Unajua kutokuficha yanayokusibu na msongo ulionao kunaweza kuboresha muonekano wako?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kama ilivyo kwa watu wengi, kuzungumza hadharani kulinifanya niogope sana. Mimi ni mwandishi na ninahisi vizuri zaidi kujieleza kwa maandishi badala ya jukwaani.
Lakini, cha kufurahisha, niligundua kuwa hisia ya wasiwasi yenyewe inaweza kuvumiliwa kabisa. Kilichonitia wasiwasi ni njia ambazo watu wangepokea wasiwasi wangu- sauti hiyo ya kutikisika kidogo, kuuma midomo bila fahamu ...
Nilifikiri ningehukumiwa vikali kwa ishara zozote zisizo za maneno ambazo zilifichua ukosefu wangu wa kujiamini. Nilikuwa na wasiwasi juu ya wasiwasi wangu—mshangao maradufu wa wasiwasi ambao ulifanya tukio lionekane la kuogopesha zaidi.
Huenda tayari umewahi kujisikia ama kukutana na hali hiyo kabla ya kufanya usaili wa kazi au mkutano muhimu wa kazi na wakuu wako. Na kadiri unavyojaribu kujisahaulisha hisia zako, ndivyo zinavyopata nguvu zaidi.
Lakini utafiti mpya wa kushangaza uliofanyika hivi karibuni umethibitisha kuwa wasiwasi huu unaweza kuwa hauna msingi. Jamie Whitehouse, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Trent cha Nottingham, Uingereza, ameonyesha kwamba dalili zinazoonekana za mfadhaiko mara nyingi huwa chanya na huwafanya watu kutupenda na kututendea mazuri.
Ikiwa hiyo ni kweli, hatuhitaji kuhangaika sana kuhusu kujiweka tulivu, wa kutosita kana kwamba tunacheza mchezo wa 'poker' - kwa sababu upo uhakika kwamba watu watakaribisha uhalisi wetu wa kihisia.
Msongo wa mawazo huandaa mwili kukabiliana na changamoto yoyote
Msongo wa mawazo kwa kawaida huambatana na mabadiliko kadhaa ya ndani ya kisaikolojia ambayo hutusaidia kuandaa mwili kukabiliana na changamoto.
Moyo unapoenda mbio, kwa mfano, husaidia kutoa oksijeni katika mwili na ubongo, ambayo hutuwezesha kuchangamka kwa haraka zaidi.
Ni rahisi kuona kwa nini mabadiliko haya ni matokeo ya kuendena hali. Nyani wengi, wanapokuwa na msongoi wa mawazo pia huonyesha tabia ya 'kuvusha' - kama vile kujikuna ngozi zao kwa woga, kwa mfano.
Tabia ya aina hii haionekani kutumikia kusudi lolote dhahiri katika kushughulikia hali inayosababisha usumbufu.
Kuvutia watu
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mbali na kujikuna ngozi kunakoonyeshwa na nyani, wanadamu wana tabia nyingi za namna hii zinazohusiana na wasiwasi, ambazo ni pamoja na kugusa uso na nywele, kulamba midomo, na kuuma kucha.
Zote zinaweza kuonyesha hali yetu ya kuathiriwa na kuibua hisia nzuri kutoka kwa wengine. Ili kujua kama hii ni kweli, timu ya Whitehouse (watafiti) ilianza kwa kuwauliza washiriki 23 wa utafiti kufanya "Jaribio la Mfadhaiko wa Kijamii" - utaratibu wa kuleta wasiwasi ambapo washiriki lazima wafanyie mahojiano ya kazi na uwasilishaji. Dakika tatu kuonyesha kwa nini wao ni watahiniwa bora.
Washiriki wengine 133 walitakiwa kuzipa viwango video za mahojiano hayo ya uwongo, wakiwa na maswali kuhusu kiwango cha mfadhaiko wa kila mtu na jinsi walivyopenda watu waliokuwa wakitazama.
Sambamba, wanasaikolojia walihesabu ni mara ngapi washiriki walionyesha ishara zisizo za maneno za wasiwasi. Kama ilivyotarajiwa, waliweza kutabiri kiwango cha mfadhaiko wa waliojibu maswali.
Muhimu zaidi, mitazamo hii iliathiri—kwa bora—tathmini ya jinsi wahojiwa walivyokuwa wanavutia na kupendeza. Kadiri waliojibu walivyoonyesha dalili za mfadhaiko, ndivyo walivyovutia zaidi watu waliokuwa wakitazama video zao.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mtafiti Whitehouse anpendekeza kwamba kubadilisha tabia ya wengine kunaweza kutoa njia ya kusaidia. "Kuzalisha tabia zenye msongo kunaweza kutoa mwitikio wa ushirikiano zaidi, ambao unaweza kumtoa mtu kwenye mfadhaiko ama msongo na kupata nafuu ya haraka zaidi."
Pia kuna uthibitisho wenye nguvu kwamba kufikiri kwetu kuhusu mfadhaiko kunaweza kuamua matokeo yake. Watu wanaopata wasiwasi ukiwapa nguvu huwa na uwezo wa kufanya vizuri zaidi kwenye kazi ngumu kuliko wale wanaoogopa hisia hii.
Utambuzi wa thamani ya kijamii ya wasiwasi inaweza kuwa sababu moja zaidi ya kuangalia hali zetu kwa namna chanya zaidi.
Hakika nimegundua kuwa msimamo huu unaweza kusaidia katika kuzungumza kwangu hadharani. Mara nilipojifunza kukubali woga wangu ninapokuwa kwenye majukwaa na mihadhara, niliacha kuhisi wasiwasi kuhusu wasiwasi wangu.
Matokeo ni kwamba sasa ninaweza kuelekeza nguvu zaidi ya kiakili kwenye ujumbe ninaotaka kutoa, nikiwa na usalama wa kujua kwamba wasikilizaji wangu wataitikia kwa uchangamfu zaidi wa kibinadamu kuliko nilivyofikiria.















