Liz Truss ajiuzulu kama Waziri Mkuu wa Uingereza

Liz Truss amejiuzulu kama waziri mkuu wa Uingereza siku 45 tu baada ya kushika nafasi hiyo.

Truss alisema mrithi wake atachaguliwa katika uchaguzi wa ndani wa chama cha Tory, utakaofanyika wiki ijayo.

Wabunge wa Tory walimtaka Bi Truss aondoke madarakani baada ya serikali yake kukumbwa na misukosuko ya kisiasa, kufuatia kupuuzwa kwa sera zake nyingi za kiuchumi.

Bi Truss alichaguliwa na wajumbe wa Tory mnamo Septemba, na anakuwa Waziri mkuu aliyekaa muda mchache zaidi.

Katika hotuba yake, Bi Truss alisema Chama cha Conservative kilimchagua kwa jukumu la kupunguza ushuru na kukuza ukuaji wa uchumi.

Lakini kutokana na hali hiyo, Bi Truss alisema: "Ninatambua kwamba siwezi kutekeleza mamlaka ambayo nilichaguliwa na Chama cha Conservative."

Bi Truss alisema atasalia kwenye wadhifa huo hadi mrithi atakapochukua rasmi wadhifa wa kiongozi wa chama na atateuliwa kuwa waziri mkuu na Mfalme Charles III.

Jeremy Hunt - ambaye aliteuliwa kuwa kansela wiki jana - amesema hatasimama katika kinyang'anyiro cha uongozi kuwa waziri mkuu ajaye.

Truss -Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi Uingereza 

Bi Truss - ambaye aliingia madarakani siku 44 zilizopita - atakuwa Waziri Mkuu aliyehudumu kwa muda mfupi zaidi katika historia ya Uingereza

Kiongozi wa chama cha Labour Sir Keir Starmer aliitisha uchaguzi mkuu mara moja kufuatia hotuba ya Bi Truss ya kujiuzulu.

Katika hotuba yake, Bi Truss alisema aliingia "ofisini wakati wa machafuko makubwa ya kiuchumi na kimataifa", huku vita vikiendelea nchini Ukraine na gharama za maisha zikiongezeka.

Lakini kujiuzulu kwake kunakuja baada ya waziri mkuu, katibu wa zamani wa mambo ya ndani Suella Braverman, kujiuzulu na wabunge wa Tory kuasi katika kura ya bunge iliyokumbwa na machafuko