Mtoto wa mwaka mmoja amng'ata nyoka hadi kumuua - Je, ilikuwaje?

.

Chanzo cha picha, Alok Kumar

Maelezo ya picha, Kesi ya mtoto anayedaiwa kumuuma nyoka imefichuliwa huko Bettiah, Bihar.
Muda wa kusoma: Dakika 4

Kisa cha kipekee kimejitokeza huko Bettiah, Bihar, ambapo mtoto wa mwaka mmoja anadaiwa kumng'ata nyoka kwa meno hadi kumuua .

Familia ya mtoto huyo inadai kuwa ni nyoka huyo ni wa aina ya cobra mwenye sumu kali.

Kufuatia kisa hicho mtoto huyo amekuwa kivutio cha wakazi wa eneo hilo tangu lilipotokea Alhamisi iliyopita. Mtoto kwa sasa yuko katika hali nzuri ya kiafya.

Tukio hili lilifanyika katika wilaya ya Champaran Magharibi ya Bihar, ambayo makao yake makuu ni Bettiah.

Sunil Sah anayeuza ice Cream ana mtoto wa kiume wa mwaka mmoja - Govind Kumar. Ni Govind ambaye anadaiwa kumng'ata nyoka huyo kwa meno yake hadi kumuua.

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Familia ya mtoto huyo inadai kuwa ni nyoka aina ya cobra (picha elekezi)

Bibi yake Govind Kumar Matisari Devi anasema, "Mama yake alikuwa akifanya kazi nyuma ya nyumba. Alikuwa akipanga mbao vizuri. Ghafla, nyoka akatoka. Govind alikuwa amekaa pale akicheza. Alipomwona nyoka huyo, akamshika na kumng'ata kwa meno. Hapo ndipo tulipogundua. Ni nyoka aina a cobra mwenye sumu kali."

"Baada ya kumng'ata nyoka huyo kwa meno, mtoto huyo alipoteza fahamu kwa muda, ndipo tulipomkimbiza katika Kituo cha Afya cha Manjhaulia ambapo alipewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Bettiah (Chuo cha Tiba cha Serikali, GMCH). Mtoto huyo kwa sasa ni mzima wa afya.

Niaz, mwandishi wa habari wa eneo hilo kutoka Manjolia, anasema, "Mtoto huyo alirudi nyumbani Jumamosi jioni. Kuna mjadala wa mara kwa mara kumhusu. Ni kawaida kwa nyoka kutoka nje wakati wa mwezi wa Sawan. Lakini hii ni mara ya kwanza kwa tukio kama hilo kutokea katika eneo letu."

Maelezo ya video, Mtoto alivyomuua nyoka kwa kumng'ata nchini India

Kwanini mtoto huyo alipoteza fahamu?

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Govind Kumar alilazwa katika Chuo cha Matibabu cha Serikali huko Bettiah Alhamisi jioni. Alitibiwa na Dk. Kumar Saurabh, profesa msaidizi katika Idara ya Madaktari wa Watoto.

Wanasema, "Mtoto alipowasili hopsitalini humo, uso wake ulikuwa umevimba hasa mdomoni. Wanafamilia walisema alikuwa amemng'ata nyoka karibu na mdomo na kumeza sehemu hiyo."

Dk. Kumar Saurabh aliambia BBC, "Cobra anapomuuma mwanadamu, sumu yake huingia kwenye damu kwa haraka. Sumu inapoingia kwenye damu, husababisha sumu ya neva, ambayo huathiri mfumo wetu wa fahamu na inaweza kusababisha kifo."

Dkt. Saurabh anaeleza, "Mwanadamu anapoumwa na nyoka aina ya cobra, sumu hiyo hufika kwenye mfumo wetu wa usagaji chakula kupitia mdomoni.

Mwili wa mwanadamu hutenganisha sumu hiyo na kuitoa nje. Katika hali moja, sumu huathiri mfumo wa neva, na katika hali nyingine mwili wa binadamu huondoa sumu hiyo."

Hata hivyo, Dkt. Kumar anaeleza kuwa binadamu anapong'atwa na nyoka huweza kusababisha madhara.

Wanaeleza, "Mwanadamu anapoumwa na nyoka, hali inaweza kuwa mbaya zaidi ikiwa kuna aina yoyote ya kutokwa na damu - kama vile kidonda."

'Mji mkuu wa kung'atwa na nyoka'

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, watu 80,000 hadi 130,000 hufa kutokana na kuumwa na nyoka kote duniani kila mwaka.

Kati ya hawa, wastani wa watu 58,000 hufa kila mwaka nchini India. Kutokana na hili, India imepewa jina la 'Snake Bite Capital of the World'.

Kulingana na data iliyopatikana kutoka kwa Mfumo wa Taarifa ya Usimamizi wa Afya (HMIS) wa jimbo la Bihar, kulikuwa na vifo 934 kutokana na kuumwa na nyoka katika jimbo hilo kati ya Aprili 2023 na Machi 2024.

Katika kipindi hiki, wagonjwa 17,859 walifika katika hospitali za serikali kwa ajili ya matibabu kutokana na kuumwa na nyoka.

Lakini kulingana na ripoti ya serikali kuu, idadi ya vifo kutokana na kuumwa na nyoka kote nchini 'hairipotiwi'.

Ripoti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Familia ya Muungano imeeleza kuwa katika visa vingi vya kuumwa na nyoka, ni wagonjwa wachache sana wanaofika hospitalini, jambo linalosababisha kuripotiwa kwa idadi ndogo ya vifo vinavyotokana na kuumwa na nyoka.

Zaidi ya hayo, asilimia 70 ya vifo vya kuumwa na nyoka hutokea Bihar, Jharkhand, Madhya Pradesh, Odisha, Uttar Pradesh, Andhra Pradesh, Telangana, Rajasthan na Gujarat.

Seif Abdalla