‘Bwana Usalama’: Je, mbinu za kijanja za kisiasa za Benjamin Netanyahu zitaondoa doa la shambulio la Hamas?

.

Chanzo cha picha, Reuters

Watu wengi nchini Israel humwita 'Bwana Usalama'. Benjamin Netanyahu ndiye waziri mkuu aliyekaa muda mrefu zaidi Israel tangu taifa hilo kupata uhuru wake mwaka 1948.

Aliingia madarakani takriban miongo mitatu iliyopita na tangu wakati huo lengo lake la kwanza limekuwa kulinda Israeli.

Lakini mnamo Oktoba 7, walipata pigo kubwa wakati Hamas, kundi la wapiganaji la Palestina ambalo linatawala Ukanda wa Gaza, liliposhambulia miji ya karibu ya Israeli.

Kwa mujibu wa maafisa wa Israel, zaidi ya watu 1,200 waliuawa huku wengine 240 wakichukuliwa mateka katika shambulio hilo la Hamas.

Lilikuwa shambulio la umwagaji damu zaidi kwa Wayahudi tangu mauaji ya Holocaust na mzozo wa kwanza wa Waarabu na Israeli.

Ndani ya saa chache baada ya shambulio hilo, Netanyahu alitangaza kulipiza kisasi akisema, "Watu wa Israeli, vita vimeanza na tutashinda."

Kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, zaidi ya watu elfu 11 wamefariki huko hadi sasa kutokana na operesheni ya Israeli huku watoto 4,000 pia wakijumuishwa katika idadi ya waliofariki. Vifo hivyo vimetokana na mashambulizi ya hivi karibuni ya anga ya Israel na mashambulizi ya ardhini.

Netanyahu anakabiliwa na labda mojawapo ya hali ngumu zaidi katika kazi yake ya muda mrefu.

Sauti za maandamano dhidi ya Israel zinazidi kupata nguvu katika ngazi ya kimataifa.

Wakosoaji wanasema kuwa Israel imefanya mauaji ya halaiki na kwamba hatua zinazochukuliwa dhidi ya raia wa Palestina ni kubwa kuliko uharibifu ulioipata Israel.

Katika makala haya, BBC inajaribu kuelewa jinsi Netanyahu alivyokuwa mwanasiasa mashuhuri zaidi nchini humo katika miongo mitatu iliyopita.

Uhusiano kati ya Israel na Marekani

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kando na 'Bwana Usalama', kuna majina mengine yanayotumiwa kwa Netanyahu katika siasa za Israel.

Bado anatumia jina lake la utani la utotoni 'BB' na ni maarufu sana miongoni mwa mashabiki wake.

Ni mwanasiasa pekee wa Israel ambaye amehudumu mara sita kama mkuu wa nchi. Ameshinda chaguzi nyingi. Ndio maana wafuasi wanamwita 'Badshah Bibi'.

Alizaliwa mnamo 1949 huko Tel Aviv. Israeli ilikuwa imeanzishwa mwaka mmoja tu uliopita. Netanyahu ndiye waziri mkuu wa kwanza wa nchi hiyo aliyezaliwa baada ya kuanzishwa kwa Israel. Baba yake alikuwa mwanahistoria mashuhuri.

Mwandishi wa gazeti la Uingereza la 'The Guardian' Jerusalem Bethan McKernan aliiambia BBC kwamba 'alilelewa katika mazingira ya kilimwengu lakini ya kihafidhina. Maoni yake kuhusu Uzayuni na taifa jipya la Israeli yalikuwa wazi na yenye nguvu.'

Netanyahu alikuwa mmoja wa kaka watatu na alilelewa wakati fulani Israeli na wakati mwingine Marekani kwa sababu ya kazi ya baba yake. Alifundisha katika vyuo vikuu vya Philadelphia na New York.

Netanyahu alijifunza kuzungumza Kiingereza kwa lafudhi ya Kimarekani enzi hizo.

Baada ya kuhitimu kutoka Shule ya Upili ya Cheltenham huko Philadelphia, Netanyahu alikuja Israeli akiwa na umri wa miaka 18 kukamilisha miaka mitano ya huduma ya lazima ya kijeshi. Huko alijiunga na Kikosi Maalum cha Sirat Mutkal cha nchi hiyo. Ni kitengo cha Israel cha kukabiliana na itikadi kali ambapo Netanyahu alishiriki katika misheni kadhaa.

Miaka kadhaa baadaye, akijadili uzoefu wake na kitengo hiki cha wasomi, aliiambia taasisi ya Marekani ya Hoover Institute kwamba:

''Nilikutana ana kwa ana na kifo mara nyingi. Nilikaribia kuzama wakati wa kurusha risasi kwenye Mfereji wa Suez. Jioni, mimi hufa na kufa. Niliumwa na nge na nikaishi kusimulia hadithi hiyo.''

Baada ya kumaliza utumishi wake wa kijeshi akiwa na cheo cha nahodha, alirejea Marekani mwaka 1972 kusomea usanifu majengo na usimamizi wa biashara katika Taasisi ya Teknolojia ya Massachusetts (MIT). Alikuwa kati ya wanafunzi bora huko MIT.

Ndoa ya kwanza kati ya tatu ilifanyika katika mwaka huo huo na kuwa na watoto watatu. Lakini baada ya mwaka mmoja alilazimika kuacha masomo yake na kwenda Israeli kushiriki katika vita vya Yom Kippur dhidi ya Misri.

Siasa

Baada ya vita kumalizika, Benjamin alirudi MIT kumaliza masomo yake. Baadaye, pia alijiunga na PhD katika Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu cha Harvard .

Mnamo 1976, kikosi hiki cha kukabiliana na itikadi kali kilifanya oparesheni hatari ya uokoaji wakati wapalestina wenye itikadi kali walipoteka nyara ndege ya abiria ya Air France na kuipeleka Uwanja wa Ndege wa Entebbe nchini Uganda.

Takriban raia mia moja wa Israel walikuwa ndani ya ndege hii, ambao walichukuliwa mateka na watu wenye msimamo mkali.

‘Operesheni Entebbe', ambayo pia inajulikana na wengine kama 'Operesheni ya Ngurumo', ilikuwa na mafanikio kamili. Wanamgambo wote waliuawa na wengi walioshikwa mateka waliachiliwa.

Hata hivyo, mateka wanne na mwanajeshi mmoja wa Israel waliuawa katika operesheni hii.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Kazi yake ya kisiasa ilianza kwa kujiunga na chama cha mrengo wa kulia cha Likud. Akawa mjumbe wa Knesset kwenye bunge la Israel. Katika miaka mitano tu, alipokuwa na umri wa miaka 42, alikua mkuu wa chama cha Likud.

Dore Gould aliwahi kuwa mshauri wa sera za kigeni wa Netanyahu na

aliambia kipindi cha Radio Four cha BBC mwaka wa 2009, 'Kulikuwa na mambo kadhaa ambayo yalisababisha kupanda kwake isivyo kawaida. Asili yake ilikuwa katika jeshi. Muhimu zaidi, alikuwa anajua Kiingereza vizuri. Ufasaha wake ulikuwa maarufu. Alikuwa mpya kwa siasa, mwenye utu wa kuvutia, alizungumza Kiingereza kama mzaliwa wa Marekani. Kiakili pia alikuwa vizuri na mwenye misingi thabiti ya kuishi.’

Mnamo 1996, wakati Benjamin Netanyahu alipoamua kugombea uwaziri mkuu baada ya kuuawa kwa Yitzhak Rabin, alimteua George Birnbaum kuwa mkuu wake wa wafanyikazi.

Kulingana na mshauri wa sera za kimataifa George Birnbaum, mafanikio ya Benjamin Netanyahu yanatokana na haiba yake.

Kampeni za mtindo wa Kimarekani lilikuwa jambo jipya kwa Waisraeli, na Netanyahu alifaulu. Tulibadilisha kabisa jinsi uchaguzi ulivyofanyika nchini Israeli.

Siri ya mafanikio

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Sehemu kubwa ya vyombo vya habari vya Israel ni vya kidunia, vinavyoegemea mrengo wa kushoto," anasema Gabriel, mchambuzi mwenye makazi yake Argentina.

Kinyume chake, wengi wa watu wa Israeli ni wahafidhina na wa kidini. Wanapopiga kura, huwa na mwelekeo wa kuegemea mrengo wa kulia na hiyo ndiyo sababu kwa nini sehemu hii imekuwa ikishinda takriban kila chaguzi huko tangu 1977.'

"Kulingana na dhamira hii ya kiitikadi, Netanyahu anajua jinsi ya kutumia hofu katika akili za watu wa Israeli," anasema Gabriel.

Kwa maoni ya mwandishi wa The Guardian wa Jerusalem Bethan McKernan, 'Netanyahu amefaulu kuunda upya taswira yake katika ulimwengu wa siasa katika miongo miwili au mitatu iliyopita.

Aliambia kipindi cha BBC Four kwamba yeye ni mhusika aliyebobea katika siasa za kugeuza watu dhidi ya kila mmoja wao. Mkakati huu wa kugawanya na kushinda umeifanya Israeli kuwa sehemu ya kihafidhina zaidi kuliko hapo awali.'

Gill Hoffman anakubaliana na McKernan.

“Mpaka sasa ameweza kukiweka chama cha mrengo wa kulia upande mmoja na mrengo wa kushoto upande mwingine ili aweze kusawazisha kati ya hivyo viwili kwa kukaa katikati,” anasema.

‘’Netanyahu ni kama mchawi wa siasa," anasema Gabriel. Hawakuwahi kuimarisha muungano wa kudumu kwa serikali zao, wala hawakuanzisha uongozi mpya kuchukua nafasi zao.'

Kwa maoni ya Gabriel, mtaalamu wa siasa za Mashariki ya Kati, 'Netanyahu alichukua mtazamo huo huo katika mazungumzo yake na Wapalestina. Uongozi wa Wapalestina umegawanyika kati ya Mamlaka ya Palestina, inayotawala Jordan Magharibi, na Hamas, inayotawala Ukanda wa Gaza.

"Sera ya Netanyahu ni kuwagawanya Wapalestina na kuwagombanisha wao kwa wao," anasema Gabriel. Aliidhoofisha Mamlaka ya Palestina pamoja na Hamas. Lakini kwa upande wa Hamas, shirika hili halijadhoofika kama vile Netanyahu alivyofikiria.

Gabriel anasema badala ya kuzungumza na Wapalestina, Netanyahu alijaribu kuboresha uhusiano na majirani zake wa Kiarabu, hasa nchi za Kiarabu za Sunni. Hizi ndizo nchi ambazo zilikuwa hazijali suala la Palestina kabla ya Hamas kushambulia Israeli mnamo Oktoba 7.

Anasema kuwa 'Natanyahu alitumia fursa hiyo wakijaribu mkakati wa kudhoofisha ajenda ya Palestina hadi kufikia maangamizi.'

Mnamo 2020, Israeli ilitia saini Mkataba wa Abraham ili kurekebisha uhusiano na Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan, na Morocco. Sasa nchi hizi zinakosoa mashambulizi ya Israel dhidi ya Gaza

Kabla ya vita kuanza, Israel ilikuwa ikifanyia kazi mkataba na mamlaka ya Mashariki ya Kati Saudi Arabia.

Baadhi ya wachambuzi wanasema kuwa makubaliano haya yanaweza kuwa moja ya sababu za shambulio lisilo la kawaida la Hamas dhidi ya Israel.

Mwandishi wa habari wa gazeti la Israel la Haaretz Anshel Pfeiffer ameandika wasifu wa Netanyahu.

"Netanyahu anajua kwamba kushindwa kwake kuilinda Israel kumetia doa uongozi wake," Pfeiffer alisema kwenye kipindi cha News Night cha BBC.

Lakini hata kabla ya shambulio hili, kiongozi huyo wa Israel alikuwa amekabiliwa na upinzani mkali kuhusu mageuzi ya mahakama.

"Pia watu walifurahia uamuzi wake wa kuunda serikali ya kitaifa na mpinzani wake, Benny Gantz," anasema Gabriel.

Anasema kuwa vita hivi vitakuwa na athari mbaya sana katika taaluma yake ya kisiasa. Sidhani kama atanusurika Lakini pia anasema kuwa 'Natanyahu ana mbinu za kijanja za kisiasa na anaweza kuchomoa ujanja mwingine kutoka kwa begi lake.'

'Wana ustadi wa kufanya mambo usiyotarajia. Baada ya vita, alionekana akitia saini mkataba wa amani na kiongozi wa Saudi Arabia mjini Jerusalem.'

Jambo la kimantiki lingekuwa kujiuzulu baada ya vita, lakini kile Netanyahu atafanya ni vigumu kutabiri.

"Ingawa mashambulizi ya Hamas yameharibu taswira ya Bw. Netanyahu ya Usalama, tutalazimika kusubiri hadi mwisho wa vita ili kuona jinsi inavyoathiri siasa zake," anasema Gabriel.