Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa: Juventus inamfukuzia Sandro Tonali Newcastle United
Kiungo wa Newcastle United na Italia Sandro Tonali, 25, anawaniwa na klabu ya Juventus kwenye uhamisho wa majira ya joto. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Barcelona Inafikiria kumpa mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 37, mkataba mwingine lakini kwa kumpunguzia mshahara. Mkataba wake wa sasa unakamilika msimu wa joto. (ESPN)
Mustakabali wa mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo katika klabu ya Al-Nassr uko mashakani. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 41 ana kipengele cha kuachiliwa kwa pauni milioni 44 katika mkataba wake na klabu hiyo ya Saudi Pro League. (Athletic - Usajili unahitajika)
Mchezaji wa kimataifa wa Scotland Scott McTominay anatarajiwa kufanya mazungumzo na Napoli kuhusu mpango wa kurefusha mkataba wake huku klabu hiyo ya Serie A ikiwa na nia ya kusalia nae kwa mkataba mpya hadi 2030. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Mshambuliaji wa Colombia Jhon Duran, 22, anatarajiwa kujiunga na Zenit St Petersburg kwa mkopo baada ya kuwa msimu mzima Fenerbahce kutoka Al-Nassr. (Sportsport)
Feyenoord ni miongoni mwa vilabu vilivyotaka kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Jesse Lingard, ambaye anapatikana kwa uhamisho wa bure baada ya kuondoka FC Seoul. Mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United mwenye umri wa miaka 33 Robin van Persie ndiye anayeinoa klabu hiyo ya Uholanzi. (Mail)
Leeds United inaripotiwa kumsaka kipa mpya katika usajili wa majira ya joto. (Team talk)
Mshambuliaji wa Tottenham Muargentina Alejo Veliz, aliye na umri wa miaka 22 na ambaye yuko Rosario Central kwa mkopo , anatarajiwa kujiunga na klabu ya Brazil Bahia msimu wa joto kwa mkataba wa thamani ya euro 9m (£7.8m) pamoja na marupurupu menginea. (Fabrizio Romano)
Atletico Madrid ilionyesha nia ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uhispania Gabri Veiga, 23, siku chache zilizopita za usajili wa majira ya baridi lakini Porto walikataa mbinu ya klabu hiyo ya La Liga. (Fabrizio Romano)