Tetesi za soka Ulaya Jumatano 16.10.2024

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester City wanamfikiria kocha mkuu wa Sporting Ruben Amorim, 39, kuwa meneja wao mpya ikiwa Pep Guardiola, 53, ataondoka mkataba wake utakapokamilika mwishoni mwa msimu huu. {Guardian)
Beki wa Bayern Munich na Canada Alphonso Davies, 23, analengwa na Manchester United msimu ujao. (Sky Germany)
Barcelona wanaweza kuwalenga kiungo wa Ubelgiji Romeo Lavia na kiungo mshambuliaji wa Uingereza Carney Chukwuemeka, wote 20, kutoka Chelsea mwezi Januari. (Sport – In Spanish)
Mshambulizi wa Uswidi Alexander Isak, 25, ameviweka vilabu vikiwemo Arsenal katika hali ya tahadhari huku akiendelea kusuasua kusaini kandarasi mpya huko Newcastle. (talkSPORT)

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Senegal Cheikhou Kouyate, 34, alifanyiwa vipimo vya afya huko Leeds Jumanne kama mchezaji huru baada ya kuondoka Nottingham Forest. (Football Insider)
Paris Saint-Germain bado wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa England Marcus Rashford, 26, kutoka Manchester United baada ya mbinu yao ya . (TeamTalks)
Chelsea haiko tayari kukaribisha ofa kwa mshambuliaji wa Ufaransa Christopher Nkunku, 26, huku akihusishwa na Paris St-Germain. (Football Insider)
Tottenham na Crystal Palace zote zinamtaka winga wa Lille mwenye umri wa miaka 21 na Iceland Hakon Arnar Haraldsson. (Football Transfers),

Chanzo cha picha, Getty Images
Kipengele cha kutolewa kwa mlinda mlango wa Espanyol Mhispania Joan Garcia, 23, ambaye alikuwa anatakiwa na Arsenal majira ya joto, kimepunguzwa hadi euro 25m (£20.83m). (Mundo Deportivo – In Spanish)
Manchester City huenda ikadai ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia kwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland, 24, kujiunga na Real Madrid au Barcelona. (Teamtalks)
Wakati huo huo, City wameungana na Chelsea, Arsenal na Tottenham kumfuatilia kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk na Ukraine Georgiy Sudakov, 22. (I Sport).
Imetafsiriwa na kuchpishwa na Seif Abdalla












