Tetesi za soka Jumapili: Real Madrid waongeza kasi kumnyakua Rodri

Rodri

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Real Madrid wanaongeza juhudi zao za kumvutia kiungo wa Manchester City mwenye umri wa miaka 29, Rodri, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania akiwa na chini ya miezi 18 iliyobaki kwenye mkataba wake.(Teamtalk)

Arsenal wana nia ya kumsajili kiungo wa Bayern Munich Leon Goretzka kwa uhamisho wa bure msimu wa joto, baada ya kuripotiwa kujaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 31 mwezi Januari.(Mirror)

Juventus hawajafanya mazungumzo yoyote ya mkataba na mshambuliaji Dusan Vlahovic tangu majira ya joto yaliyopita, na kwa kuwa mkataba wa mchezaji huyo wa Serbia mwenye umri wa miaka 26 unaisha msimu wa joto, Chelsea, Tottenham, AC Milan, Inter Milan na Roma wanaonesha nia ya kumnyakua.(Foot Mercato - in French)

Vlahovic

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa Paris St-Germain Luis Enrique amehusishwa na kazi ya Manchester United, lakini Mhispania huyo haoni kama ni mradi unaomfaa na anatarajiwa kusaini mkataba mpya na klabu hiyo ya Ufaransa.(Mirror)

Manchester United na Newcastle wamejiunga na orodha inayoongezeka ya vilabu vinavyomfuatilia beki wa kulia wa Brentford na timu ya chini ya miaka 21 ya Italia, Michael Kayode, mwenye umri wa miaka 21.(Teamtalk)

Inter Milan wanatarajiwa kumpa kocha Cristian Chivu nyongeza ya mkataba wa mwaka mmoja hadi 2028 pamoja na nyongeza ya mshahara mwishoni mwa msimu.(Corriere dello Sport, via Football Italia)

Chivu

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Argentina Paulo Dybala (32) na kiungo mshambuliaji wa Italia Lorenzo Pellegrini (29) watalazimika kukubali kupunguziwa mishahara yao iwapo wanataka kubaki Roma, huku mikataba yao ikiisha msimu wa joto.(Gazzetta dello Sport - in Italian)

Kiungo wa Italia Sandro Tonali (25) anaweza kudai kuondoka Newcastle iwapo klabu hiyo itashindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa msimu ujao.(Football Insider)

Hata hivyo, Newcastle pia wanamwangalia kiungo wa Lyon mwenye asili ya England, Tyler Morton (23), kama mbadala wa Tonali, huku Crystal Palace na Nottingham Forest pia wakivutiwa na mchezaji huyo wa zamani wa Liverpool.(Caughtoffside)

Barcelona wameamua kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa England Marcus Rashford (28) kutoka Manchester United kuwa wa kudumu.(Fichajes - in Spanish)