Mtoto aliyezaliwa kutokana na ubakaji wakati wa mauaji ya kimbari

Rwanda yaadhimisha miaka 30 ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi.

Ubakaji umetumiwa na wanamgambo kama moja ya silaha.

Claudine ni mmoja wa maelfu ya watoto waliozaliwa kutokana na ubakaji wakati wa mauaji ya kimbari. Alipokuwa akikua, alikuwa na hamu ya kukutana na baba yake lakini mama yake alisita. Baada ya miaka 24 jela kwa uhalifu wa mauaji ya halaiki na ubakaji, babake Claudine yuko tayari kufanya upatanisho.

Serikali ya Rwanda inapenda maridhiano kama chaguo la kipekee la ujenzi mpya wa baada ya mauaji ya kimbari.

Je! watoto wanaozaliwa kwa njia hii wanaweza kuwa daraja la upatanisho kati ya wazazi wao?