Vita vya Ukraine: Hasara waliopata wanajeshi wa Urusi inamaanisha nini kwa Putin?

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Rais Vladmir Putin

Unaweza kwa kawaida kutaraji kwamba runinga ya taifa ya Uruusi ingetangaza mafanikio ya jeshi lake Ukraine.

Lakini awamu ya jana ilianza kwa jambo lisilo la kawaida.

Katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine, hii imekuwa wiki ngumu zaidi kufikia sasa , alikiri mtangazaji aliyehuzunika Dmitry Kiselev.

Ilikuwa hali ngumu katika mstari wa mbele wa vita mjini Kharkiv, ambapo kufuatia uvamizi wa adui waliowazidi wanajeshi wa Urusi kwa idadi, wanajeshi wa Urusi walilazimika kuondoka miji walioiteka kutoka kwa Ukraine.

‘’Miji iliookolewa na Urusi imetekwa’’.

Moscow ilikuwa imeteka miji hiyo miezi kadhaa iliopita, lakini baada ya mashambulizi makali kutoka kwa jeshi la Ukraine, Jeshi la urusi lilipoteza eneo kubwa katika eneo la kaskazini mashariki mwa Ukraine.

Na bado vyombo vya Habari vya Urusi vinajipatia motisha kuhusu masuala kadhaa. Kile kilichotokea mjini Kharkiv hakisememekani kama ‘kusalimu amri’.

Wizara ya ulinzi ya Urusi imekana madai kwamba wanajeshi wa Urusi walitoroka kutoka eneo la Balalkliya , Kupiansk na Izyum, lilisema gazeti la serikali, Rossiyskaya Gazeta.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Hawakutoroka. Hii ilikuwa mbinu ya kujikusanya’’ katika gazeti jingine la Moskovsky Komsomolets, mchanguzi wa masuala ya kijeshi alikuwa na maoni tofauti: Ni wazi kwamba tulimdharua adui.

Wanajeshi wa Urusi walichukua muda mrefu ili kujibu na wakashindwa nguvu…, na matokeo yake, tulishindwa nguvu na mwishowe ili kuweza kuzuia hasara zaidi wanajeshi wetu walitoroka ili wasizungukwe.

Kushindwa huko kumezua hasira katika mitandao ya kijamii nchini Urusi Pamoja na vyombo vya habari mbali na mabloga wazalendo wa Kirusi ambao wamelishtumu jeshi kwa kufanya makosa.

Maudhui yao yameungwa mkono na kiongozi wa Chechnya, Ramzan Kadyrov.

Iwapo leo ama kesho hakuna mabadiliko yatafanyika , bwana Kadyrov alionya , nitalazimika kuzungumza na uongozi wa wizara ya ulinzi na uongozi wa taifa ili kuelezea hali ilivyo ardhini. Ni hali ya kushangaza.

Ni zaidi ya miezi sita tangu rais Vladmir Putin kuagiza uvamizi wa Ukraine. Katika siku zilizofuata, nakumbuka wanasiasa wa Urusi , wachanganuzi katika runinga hapa wakibashiri kwamba kile ambacho wanakitaja kuwa operesheni maalum, itakamilishwa katika siku chache, kwamba raia wa Urusi watawasalimia wanajeshi wa Urusi kuwa wapiganaji wa uhuru wao na kwamba serikali ya Ukraine itaanguka mara moja.

Haikufanikiwa. Badala yake miezi sita baadaye , jeshi la Urusi limeendelea kushindwa nguvu na kupoteza maeneo ililoteka.

.

Chanzo cha picha, KREMLN.RU

Maelezo ya picha, Rais Putin

Hivyobasi haya ndio masuali muhimu: Je hali hiyo itakuwa na madhara yoyote kwa upande war ais Vladmir Putin?

Kwa zaidi ya miaka 20 , bwana Putin miongoni mwa watu maarufu nchini Urusi amekuwa akijivunia kuwa mshindi , kwa kuweza kujiondoa katika hali ngumu , mfano ni kwamba hawezekani.

Mara nyingi nimemwona kama toleo la Kirusi la msanii maarufu wa kutoroka Harry Houdini. Vyovyote vifundo au minyororo aliyofungwa, Bw Putin kila mara aliweza kuteleza.

Hilo lilibadilika baada ya february 24.

Miezi sita iliyopita inadokeza kuwa uamuzi wa Rais Putin wa kuivamia Ukraine ulikuwa ni upotoshaji mkubwa. Haikuweza kupata ushindi wa haraka, Urusi ilisongwa katika mashambulizi ya muda mrefu, ya umwagaji damu, na imepata kushindwa mfululizo kwa aibu.

Wakati azma ya kiongozi mwenye mamlaka ya kutoshindwa inapofifia, inaweza kusababisha matatizo kwa kiongozi huyo. Vladimir Putin anajua historia ya Urusi. Haijaishia vyema kwa viongozi wa zamani wa Urusi ambao walipigana vita na hawakushinda.

Kushindwa kwa Urusi na Japan kulisababisha Mapinduzi ya kwanza ya Urusi ya 1905. Kushindwa kwa kijeshi katika Vita vya Kwanza vya Ulimwengu kulichochea Mapinduzi ya 1917 na mwisho wa Tsar.

Hadharani, ingawa, Rais Putin hana nia ya kuishia mshindwa.

Siku ya Jumatatu, msemaji wake Dmitry Peskov aliwaambia waandishi wa habari: "Operesheni maalum ya kijeshi [ya Urusi] inaendelea na itaendelea hadi malengo yake yote yaliowekwa yakamilike

Hali inayotuhimiza kuuliza masuali mengine: Je rais Putin atafanya nini?

Itakuwa vigumu kupata mtu yeyote hapa ambaye anajua Vladimir Putin anafikiria na kupanga nini. Mengi yanaweza kutegemea jinsi taarifa hizo zilivyo sahihi kutoka kwa wakuu wake wa kijeshi na wa ujasusi.

Lakini hapa kuna mambo mawili tunayojua: Rais wa Urusi mara chache hukubali kufanya makosa. Na mara chache hubadilika kuhusu uamuzi wake..