Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ligi Kuu ya Uingereza: Wachezaji watano vijana wanaosaka mafanikio msimu 2023-24
Ligi Kuu ya Uingereza inaanza mwezi huu wa Agosti. Ni mchezaji gani atatafuta kuwa katika nafasi ya juu ya ligi hiyo? Ni nyuso zipi mpya, zinaweza kuwa Evan Ferguson au Rico Lewis anayefuata?
BBC inawataja vijana watano wanaosaka mafanikio katika msimu wa 2023-24. Wachezaji hawa tuliowachagua watakuwa na umri wa miaka 21 au chini ya umri huo, wakati mechi ya kwanza itakapochezwa.
James Trafford
Mchezaji wa Burnley, James Trafford . Mlinda lango huyo mwenye umri wa miaka 20 aling’aa na klabu ya Young Lions wakati wakitwaa Ubingwa wa Ulaya chini ya umri wa miaka 21 msimu huu wa joto.
Mlinda mlango wa ajabu, Trafford aliweka rekodi ya kutofungwa katika michezo sita. Vilevile aliokoa kwa ustadi mkwaju wa penalti wa dakika za lala salama kabla ya kuzuia mkwaju wa pili katika ushindi wa mwisho dhidi ya Uhispania.
Trafford anatarajiwa kushindana na golikipa Arijanet Muric, ambaye alikuwa tegemeo la Clarets waliposhinda taji la Ubingwa msimu uliopita.
Kobbie Mainoo
Kobbie Mainoo kijana aliyezua tafrani miongoni mwa mashabiki wa Manchester United baada ya matokeo mazuri ya kujiandaa na msimu mpya, alipocheza michezo minne.
Ni kiungo mkabaji, ambaye anaweza kutumika katika majukumu mengi. Kwa, utulivu wa kumiliki mpira ambao hauendani miaka yake.
Ana umri wa miaka 18, aliingia akitokea benchi katika ushindi dhidi ya Leicester msimu uliopita. Alicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu ya Uingereza, mwezi Februari. Meneja Erik ten Hag anaonekana yuko tayari kumbakisha kinda huyo Old Trafford msimu huu badala ya kumpeleka nje kwa mkopo.
Mainoo atakosa mechi za mwanzo baada ya kupata jeraha la kifundo cha mguu katika mechi dhidi ya Real Madrid ya kujiandaa na msimu mpya. Lakini anatarajiwa kurudi katika timu ya United atakapo pona.
Cameron Archer
Mshambulizi wa Aston Villa, Cameron Archer ana kila anachohitaji kuwasumbua mabeki wa ligi kuu ya Uingereza. Ana kasi ya ajabu, udhibiti wa mpira na jicho la kufunga.
Archer alipokuwa kwa mkopo katika timu ya Middlesbrough, wakati wa hatua ya mtoano msimu uliopita, alifunga mabao 11 katika michezo 20.
Ollie Watkins huenda akaongoza safu ya washambuliaji baada ya kufanya vyema katika kikosi cha Unai Emery msimu uliopita, lakini Archer anaweza kuwekwa pamoja na mchezaji huyo mwenye uzoefu au akawa mbadala wake kutokea benchi ikiamuliwa atasalia Villa Park.
Alifunga bao la ufunguzi, England iliposhinda kwenye michuano ya Ulaya ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21 msimu huu wa joto.
James McAtee
Kiungo huyo mzaliwa wa Salford ni mchezaji mbunifu na tishio awapo golini. Akitokea kikosi cha vijana cha Manchester City, McAtee alifunga bao katika ushindi wa mwezi uliopita dhidi ya Bayern Munich wakati wa mechi ya kujiandaa na msimu mpya.
Alicheza vyema na alifunga mabao tisa katika mechi 37 za mkopo, zikiwemo mechi 21 alizoanza kipindi cha kwanza wakati Sheffield United ilipopanda daraja hadi Ligi Kuu ya Uingereza mnamo 2022-23.
City haipungukiwi na viungo wa kiwango cha kimataifa kama vile Kevin De Bruyne, Bernardo Silva na Phil Foden, lakini McAtee atakuwa na hamu ya kumuiga mwenzake Rico Lewis, ambaye alipanda kwenye kikosi cha kwanza msimu uliopita baada ya kupandishwa na Pep. Guardiola.
Simon Adingra
Brighton ina rekodi nzuri ya kuibua vipaji vya vijana kama Evan Ferguson, 18, na Julio Enciso, 19 aliyesajiliwa majira ya kiangazi. Wote waliingia kwenye kikosi cha kwanza msimu uliopita.
Winga wa Ivory Coast Simon Adingra anaweza kuwa wa hivi punde kuibuka, baada ya kudhihirisha yeye ni mpigaji mzuri wa mshuti na mwenye kasi ya kuivuruga safu ya ulinzi ya timu pinzani.
Alifunga mabao 10 ya ligi katika mechi 30 alizocheza kwa mkopo katika klabu ya Union SG ya Ubelgiji msimu uliopita, kufuatia kuhamia Brighton kutoka klabu ya Nordsjaelland ya Denmark kwa pauni milioni 6 mwezi Juni 2022.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 bado hajacheza mechi yake ya kwanza ya ushindani kwa Seagulls, lakini alionyesha umahiri wa kufunga katika ushindi wa Brighton wa kujiandaa na msimu mpya dhidi ya Brentford.