Baada ya miaka mingi ya ukame, Arsenal inakaribia kuukana 'utoto?

Arsenal's William Saliba and Gabriel

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arsenal wameingia fainali yao ya kwanza kubwa baada ya miaka 6
    • Author, Andy Cryer
    • Author, Steven Sutcliffe
  • Muda wa kusoma: Dakika 4

Baada ya karibu miaka sita na robo ya majaribio yaliyoshindikana, Arsenal imefanikiwa kuingia fainali kubwa baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-2 dhidi ya Chelsea kwenye nusu fainali ya Kombe la Carabao. Hii itakuwa fainali yao ya kwanza chini ya kocha Mikel Arteta tangu waliposhinda kombe la FA mwaka 2020, na ya pili tangu ajiunge la klabu hiyo.

Mechi hiyo ilikuwa ngumu na yenye mvuto wa kawaida tofauti na ile ya mzunguko wa kwanza pale Stamford Bridge ambapo Arsenal ilishinda 3-2, lakini ilimalizika kwa Kai Havertz kufunga bao katika dakika za lala salama na kuipeleka Arsenal Wembley. Furaha ya mashabiki na wachezaji ndani ya Emirates ilionyesha wazi umuhimu wa ushindi huu.

Ingawa pande zote mbili zilipata mashuti mbili tu yaliyolenga lango, Arsenal hawakuonekana kuwa na hatari kubwa, na walionyesha sifa zote zinazowafanya kuonekana wagumu kufunguika.

Matokeo haya yanamaanisha Arsenal itacheza fainali ya tisa ya EFL Cup, ikikutana na Manchester City au Newcastle Jumapili, Machi 22, kwenye mechi ya mwisho ya mashindano haya. Iwapo watakutana na City, itakuwa marejeo ya fainali ya mwaka 2018, ambayo Manchester ilishinda, wakati Arteta akiwa sehemu ya benchi la ufundi la City chini ya Pep Guardiola.

Mbali na kuwa nafasi ya kulipa kisasi cha fainali ya 2018 na kushinda Kombe hilo baada ya miaka 33, hii pia ni hatua ya kubadilisha mitazamo baadhi ya mashabiki na wachambuzi.

Kocha Arteta alisema: "Tumekuwa tukisubiri kwa miaka michache kufika hapa na hakika tutaifurahia fainali. Unaona furaha, tabasamu, na nguvu yote ndani ya klabu."

Kiungo Declan Rice aliongeza: "Tunastahili hili. Miaka mitatu au minne iliyopita tulikuwa kileleni mwa ligi kuu, tukishindana na kufikia karibu (kutwaa kombe) lakini hatukutosha. Hii ndiyo sababu msimu huu tuna ari zaidi ya kushinda kila mashindano. Safari bado ni ndefu, lakini kufika fainali na klabu hii ni jambo la kushangaza."

Kwa miaka michache, uongozi wa Arteta umekuwa hadithi ya "karibu tu (kwa maana ilibaki kidogo tu tutwae kombe)," ikiwa ni pamoja na kupoteza robo-fainali na kushindwa kutwaa taji la ligi kuu. Sasa, wakiwa na mchezo mmoja tu ili kumaliza ukame wa taji, je, Arsenal wanakaribia kuondoa sifa ya kuitwa watoto ama waliokaribia kutwaa kombe?

Nyota wa zamani wa Arsenal, Matt Upson, anasema: "Ushindi huu ni matokeo ya miaka mingi ya kutengeneza msingi. Mikel Arteta amekuwa akianzisha falsafa ya timu, mshikamano, na mshikamano wa wachezaji."

Shauku ni kubwa ndani ya Arsenal

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Tangu walipotwaa FA Cup mwaka 2020, Arsenal wamecheza robo-fainali nne na kupoteza zote. Wakati huo hawakushinda hata mchezo mmoja kati ya miwili ya hatua hiyo (nyumbani na ugenini), hivyo ushindi wa hivi karibuni unaweza kuwa nguvu kubwa ya kisaikolojia, na pia huongeza matumaini ya kushinda taji la Machi.

Katika misimu ya hivi karibuni, Arsenal pia wamepoteza nafasi za ubingwa wa ligi kuu, jambo lililosababisha shinikizo kubwa kwa Arteta kuhakikisha klabu inapata taji msimu huu. Ingawa Kombe la Carabao si lengo kuu, kushinda taji hili kunaweza kuwa kigezo cha kuimarisha morali kuelekea mashindano mengine makubwa.

Upson aliongeza:

"Nadhani mashabiki wako na shauku kama wachezaji na kocha kushinda taji la maana. Wanataka taji la ligi kuu, lakini hili ni sehemu kubwa ya kufanikisha lengo hilo. Ni muhimu kushinda robo fainali na kushinda taji, kwani hawajashinda vya kutosha katika miaka michache iliyopita. Huu msimu unahusu kupata mafanikio hayo. Ushindi huu unaweza kutoa msukumo mkubwa wa katika ligi kuu. Hisia ndani ya uwanja baada ya mechi ilikuwa jambo kubwa sana kwa Arsenal."

Mlinzi William Saliba alisema:"Ni klabu kubwa, hivyo shinikizo ni kubwa kila wakati. Lakini ni vizuri kuwa na shinikizo; tunacheza soka kwa ajili ya hilo. Tuna mechi nyingi mbele, takriban miezi minne, na tunataka kushinda mashindano yote. Tuna kikosi cha kutosha na kocha anayefaa."

Kiungo wa zamani wa Liverpool, Jamie Redknapp, alisema: "Wamejipanga kushinda. Wamepitia mateso kwa miaka mingi, lakini matokeo haya yanaweza kuwapa nafuu kidogo na kuwaruhusu kufurahia. Wanachofanya msimu huu ni jitihada kubwa, hakuna sababu ya kukosa taji moja, mawili au hata tatu."

Arsenal watatimiza ndoto?

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mara ya mwisho Arsenal kutwaa kombe ilikuwa 2020 miezi michache baada ya Arteta kujiunga na klabu hiyo

Wiki 17 zikisalia kabla ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, timu hiyo bado haijashinda taji lolote, lakini wanaongoza Ligi Kuu kwa alama sita. Msukumo huu, pamoja na ushindi wa hivi karibuni, unaweza kuwa kielelezo cha mafanikio makubwa.

Arsenal tayari wapo katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa, wako bado katika mashindano ya FA Cup watakutana na Wigan, klabu ya daraja la chini. Ingawa kuzungumzia kutwaa makombe manne"Quadruple" bado ni ndoto, hali ya sasa inawaweka karibu zaidi na mafanikio makubwa kuliko timu yao maarufu ya "Invincibles" iliyocheza msimu mzima bila kufungwa mwaka 2003-04.

Hata hivyo, timu hiyo ilipata kombe la tu FA Cup kama taji la pekee msimu huo, na ndoto ya kutwaa mataji manne 'Quadruple' ilikufa Februari 3, 2004, baada ya kuchapwa na Middlesbrough 3-1 kwa matokeo ya jumla katika robo fainali ya Kombe la Ligi.

Tangu mwaka 1960, si rahisi kushinda ubingwa wa England, kushinda Kombe la FA, Kombe la Ligi, na pia Ligi ya Mabingwa Europe katika msimu mmoja, kuna historia ya kuonekana mara chache tu. Matokeo ya Liverpool 1984, Manchester City 2018-19, na Manchester United 1998-99 na 2022-23 yanaonyesha jinsi kufanikisha kutwaa makombe yote manne makubwa ni changamoto kubwa. Hadi sasa, hakuna timu ya England iliyowahi kushinda mataji manne katika msimu mmmoja.

Lakini msimu huu, kwa sababu Arsenal wanaongoza Ligi Kuu na wapo kwenye hatua nzuri ya mashindano mengine, ndoto bado haiwezi kupuuzwa. Arteta hajatangaza kuwania mataji manne rasmi, lakini mashabiki wa Arsenal wanaweza kuota, wakijua kuwa timu yao ina nafasi ya kubadilisha historia ya miaka ya 'karibu tu' na kuunda historia mpya ya mafanikio makubwa msimu huu.