Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tunachojua kuhusu video inayoonyesha wafungwa wa Gaza wakidaiwa 'kusalimisha bunduki'
Na Benedict Garman
BBC Verify
Picha za Wapalestina waliozuiliwa na kuvuliwa nguo wakionekana kusalimisha baadhi ya silaha kwa wanajeshi wa Israel katika Ukanda wa Gaza zimezua uvumi kuhusu mazingira ya matukio na upigaji picha huo.
Hapo awali, video mbili za kile kilichoonekana kuwa eneo moja - mwanamume aliyevaa nguo yake ya ndani akitii maagizo ya kuweka silaha chini - lakini kwa tofauti kidogo, iliyozua uvumi inaweza kuwa ilirekodiwa mara kwa mara .
BBC Verify imechunguza kanda hiyo na kubaini kuwa klipu zote mbili zilitoka kwa muendelezo wa vidio unaoendelea ambapo bunduki tatu kwa jumla zinaonekana kusalimishwa. Lakini maswali yanasalia kuhusu hali halisi na kutolewa kwa video hizo.
Klipu mbili tofauti zinazoonyesha tukio moja lakini zenye tofauti ndogo ndogo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii Jumamosi tarehe 9 Desemba. Hii ilisababisha shutuma kwamba video hizo zilikuwa zimerekodiwa kwa kuchukua picha katika amaeneo tofauti . Wengine walionyesha jinsi mtu kwenye video alivyokuwa ameshikilia bunduki kwa mkono tofauti katika matukio mawili.
BBC Verify imegundua kwamba kwa kweli video hizi ni sehemu tofauti za mfuatano unaoendelea, na mtu huyohuyo anaenda huku na huko akileta bunduki tofauti .
Katika picha hiyo, makumi ya wanaume wengine wanaonekana wamesimama kando ya barabara wakitazama, pia wakiwa wamevalia nguo zao za ndani, wengi wao wakiwa wameinua mikono yao juu na wakiwa na vitambulisho. BBC Verify imethibitisha kuwa wako mbele ya shule ya Umoja wa Mataifa huko Beit Lahia, kaskazini mwa kambi ya wakimbizi ya Jabalia.
Video moja, ambayo tunajua ilipigwa ya kwanza kwa sababu mwelekeo wa jua, inaonyesha mtu huyo akiweka bunduki kutoka mkono wake wa kulia juu ya mwingine kwenye barabara. Katika video inayofuata, jua likiwa chini, mwanamume huyo anaweka bunduki tofauti juu ya zile za mkono wake wa kushoto. Picha zinathibitisha na kuhifadhi mfuatano huu, huku moja ikionyesha bunduki ya kwanza kabisa ikiwekwa, na nyingine ikionyesha bunduki na mikoba mitatu ya kubeba risasi kwenye lami.
Bado kuna maswali kadhaa yanayoulizwa na video. Hasa, mwanamume huyo anashikiliwa kwa mtutu wa bunduki na alitoa maelekezo kutoka nje ya skrini, kwa hivyo haijulikani ikiwa "anasalimisha" silaha au anazihamisha kama alivyoelekezwa. Ikizingatiwa kuwa tayari amevaa nguo zake za ndani na hawezi kuwa amezificha , kuna uwezekano wanajeshi wa Israel hawakujua kuhusu silaha hizi, wakipendekeza hii inaweza kufanywa kwa kamera, badala ya kama kitendo cha kujisalimisha. Pia hatujui kama yeye, au watu wengine wengine kwenye video, wanahusika na Hamas au shambulio la tarehe 7 Oktoba.
Katika mojawapo ya video, mwisho wa kile kinachoonekana kuwa lenzi ya Kamera ya DSLR inaonekana kwa ufupi. Pia kulikuwa na picha zinazozunguka kando ya video ambazo zilinaswa kutoka kwa pembe tofauti kidogo. Hii inapendekeza matukio yalirekodiwa au kupigwa picha na zaidi ya mtu mmoja au kamera.
Katika kipindi cha wiki moja iliyopita, picha zilziozua hisia kali za Wapalestina wanaozuiliwa huko Gaza zimezusha zimezua lalama- huku baadhi wakieleza wasiwasi wao kuhusu jinsi wafungwa hao wanavyotendewa, na Shirika la Msalaba Mwekundu likisema wafungwa wote lazima washughulikiwe kwa mujibu wa sheria za kimataifa.
Lakini Israel imekuwa na nia ya kuonyesha ushahidi inapiga hatua dhidi ya Hamas huko Gaza. Siku ya Jumapili Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alisema: "Katika siku za hivi karibuni, makumi ya magaidi wa Hamas wamejisalimisha kwa vikosi vyetu. Wanaweka silaha zao chini na kujisalimisha kwa wapiganaji wetu mashujaa.
"Itachukua muda zaidi, vita vimepamba moto, lakini huu ni mwanzo wa mwisho kwa Hamas."
Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) halikujibu moja kwa moja maswali kuhusu mazingira ya video hizi lakini msemaji aliiambia BBC kwamba watu waliozuiliwa "hutendewa kwa mujibu wa sheria za kimataifa".
"Mara nyingi ni muhimu kwa washukiwa wa ugaidi kutoa nguo zao ili nguo zao ziweze kupekuliwa na kuhakikisha kuwa hawafichi fulana za vilipuzi au silaha nyingine."
Taarifa ya ziada ya Paul Brown
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah