Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mwanajeshi mtoto aliyekuwa katika kundi la LRA aliyeanza maisha mapya katika sanaa
Furaha anayoipata aliyekuwa mpiganaji mchanga Peter Oloya katika Sanaa hii ya uchongaji wa sanamu, iliibuliwa alipokuwa akimtafutia bibi yake udongo wa aina ya CLAY huko kaskazini mwa Uganda, eneo ambalo limejipatia sifa mbaya ya mashambulizi yaliyotekelzwa na kundi la Lwaasi la LORD’S RESISTANCE ARMY {LRA}.
‘Bibi yangu alinionyesha palipo udongo huo wa CLAY, ni aina gani ya udongo unaofaa kutumiwa na kwa nini,’ asema msaanii huyu kutoka Uganda, ambaye aliliewa kijijini Lemo Bongolewic uliopo kwenye wilaya ya Kitgum.
Huu ulikuwa wakati wa miaka ya awali ya themanini, kabla idadi kubwa ya wakazi wake walikusanywa na kuwekwa kwenye kambi zilzizotazamiwa kuwaokoa dhidi ya mashambulizi ya mara kwa mara na kutekwa nyara.
Oloya na marehemu bibi yake – Hellen Atoo Ocula, walikuwa wakiwapeleka mifugo wao malishoni wakitazamia maeneo yenye kibaridi kiasi chini ya kivuli cha aiana mbali mbali ya miti mikubwa .
Kulikuwa na aina moja ya udongo wa CLAY uliofahamika kaama ‘PUNU’ kwa lugha ya kiaACHOLI ambayo ndio anayoizungumza Oloya. Udongo huo ulipendwa na ngombe wanaosemekana kuvutiwa na madini yake muhimu – na vile vile na bibi yake Oloya kwa sababu ulikuwa mzuri zaidi kutengeneza nyungu za kupikia na kuhifadhi maji.
Oloya aliyekuwa mchanga wakati huo, alivutiwa na kupendezwa na michoro aliyoyaweka kwenye baadhi ya nyungu kwa kutumia vifaa vidogo.
‘Ilikuwa baadaye ambapo niliangazia Sanaa kama taaluma rasmi na nikagunduwa kwamba bibi alukuwa na ujuzi wa sanaa,’ amesema.
Oloya sasa ni msanii tajika kutoka Uganda ambaye anafahamika kwa umaarufu wa sanamu au vifaa ambavyo amechonga – Na jumba linaloonyesha Sanaa hii huko London linaandaa maonyesho ya kazi yake mwezi huu.
Aidha anaheshimika kwa sababu alipitia na kuokoka madhila ya kutekwa nyara akiwa mtoto na kundi la LRA ambalo liliongozwa na Joseph Kony, ambaye anasakwa na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC kukabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu.
Msanii huyu amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na sanamu yake ya ndege wa aina ya CROWNED CRANE, Sanaa ya chuma cha shaba inayofanana na ndege rasmi wa taifa la Uganda na ambalo ni zawadi alilipewa marehemu Malkia Elizabeth wa pili wakati huo akiwa kiongozi wa Uingereza.
Miongoni mwa mashabiki wa Soka, anajulikana sana kwa kutengeneza tuzo mashuhuri la BBC Mchezaji bora barani Afrika ambalo lilitolewa kwa wachezaji kwa muongo mmoja tangu 2009.
Katika muda wa hivi maajuzi amegaukiwa Sanaa ya kutumia shaba, mbao na marumaru – ila vyanzo vyake vya Sanaa hii vinatokana na udongo wa CLAY ambao alikusanya kwa Pamoja na bibi yake kandokando mwa mito katika bonde lililokuwa karibu na nyumbani kwao.
‘Ufinyazi wa udongo ni saw ana kuchonga sanamu , na udongo umekuwa na nafasi muhimu katika maisha yangu tangu utotoni,’ ameiambia BBC.
Akiwa mtoto mdogo, Oloya alikabiliwa na dhihaka kutoka kwa jamii kwa kutengeza nyungu akiwa na bibi yake – kwani katika tamaduni ya jamii ya Acholi, kazi hiyo ilikuwa imetengewa wasichana na akina mama.
Lakini Oloya alipuuza hilo na kuendelea kuchukuwa udongo huo katika kichuguu na kutengeneza mpira mdogo wa kurusha kwa kombeo/manati au kitu kingine.
‘Kina ninapoitazama, mimi hupata hisia ya kuchukuwa udongo huo na kutengeza kitu kutoka kwake – kwa raha zangu au kwa mzaha..’ anasema
Sanamu yake ya kwanza aliyoichonga , ilitokana na kitu kingine anachokipenda – kusikiliza redio. Baba yake, aliyekuwa askari polisi mjini Kampala, alikuwa ametuma redio moja nyumbani. Ilikuwa na mataa yaliyobadilisha rangi kutoka kijani hadi manjano na nyekundu kulingana na viwango vya sauti.
‘Niliipenda sana, na nikiwa mtoto, nilkuwa nikijiuliza , jinsi kifaa kidogo kama hicho kingeweza kuzungumza,’ asema Oloya.
Alichonga redio kutoka kwa udongo, akitoa mashimo madogo katika eneo ambapo mataa yalipokuwa. Alipajaza wadudu aina ya kimemeta/kimulimuli , ambao hutoa mwanga wakati giza kinapoingia.
Lakini maisha yake ya utotoni hayajakuwa salama, yamekubwa na miaka mingi ya mizozo iliyoshuhudiwa kaskazini mwa Uganda, ambako jeshi la UPDF yalikabiliana na wapiganaji wa kundi la LRA, ambao wanasifa mbaya tya kutekeleza mauaji, kuwabaka wanawake na kuwateka nyara Watoto wanaolazimishwa kuwa wapiganaji kwenye kundi hilo au kufanywa mateka wa ngono.
Na kama maelfu ya watu wengine, Oloya alilazimishwa kuondoka nyumbani hadi kwenye kambi ya wakimbizi wa ndani iliyowekwa na serikali ya Uganda.
Na kisha alipotimia umri wa miaka 11, alitekwa na kundi la LRA, wakati ambapo familia yake ilirejea nyumbani kuvuna zao la simsim liliokuwa limepandwa shambani ili kutengeza rojo lenye maidini muhimu linalopendeza kwani wakati huo chakula kilikuwa kimepungua sana kwenye kambi hilo.
Alichapwa, kutengwa na mama yake na kwa Pamoja na wavulana wengie waliotekwa wakaingizwa kichakani. Walihamisha mara kwa mara, ili kuwa kwepa wanajeshi wa UPDF , huku waasi wa LRA waki walazimu kuwa wapiganaji.
Wakati huo , Oloya aligeukia kipenzi chake -Udongo wa CLAY kaama njia ya kumtuliza kujisahaulisha yaliyokuwa yakimpata – jambo ambalo hadi sasa hulipata kuwa gumu kulizungumzia.
Angechukuwa udongo mwingi kutoka kwa vichunguu vingi ambavyo vilijaa mwituni ambapo walikuwa wanazuiliwa.
‘Niligunduwa haraka kwamba , ninachokifanya ni Sanaa, hata nilipokuwa mwituni,’ amesema.
Kwa miezi kadha alifikiria kwamba mama yake alikuwa amefariki hadi mateka mgeni alipomnuelezea kwamba alikuwa hai n ani hapo ambapo aliamua kutoroka na kujinasua.
Oloya alifanikiwa kutoroka baada ya miezi 18. Huku Sanaa ikiwa eneo lake la kupata utulivu.
Mwaka 2004 alifuzu katika Chuo Kikuu cha Makerere aliposomea Sanaa na kulipia masomo yake kwa kufanya kazi ya UDeeJay kwenye maeneo ya burudani usiku na kuuza vinyago ambavyo alikuwa akivitengeneza tangu utotoni.
Baada ya kufuzu katika chou kikuu alikosomea Sanaa, alirejea katika kambi za wakimbizi wa ndani zilizoko kaskazini mwa Uganda kutoa mafunzo ya Sanaa, kukuza vipaji vya vijana na pia kufanya maonyesho ya kazi yake jijini Kampala.
Faida alizopata kutokana na mauzo ya Sanaa yake, aligawanya.
Kambi hizo sasa zimefungwa na wakazi wa kaskazini mwa Uganda wamerejea makwao. Lakini shikila lake la kijamii bado linahudumu huko – na anatengeneza eneo la maonyesho na jumba la makumbusho la Sanaa ya jamii ya Acholi kw apamoja na tamaduni za jamii hiyo katika Kijiji chake.
Katika onesho lake la kwanza binafsi katika jumba la maonesho la Pangolin, Oloya amebuni aina mpya ya kazi ambayo inaangazia tena mada ambazo zinamvutia yeye: suala la urembo, nafasi ambapo usasa na utamaduni inapokutana na kisha mazingira na hali ya anga.
Hapa kuna sanamu ya shaba ambayo imetengezwa mithili ya ardhi iliyokauka na kupasuka. Usipotazama kwa uangalifu utakosa kuona picha ndogo ya binadamu, aliyaanguka katika mojawapo ya maeneo yaliyopasuka – au eneo ambalo ardhi imewachana.
Ujumbe wa Oloya ni wazi: ‘Mabadiliko ya tabianchi, joto linalopanda duniani – ni sisi wa kulaumiwa nah atua hii inatuua.’
Kipande kingine ambacho kinaandamana na kile ni hiki cha shaba cha mtoto anayelia. Kinatoa matumaini makubwa, kwa sababu mtoto huyu anashikilia mche huu wa kijani kwenye mkono mmoja.
‘Tunapaswa kuwacha kufikiria kuwa dunia ni mama, ambaye yuko hapa kutupatia tunachokitaka na kutupatia usaidizi,’
Badala yake tunahitaji kuifikiria dunia kuwa mithili ya mtoto aliye taabani na anaomba kubebwa na anahitaji msaada wetu,’
Kipande kingine kinachovutia, ambacho ni tofauti na kazi zake za kawaida ni cha vazi la kitamaduni la mwanamke ambalo Oloya alitengeneza kwa kitambaa kinachotokana na gome la miti .
Ameshikanisha vipande vya simu za mkononi kwenye vazi hilo . Oloya anatumia ishara hizo za usasa na utamaduni kama alama ya athari ya uchafu wa plastiki kutoka nje ya bara Afrika ambao unakinzana kwa karibu na vazi lililotokana na Ngozi ya nje ya miti ambalo linatokea barani afrika .
Oloya aidha huangazia mada ya usasa katika baadhi ya vibuyu vyenye umbo na ukubwa tofauti, ambao ni tunda linalotokana na miti ya mibuyu.
Amechomea picha mbali mbali za mapambo ya kiafrika kwenye upande w anje wa mibuyu hiyo. Kwa mtazamo wa kwanza yanaonekana kama mibuyu ya kwwaida ambayo inatukima vijijini kuhifadhi maziwa, mafuta au maji. Lakini ukitazama kwa karibu, unaona nembo za kampuni kubwa za kimataifa ambazo kwa sasa zinasheheni soko la kimataifa la vinywaji vinavyouzwa barani afrika.
‘Ninaipenda Sanaa sana,’asema Oloya, “kwa sababu inanipa lugha nyingine ya kuzusha mijalada ,’
Imetafsiriwa na Leila Mohammed na kuhaririwa na Lizzy Masinga