Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatano 13.11.2024
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola anafikiria kumnunua mlinzi wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 23, na mlinzi mwenzake Mholanzi Sepp van den Berg, 22, ambaye alijiunga na Brentford kutoka Liverpool msimu uliopita. (Football Transfers )
Wakala wa mshambuliaji wa Canada Jonathan David amewaambia wanaomtaka kama vile Juventus, Inter Milan, Liverpool na Manchester United kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anataka kandarasi yenye thamani ya £5m kwa mwaka ili kujiunga nao kwa uhamisho wa bila malipo mkataba wake na Lille utakapokamilika msimu ujao (Tuttosport - In Itali)
Juventus wanataka kumchukua mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 23, kwa mkopo kutoka Manchester United mwezi Januari. (Tuttosport - In Itali)
Arsenal na Liverpool ni miongoni mwa klabu kuu za Ulaya zinazotaka kumuongeza kiungo wa kati wa Eintracht Frankfurt na Uswidi Hugo Larsson, 20, kwenye klikosi chao mwezi Januari. (Team Talks)
Chelsea ni miongoni mwa klabu kadhaa, ikiwa ni pamoja na Newcastle na Crystal Palace, ambao wanamtaka beki wa kati wa Benfica Mreno Tomas Araujo, 20. (O Jogo - In Portuguese).
Manchester United imekuwa ikitafuta chaguo la kumnunua beki wa kushoto wa Uhispania Alvaro Carreras, 21, ambaye walimuuza kwa Benfica msimu wa joto. (Marca - In Spanish)
Liverpool wamevutiwa na Daniel Svensson wa Sweden, huku Manchester United na Arsenal FC pia wakiwa miongoni mwa klabu zinazomuwania Nordsjælland beki wa kushoto, 22. (Teamtalk),
Barcelona wamemuorodhesha mshambuliaji wa Porto Mhispania Samu Omorodion, 20, kama mbadala wa Robert Lewandowski wa Poland, 36. (El Nacional - In Spanish)
Real Madrid wamemuweka beki wa kati wa Al-Nassr wa Uhispania Aymeric Laporte, 30, na beki wa kulia wa Tottenham Pedro Porro, 25, kwenye rada yao. (Relevo - In Spanish)
Mkurugenzi wa ufundi David Weir na msaidizi wake Mike Cave wameongoza marekebisho ya idara ya uajiri ya Brighton na kuhusisha kuondoka kwa maskauti kadhaa, licha ya klabu hiyo kufanikiwa katika misimu ya hivi majuzi. (Telegraph - Subcription Required)
Mshambulizi wa zamani wa Roma Vincenzo Montella ndiye anayeongoza kuwania nafasi ya kocha mpya wa Giallorossi na anaonekana kuwa tayari kuvunja mkataba wake kama kocha wa Uturuki, ingawa itamgharimu karibu pauni milioni moja kufanya hivyo. (Gazzetta dello Sport - In Itali)
Imetafsiriwa na Seif Abdalla