Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mchungaji wa Marekani aliyenusurika miaka 17 katika jeshi lililosahaulika msituni
- Author, George Wright
- Nafasi, BBC News, London
Mchungaji Y Hin Nie, 75, anahubiri injili kutoka katika kanisa lake lililopo katika jimbo la North Carolina nchini Marekani. Lakini akiwa kijana alinusurika karibu miongo miwili msituni, akitoa mahubiri kwa wenzake wakipigana na wanajeshi wa Vietnam muda mrefu baada ya vita kumalizika - AK-47 yake haikuwa mbali naye.
Hin Nie na kitengo chake cha waasi huku wakikimbia na kutengwa na ulimwengu walitafuta chakula na kuwinda ngozi ya chui milia ili kulipa Khmer Rouge. "Jeshi lake lililosahaulika" halikuweka silaha chini hadi 1992, baada ya Hin Nie kujadili uhuru wao.
Mara ya kwanza Y Hin Nie karibu kufa ilikuwa usiku wa 30 Januari 1968, wakati Vietcong, inayopigania Kaskazini ya Kikomunisti huko Vietnam, ilianzisha mashambulizi makubwa, kurusha makombora kwenye maeneo yanayoshikiliwa na Marekani wakati wa Tet - au sherehe ya Mwaka Mpya.
Hin Nie, ambaye alikulia Vietnam, alikuwa akiishi na wamishenari Wakristo wa Marekani huko Buon Ma Thuot, jiji kubwa zaidi katika Nyanda za Juu na Kati za Vietnam. Wazazi wake walikuwa wamemwacha pamoja na wamishonari alipokuwa na umri wa miaka minane kwa sababu walikuwa maskini na walitaka awe na maisha bora, anasema.
Mama yake mlezi Carolyn Griswold, alikuwa amelala wakati roketi hizo zilipogonga. Ripoti tofauti kutoka kwa wamishonari zinasema kwamba wanajeshi wa Kikomunisti pia walilipua vilipuzi ndani ya nyumba hiyo.
Baba ya Carolyn, Leon, alikufa papo hapo. Hin Nie - ambaye alikuwa kwa rafiki yake usiku huo - alikimbia nyumbani na kusaidia kumtoa Carolyn kutoka kwenye vifusi. Alifariki muda mfupi baadaye.
"Mama yangu mlezi alikufa kwa mateso," anasema. "Mungu aliokoa maisha yangu."
Wamishonari wengine wengi waliuawa na kutekwa huku Hin Nie akijificha kwenye chumba cha kulala.
Licha ya yote aliyopitia alijipa moyo na kuendelea na maisha. Alijiunga na shule ya Biblia na kufanya kazi katika kanisa.
Hakujiunga na vita hadi Machi 1975, wakati wanajeshi wa Kusini wanaoungwa mkono na Marekani walipoangamizwa na kulazimishwa kurudi kutoka Buon Ma Thuot.
Mabomu yalipozidi, Hin Nie na wanafunzi 32 wa shule ya biblia walitoroka, wakitembea mwendo mrefu.
Huo ndio ulikuwa wakati Hin Nie alipofikiwa na wapiganaji wa United Front for the Liberation of Oppressed Races (Fulro), vuguvugu la waasi wenye silaha ambalo lilitetea uhuru wa makabila madogo yaliyoitwa Montagnards. Watu hawa wa nyanda za juu kwa muda mrefu wamekabiliwa na mateso nchini Vietnam sababu ikiwa ni pamoja na imani yao ya Kikristo.
Walitumaini kwamba uhusiano wa karibu wa Hin Nie na wamishonari wa Marekani na Uingereza hasa uwezo wake wa kuzungumza ungewezakuwaunganisha tena na wanajeshi wa Marekani, ambao walikuwa wameajiri maelfu ya wakazi wa milimani kama wapiganaji kabla ya kujiondoa kwenye vita mwaka wa 1973.
Hin Nie anasema alivutiwa kujiunga na wapiganaji, ambao walikuwa Wakristo waaminifu kama yeye. "Sikuwa na chaguo, iligusa moyo wangu."
Mnamo tarehe 10 Machi 1975, alikimbilia msituni pamoja nao.
Kwa miaka minne ya kwanza, walikaa ndani ya Vietnam, mara kwa mara wakikimbia, wakijificha kutoka kwa jeshi.
"Piga risasi na kukimbia, piga na kukimbia. Hatukuwa na silaha kali," Hin Nie anasema, akiongeza kuwa hakuhusika katika mapigano ya moja kwa moja, lakini alibeba AK-47 kwa ajili ya kujilinda na kuwinda.
Kufikia 1979, wanajeshi wa Vietnam walikuwa wakipanua oparesheni zao za kumtafuta Fulro, kwa hiyo kikundi hicho kilikimbilia Cambodia, magharibi mwa Vietnam.
"Hatukuweza kukaa, kwa hivyo tulivuka mpaka - ilikuwa hatari sana," anasema.
Lakini kuondoka Vietnam kulileta hatari mpya. Waasi wa Khmer Rouge wa kundi la Khmer Rouge la mauaji ya halaiki ya Pol Pot walidhibiti maeneo kwenye mpaka wa mashariki wa Cambodia.
Mabaki ya serikali - iliyohusika na vifo vya takriban watu milioni 1.7 wakati wa miaka minne ya ugaidi nchini Cambodia - walikuwa wamekimbilia huko baada ya kupinduliwa na vikosi vinavyoungwa mkono na Vietnam.
Fulro alihitaji ruhusa kutoka kwa Khmer Rouge ili kukaa ili Hin Nie akutane na makamanda wao wa ndani katika misitu ya jimbo la Mondulkiri.
"Nilisema, 'Tunamuwinda adui mmoja' - lilikuwa jambo pekee tulilokubaliana. Ikiwa wakomunisti watakuja kutoka Vietnam hadi upande huu, bila shaka tutaweza kuwafahamisha," anasema.
Khmer Rouge iliruhusu Hin Nie na kikosi chake kubaki. Lakini walidai "kodi" za kila mwezi kwa kiasi kikubwa cha ngozi yachui milia na chatu, na pembe ya kulungu.
Hin Nie anasema kitengo chake kiliwanasa simbamarara kwenye mitego. Wakati huo hofu ya kuuliwa na simbamarara ilikuwa sana - simbamarara waliua watu watatu kambini - hofu ya Khmer Rouge ikaongezeka zaidi.
"Walikuwa na hasira sana, walihesabu kila kitu," anakumbuka. "Mara nyingi walitutishia: 'Ikiwa hutalipa kodi lazima turudi."
Fulro bado angefanya doria na kulikuwa na mapigano ya hapa na pale na vikosi vya Vietnam wakati kitengo kikihama kutoka msitu mmoja hadi mwingine, bila kutulia kwa muda mrefu zaidi ya mwezi mmoja.
Hin Nie anakumbuka "maisha ya porini" - wapiganaji wa Fulro walizurura kama wanyama, wakila chochote walichoweza kupata, ikiwa ni pamoja na majani ya miti, anasema.
"Tulitembea na kutembea mwendo mrefu ... tungepiga risasi tembo, chochote tulichoweza kuona."
Wakati huo ndio alimuoa mke wake H Biuh, ambaye alikuwa sehemu ya kundi hilo. Walipata watoto watatu msituni, lakini mmoja alikufa.
Dini ilikuwa msingi wa kudumu kambini.
Kitu cha kwanza ambacho Hin Nie angefanya walipofika mahali pageni kilikuwa ni kuweka msalaba. Kisha angefanya mahubiri kwa askari, wanawake na watoto.
Pamoja na kuwa mchungaji wa Fulro, Hin Nie pia alikuwa afisa wake mkuu wa uhusiano. Hii ilimaanisha kushughulika na Khmer Rouge ya ndani, lakini pia kusikiliza redio ya mawimbi mafupi kila asubuhi, ikiwa ni pamoja na BBC, Sauti ya Amerika na redio ya Kivietinamu, kujaribu kufuata kile kilichokuwa kikifanyika katika ulimwengu ambao ulikuwa umewasahau.
Kufikia 1991, vikosi vya Cambodia chini ya Waziri Mkuu wa wakati huo Hun Sen - ambaye alikabidhi hatamu kwa mwanawe mapema mwezi huu baada ya miaka 38 madarakani - vilikuwa tishio jipya kwa Hin Nie kufanya mazungumzo.
Lakini mbali na askari wachache wa eneo la Khmer Rouge na Cambodia, hakuna mtu aliyejua kwamba wapiganaji wa Fulro walikuwa bado msituni. Wenzao wa zamani hawakujua kama bado walikuwa hai na hata jumuiya ya kimataifa haikujua.
Kwa hivyo ilikuwa mshangao mkubwa mnamo 1992, wakati Hin Nie alipoanza mazungumzo na maafisa wa Umoja wa Mataifa. Walikuwa wamefika kufuatia mauaji ya halaiki ili kusimamia uchaguzi wa kitaifa wa Cambodia kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani.