Kwanini vizazi vya kati ya 1980 na 2000 wanajulikana kama "Wenye msongo wa Mawazo"

Chanzo cha picha, Getty Images
Miezi michache iliyopita mgonjwa aliniambia: "Mimi ni wa kizazi cha msongo wa mawazo"
Ilikuwa kikao chake cha kwanza na alikuja kwa matibabu kwa sababu alijikuta bila hamu ya kitu chochote, bila motisha na hisia za kwamba maisha hayana maana.
Alikuwa sahihi, yeye ni wa kile kizazi kinachoitwa "kizazi cha msongo wa mawazo", kizazi ambacho kinajumuisha wawili kati yao: waliozaliwa kati ya mwaka 1981 na 1995 yaani (milenia) na wale waliokuja ulimwenguni kati ya 1995 na 2010 yaani (kizazi Z) (tarehe zote mbili ni za makadirio kwani hakuna makubaliano ya wazi ya kijamii kwa uainishaji huu).
Ukweli ni kwamba kuna ongezeko la matumizi ya dawa za kukabiliana na mfadhaiko, kuonana mara nyingi zaidi na daktari wa kisaikolojia na kujieleza zaidi kuwa na wasiwasi na huzuni kwa vizazi hivi.
Wacha taratibu ili kugundua ni mambo gani yanachangia hii.
Ni mambo gani ambayo yamechangia hilo
Kwanza kabisa, hebu tuanze kwa kufafanua zaidi tatizo kubwa katika msongo wa mawazo.
Hii inajidhihirisha kama dalili fulani, ambazo tunaweza kuangazia kama unapokuwa na msongo wa mawazo sehemu kubwa ya siku, kupungua kwa shauku katika shughuli ambazo hapo awali zilisababisha raha, kuongeza au kupungua kwa uzito, kukosa usingizi, kuhisi huna maana, kupoteza nishati, hisia za kutokuwa na thamani au hatia nyingi, kupungua kwa uwezo wa kufikiri au kutuliza akili katika kufanya jambo lako, na mawazo ya mara kwa mara ya kutaka kujiua.
Kuna sababu kadhaa kwa nini kwanini viazi vya Milenia na Z wanajulikana kwa pamoja kama 'Kizazi chenya Msongo wa mawazo'.
Wacha tuchambue sababu tofauti ambazo zinaweza kuchochea hali hiyo:
Janga, corona na upweke
Hatuwezi kupuuza ukweli uliopo wa uwepo wa janga la covid-19 lililo kumba karibu dunia nzima kwa ujumla.
Tumezungumza kuhusu hali zisizopendeza kama vile (wasiwasi kupita kiasi kuhusu kuambukizwa virusi vya corona), wasiwasi juu ya janga (mwili unavyokuwa wakati unakumbana na ugomvi ambao bado hauja tatuliwa), n.k. Kwa kuzingatia hali kama hiyo.
swali ni: Je! hali hizi zilizoathiri hasa vizazi hivi viwili?

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasiwasi kila mara kuhusu jamii
Kwa upande mwingine, upweke wa wakati huo sasa unagongana uso kwa uso na kurejea kwa maisha ya kijamii, mara nyingi husababisha wasiwasi kwa waliobalehe na vijana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Uzoefu wangu wa kibinafsi katika kutoa ushauri umenifunulia kwamba watu wengi wa umri huu wanashutumu kutoka wakati wa hisia ya kutoweza "kuunganishwa" na wenzao wa marika zao.
Wanahisi kwamba hawafurahii hali za kijamii na watu wengi na hupata wasiwasi wanapozungukwa na mtu ambaye ndio tu wamekutana hivi karibuni.
Mitandao ya kijamii
Mitandao ya kijamii imekuwa kimbilio la vijana wengi wanaojisikia vibaya. Ikumbukwe kwamba matumizi sahihi ya mitandao hiyo ni chanya. Kwa kweli, shukrani kwao kwa hilo, jamii kutoungana wakati wa kilele cha janga la corona haukuhisiwa sana.

Chanzo cha picha, Getty Images
Lakini kuna mambo mawili ambayo yanaweza kuathiri vibaya vijana: Matumizi ya kupita kiasi au kuepuka nyakati za wasiwasi.
Hii inaweza kuwafanya kukimbilia katika mitandao kwa lengo la kuwa mbadala wa hali za kijamii.
Matumizi ya upendeleo.
Hali kama hiyo inaweza tu kuwaweka katika athari ya kufikia maudhui ambayo wanaweza kujilinganisha nayo vibaya.
Hata kwa machapisho yanayoonyesha uchungu wa kihisia na watu wasiojulikana (kwa mfano, picha za kujidhuru).
Msongo kwa ukosefu wa ajira
Kizazi cha milenia kilielimishwa katika "taratibu" iliyozingatia sana mafanikio ya kijamii, kiuchumi na ajira yaliyotokana na juhudi.
Maneno kama "Ukifanya juhudi, utapata kile ulichokusudia kufanya", hakika wengi wao wamesikia.
Ni kizazi ambacho kimejitahidi kufikia malengo yao katika maisha lakini mara nyingi matokeo yake imekuwa ni kupata msongo wa mazazo.
Masomo ya chuo kikuu yalifananishwa na mafanikio ya kupata ajira, hata hivyo, wakati kipindi hicho kilipoisha, kulikuwa na mgogoro wa kiuchumi ambao haukuwaruhusu kuendeleza kazi.
Sasa wanaweza kuogopa jambo lile lile kutokea baada ya janga hili.
Wasiwasi wa Kidunia
Miongoni mwa masuala ambayo yanahusu vizazi vya milenia na Z, tunapata masuala ya wanawake, wasiwasi wa mazingira, haki za LGTBQ +, uhamiaji...

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni vizazi vinavyojali ulimwengu na sio tu juu ya mambo maalum.
Wanafikiri zaidi na kuhisi wasiwasi kwa mambo zaidi kuliko mtu fulani na mtu binafsi.
Maswala haya ya kimataifa na uwezekano wa kuwasiliana kupitia mitandao huwapa hisia chanya ya kuhusika.
Inawafanya wajisikie kuwa sehemu ya jumla na kuhisi kueleweka kwa wenzao.
Walakini, sio tu kuwa na wasiwasi, lakini pia kutafuta suluhisho, mara nyingi huhisi uwajibikaji kupita kiasi kwa hali ambazo ni za kimataifa, ngumu zaidi kutatua na, kwa hivyo, husababisha wasiwasi.
Utambuzi mkubwa wa mtu mwenyewe kujua dalili zake
Mojawapo ya sababu kwa nini msongo wa mawazo na wasiwasi huzungumzwa zaidi katika vizazi hivi ni kwamba watu wanaougua huzungumza kwa kawaida zaidi juu yake na kutambua dalili kwa urahisi.
Kwa kweli, afya ya akili tayari ni suala linalozungumzwa sana kwenye mitandao ya kijamii, majukwaa ambayo vijana huhamia zaidi.
Hii ni chanya kwa sababu mtu anapotambua kwamba ni mgonjwa, anaweza kutafuta msaada.
Kwa kweli, ni vizazi hivi ambavyo vimevunja mwiko unaozunguka huduma ya afya ya akili.
Sasa wao ndio ambao wengi (na kwa uwazi) huzungumza juu ya kwenda kwenye matibabu.
Pia ndio wanaoipendekeza zaidi na ambao wengi hutambua matatizo yao wenyewe.
Hiki ni kizazi chenye msongo wa mawazo kwasababu ni kizazi kinachokubali usumbufu wao bila aibu wala woga.












