Hijra iko nyuma ya kalenda ya Kiislamu kwa siku 11, Ramadhani itafungwa mara mbili mnamo mwaka 2030 - ya kwanza itaanza tarehe 5 Januari na ya pili tarehe 25 Disemba.

Hizi ndizo nchi ambazo zitafunga kwa muda mfupi zaidi ramadhani ya mwaka huu

Mwaka huu, Waislamu nchini Chile watafunga kwa muda mfupi zaidi, kwa sababu watafunga kwa mwezi wa Ramadhani kwa saa 11 na nusu kila siku.

Ikiwa mtu anaishi kusini mwa dunia kama vile New Zealand, Argentina na Afrika Kusini, pia atafunga kwa saa 11 hadi 12 katika mwezi wa Ramadhani mwaka huu.

Nchi ambazo zitafunga kwa muda mrefu zaidi mwaka huu

Waislamu katika mji wa Reykjavík huko Iceland, mfungo wao utakuwa mrefu zaidi mwaka huu. Wanatarajiwa kufunga kwa saa 16 na dakika 50 kila siku katika mwezi huu mtukufu.

Nigeria : Kati ya saa 13 na dakika 18 na saa 13 na dakika 25

Tunisia : Kati ya saa 13 na dakika 44 na saa 14 na dakika 55

Morocco : Kati ya saa 13 na dakika 37 saa 14 na dakika 41

Misri : Kati ya masaa 14 na dakika 34

Saudi Arabia : Kati ya saa 13 na dakika 29 na saa 14 na dakika 11

Qatar : Kati ya saa 13 na dakika 29 na saa 14 na dakika 13

Somalia : Kati ya saa 13 na dakika 22 na saa 13 na dakika 27