Israel ilitupa dakika tano kuondoka nyumbani kwetu

Kamal Nabhan alikuwa akipiga makelele huku akichukua simu mikononi mwa binamu yake, hakuamini alichokuwa akiambiwa na mtu aliyepiga simu ambaye hakufahamika jina lake.

Wanaume hao walikuwa walikua wanajitayarisha kwenda msikitini kuswali sala ya alasiri katika kambi ya wakimbizi ya Jabalia. Lakini ratiba yao ya kawaida sasa ilikua imeharibiwa na simu moja tu waliyoipokea ,Simu ilikua ikiwapa onyo la kuondoka walipo.

Binamu yake Kamal Ataf alishikwa na uoga na kukimbia kuwaambia ndugu zake.

"Nilimnyang'anya simu na kuongea na mtu huyo alipiga simu," anasema Ataf. "Alisema anatoka katika idara ya ujasusi ya Israel, na kuongeza kuwa tulikua na dakika tano tu za kuhama katika nyumba tuliokua tukiishi."

Wote walianza kuingiwa na hofu na kumwambia mtu aliyepiga simu kwamba lazima amekosea namba kwa sababu jengo hilo limejaa watu. "[Afisa wa upelelezi] alisikika akisema 'hapana, ondokeni kwenye hiyo nyumba mara moja," anasema Ataf.

Ilikuwa ni siku ya tano ya mashambulizi makali zaidi ya anga ya Israel huko Gaza katika kipindi cha miezi tisa. Kampeni ya kile kinachoitwa mauaji yaliyolengwa iliua watu sita wakuu katika Islamic Jihad, shirika la pili la wanamgambo wenye nguvu katika eneo la Palestina.

Lakini mashambulizi hayo pia yaliwaua raia 10 katika usiku wa kwanza pekee ikiwa ni pamoja na wake na watoto wa baadhi ya wanaume waliolengwa wakiwa wamelala.

Kundi hilo lililipiza kisasi kwa mawimbi ya mashambulizi ya roketi katika miji ya Israel, na kuwalazimu makumi ya maelfu ya watu kujificha.

Israel ilisema ilichukua hatua hiyo baada ya duru za mara kwa mara za kurusha roketi na Islamic Jihad, ambayo kwa upande wake ilisema ilifyatua kwa sababu ya uvamizi wa polisi dhidi ya Wapalestina katika msikiti wa al-Aqsa huko Jerusalem mashariki inayokaliwa, na kifo cha mshambuliaji Khader Adnan. kilichotokea hivi karibuni katika jela ya Israel .

Mapigano ya wiki iliyopita yaliua Wapalestina 33 huko Gaza na watu wawili huko Israeli raia wa israel na raia wa palestina.

Kulingana na shirika la umoja wa mataifa mapigano hayo yamewafanya zaidi ya Wapalestina 1,200 kuwa wakimbizi.

Katika jengo la familia ya Nabani, Israeli ilitoa onyo lake. Kombora moja lilisambaratisha jengo.

Muda mfupi kabla ya makubaliano ya kusitisha mapigano kuafikiwa siku ya Jumamosi, Israel iliharibu majengo ya makazi katika hali kama hiyo huku ikionya kuwahamisha wakazi kabla ya kulipua majengo hayo.

Mashambulizi haya ambayo yanaangusha vyumba vyote vya ghorofa ni mbinu iliopangwa na kuandaliwa vyema katika mashambulizi yake huko Gaza.

Israel inasema majengo yaliyolengwa yalitumiwa kama "vituo vya operesheni ya kudhibiti" na kundi la Islamic Jihad na kuelekeza kwamba kurusha roketi ilikua ni njia yake ya kuzuia madhara kwa raia wasiohusika.

Vyanzo vya ndani vinaamini kuwa mwanamgambo aliishi katika jengo hilo lakini sio kwamba lilikuwa kituo cha operesheni.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yanalaani mashambulizi kama hayo yanayoharibu makazi ya watu na hatua hiyo inachukuliwa kama ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Mkazi mwingine ambaye alipokea simu ya onyo alirekodiwa akiomba vikosi vya Israeli viweke kikomo shambulio lolote "kwenye nyumba ya wenye hatia".

Baadhi ya makazi yaliyoharibiwa yalikua yanatumika na watu wenye ulemavu na wengi walikua hawana uwezo wa kutembea na viti vya magurudumu, vitanda vilivyorekebishwa na dawa zilizoharibiwa .

Jamal al-Rozzi, mkurugenzi mtendaji wa Jumuiya ya Urekebishaji yenye makao yake makuu huko Gaza, ambaye alikuja kusaidia familia iliyokumbwa na mkasa huo anasema kundi lake litatoa misaada ikiwa ni pamoja na chakula na vifaa vya matibabu.

Pia aliyejihifadhi kwenye vifusi ni jamaa mwingine wa Kamal Nabhan. Rahma Nabhan na mumewe Yasser wameketi chini ya ubao wa paa uliovunjika, wanampa mtu mwingine binti yao mchanga Jori ili aweze kubembelezwa

Wifi zangu ni walemavu hawakuweza hata kujistiri [walipookolewa], viti vyao vya magurudumu vilizikwa chini ya nyumba," anasema Rahma.

"Kila mtu aliwaona walemavu wakikimbia. Walikuwa wakiuliza: 'Kwa nini nyumba yetu inaharibiwa,kwani ni lazima kuharibiwa? Je, walemavu hawa wamerusha makombora?' Hatuna uhusiano wowote na kile kinachoendelea," anasema.

Rahma ananitembeza karibu na mabaki ya nyumba, akiwa bado amemshika Jori huku tukipita kwenye kifusi.

Nyumba yake ilikuwa kwenye ghorofa ya juu. Sasa kuna ubao mkubwa tu wenye majina ya watu waliowahi kukaa katika eneo hilo ,ubao huo umewekwa ili kuweka kumbukumbu ya majina ya kila mkazi aliyekaa hapo zamani.

“Hatuendi popote, tutakaa juani, tulale juani, hatutoki nyumbani,” anasema Rahma.

"Tunatoa wito kwa mashirika ya kimataifa na [Rais wa Palestina Mahmoud Abbas] kusimama pamoja nasi na kujenga upya nyumba hii kwa sababu hatuna mahali pa kwenda," anasema.

Usitishaji mapigano uliofikiwa Jumamosi usiku, uliopatanishwa na Misri, umefanyika kwa kiasi kikubwa.

Lakini hali ya wasiwasi imesalia kuwa juu sana, baada ya miezi kadhaa ya ghasia zinazoendelea katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu ambao umeenea hadi Gaza katika matukio matatu makubwa tangu vita vya pande zote kati ya Israel na Hamas mwezi Mei 2021.

Mashambulizi ya wiki iliyopita yamemwacha Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiwa na ujasiri wa kisiasa. Wangeweza kwa urahisi kuwasha makabiliano makubwa zaidi - kwa kweli bado wangeweza licha ya kusitisha mapigano. Lakini ametumia mapigano hayo kuharibu sifa yake ya usalama katika kukabiliana na machafuko ya nyumbani ambayo hayajawahi kushuhudiwa na shinikizo linaloongezeka kutoka kwa watu wenye msimamo mkali wa kidini na wenye msimamo mkali katika muungano wake.

Tangu mwaka 2021, serikali ya Israeli imetoa vibali kwa maelfu ya wafanyakazi kuvuka kuingia Israeli, kukuza uchumi wa Gaza na kuimarisha mapato ya ushuru kwa Hamas. Hata hivyo, kundi hilo limeonya dhidi ya mipango ya kila mwaka ya kuandamana kwa bendera ya Israel yenye msimamo mkali kupitia maeneo ya Waislamu ya Jerusalem mashariki siku ya Alhamisi, na hivyo kuzidisha hali ya wasiwasi.

Hamas na Islamic Jihad zote zimeorodheshwa na Israel na Magharibi kama mashirika ya kigaidi.

Hata hivyo, Wapalestina wengi hapa wanahisi kutelekezwa na jumuiya ya kimataifa ambayo bado inazungumza kuhusu mustakabali wa kisiasa wa eneo hilo, suluhu la mataifa mawili ambalo linakataliwa moja kwa moja na serikali ya taifa ya Israel na makundi yenye silaha ya Palestina.

Katika nyumba ya akina Nabhan, majirani na mashirika mengine ya misaada yenye makao yake makuu huko Gaza yanawasili kwa mkusanyiko wa mshikamano na wakazi.

Hatua hiyo inajiri siku hiyo hiyo Wapalestina wanaadhimisha miaka 75 ya Nakba, wakati watu 700,000 walikimbia au kulazimishwa kutoka kwa makazi yao katika migogoro inayozunguka kuundwa kwa Israeli.

Wakaazi wasio na makazi hushikilia mabango yanayosema "Tulinde" na "Tunaomba msaada".

Ataf Nabhan, ambaye alipokea onyo kutoka kwa afisa wa ujasusi wa Israeli, anaashiria vifusi na kuniambia ombi lake ni rahisi.

"Familia hii inahitaji makazi," anasema. "Tunaomba tu mashirika ya kutetea haki za binadamu ilinde familia hii."