Ni kwanini uvamizi wa Urusi nchini Ukraine bado unaigawanya Afrika?

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika nchi thelathini – ni nchi mbili tu zaidi ya idadi ya mwaka jana – zilipiga kura ya kuunga mkono azimio la Mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa linalopinga Urusi, kuunga mkono hadhi ya mpaka wa Ukraine, na kutoa wito wa amani.
Madagascar na Sudan Kusini, ambazo kwa pamoja hazikupiga kura mwaka jana , mara hii zote zilunga mkono azimio hilo. Morocco pia haikupiga kura mwaka 2022 lakini ikapiga kura kuunga mono azimio Alhamisi wiki hii.
Mataifa ya Afrika yalikuwa ni karibu nusu ya mataifa yote ambayo hayakushiriki kura kwa kutohudhuria kika kura hiyo. Gabon, ambayo ilibadili kura yake kutoka kuunga mkono azimio la kuiunga mkono Ukraine mwaka jana, ilikuwa miongoni mwa nchi 15 ambazo zilisusia kupiga kura mwaka huu.
Rasmi , nchi hizi zinasema msimamo wake ni kutofungamana na Urusi au mataifa mengine ya Magharibi yanayoiunga mkono Ukraine.
Licha ya kuongezeka kwa mazungumzo na ziara za maafisa wa ngazi ya juu kutoka mataifa ya magharibi, pamoja na mawaziri wa kigeni wa Ukraine na Urusi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, msimamo wa mataifa ya kiafrika bado haujabadilika.

Siku moja kabla ya mkutano mkuu wa hivi karibuni wa Umoja wa mataifa , rais wa Ukraine President Volodymyr Zelensky alizungumza na mwenzake wa Uganda, Yoweri Museveni -lakini mazungumzo ya mud awa mwisho hayakuweza kubadili kura ya Uganda.
Namibia, ambayo ilimpokea Mke wa rais wa Marekani Lady Jill Biden katika ziara yake ya Afrika wiki hii, pia haikubadili msimamo wake.
"Sio kugeuza swichi ya mwangaza," Waziri wa sheria wa marekani Blinken aliliambia gazeti la The Atlantic, akikiri kuwepo kwa changamoto ya kidiplomasia katika kupata uungaji mkono kwa ajili ya Ukraine katika baadhi yan chi za Kiafrika.
Alielezea kuwa na matumaini, hatahivyo, kwamba Afrika Kusini kwa sasa kuwa mwenyeji wa mazoezi ya kijeshi ya siku 10 pamoja na Uchina na Urusi - ni "matarajio ya taratibu " ya kuwa mbali na Urusi.
Maafisa nchini Afrika Kusini wamekanusha michezo ya kivita ni ya uchokozi kutokana na na kwamba inafanyika wakati yakifanyika maadhimisho yam waka mmoja ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine.
Ni kwanini uhusiano wa Urusi ni imara katika baadhi ya maeneo ya Afrika?
Baadhi ya mataifa ya Afrika yalikuwa na uhusiano wa miongo kadhaa ya Muungano wa Usovieti. Baada ya kuvunjika mwaka 1991, uhusiano huu uliendelea na Urusi, huku viongozi wa waliopata uhuru wa mataifa mengi ya Afrika wakisema silaha na mafunzo ya kijeshi waliyoyapata kutoka Urusi vilikuwa muhimu katika kuwasaidia kupambana dhidi ya utawala wa wazungu walio wacheche na ukoloni.
Nchini Afrika Kusini, wakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi, serikali ya Marekani ilikitaja chama cha tawala cha Africa National Congress – kama kikundi cha ugaidi.
Kiongozi wake Nelson Mandela, pia alitawa kama miongoni mwa magaidi.
Licha ya kushinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 1993, pamoja na kiongozi wa mwisho wa ubaguzi wa rangi Frederik de Klerk, na kuwa rais wa kwanza mweusialiyetawala kuanzia 1994 hadi 1999, Mandela aliendelea kuwa katika orodha ya watu ambao marekani inawatambua kama magaidi hadi iliporekebishwa mwaka 2008.

Chanzo cha picha, Getty Images
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Nelson Mandela na Winnie Mandela (katikati) akizungumza na ujumbe wa Usovieti wakati wa sherehe za uhuru wa Namibia mwaka 1990.
"Bila shaka, kwa bahati mbaya, zaidi ya bahati mbaya, Marekani ilikuwa na huruma sana kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, kwa hiyo historia haifutiki, unafahamu, kwa usiku mmoja ," Bw Blinken aliiambia The Atlantic.
Lakini ukoloni uliopita hauelezei uhusiano wa sasa, walau kwa baadhi ya nchi.
Nchi kama vile Eritrea na hivi karibuni Mali – zilitengwa kwa kiasi kikubwa na jamii ya kimataifa – zimepata mshirika katika Urusi.
Zilikuwa miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zilimpokea hivi karibuni waziri wa mambo yan je wa Urusi Sergei Lavrov, n azote zilipiga kura dhidi ya azimio la Umoja wa Mataifa linaloiunga mkono Ukraine.
Kiongozi wa kijeshi wa Mali mwaka jana aliyaamuru majeshi yote ya Ufaransa kuondoka nchini mwake na amelikaribisha kundi la mamluki wa Wagner kuchukua nafasi yao katika kusaidia kupambana na makundi ya ghasia ya Kiislamu nchini humo.
Nchi nyingine saba za Kiafrika - Senegal, Tanzania, Equatorial Guinea, Burkina Faso, Eswatini, Guinea Bissau na Cameroon – hazikupigia kura kabisa azimio la Umoja wa Mataifa.
Nchi za kwanza tatu zilipiga kura ya kujizuia kupiga kura mwaka jana.
Sio sahihi kuchukulia kwamba nchi zaidi ya 50 za Afrika zina majibu na hisia sawa. Kila moja ina sababu zake za ni kwanini ilipiga kura jinsi ilivyopiga.
Na kwasababu kura hiyo sio ya lazima kisheria, bila shaka itaendelea kuonyesha ushirika wa kijiografia katika miezi na miaka ijayo.















