Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
'Kwa nini nilitumia ada yangu ya chuo kikuu kwenye vita vya TikTok vya Somalia'
Ukikagua vizuri miamala ambayo Zara hufanya inaonyesha ametumia maelfu ya dola kwenye TikTok.
Zara, sio jina lake halisi, ana umri wa miaka 20, anaishi Marekani na ana asili ya Kisomali.
Alivutiwa na kipengele cha majibizano mubashara mtandaoni ambacho huwaona washawishi wawili wakirushiana maneno na wakati mwingine hudhihakiana wao kwa wao wanapoomba pesa kutoka kwa wafuasi wao ili washinde pambano hilo.
Aligundua baadae kwamba kuna upande mbaya zaidi wa michezo hii na ameieleza BBC.
Majibizano hayo yanapendwa na watumiaji wa TikTok kote ulimwenguni lakini dhana ya mchezo wa Kisomali ni tofauti kwa sababu washawishi wa pande zote mbili mara nyingi huwakilisha koo za Kisomali na wakati mwingine kujibizana matusi ambayo yanaweza kusababisha lugha kali.
Hufahamika kama Big Tribal Game ambapo makumi kwa maelfu ya watu hujiunga wakati washawishi huweka muziki wa Rap ambao unatukuza koo zao,kwa mashairi yenye kusifu ushujaa na uzuri wa watu wao.
Tukio tulilotazama Jumamosi usiku wa Oktoba lilikuwa mfano wa kawaida: kulikuwa na washawishi wawili kwenye skrini iliyogawanyika. Watu wapatao 50,000 walikuwa wakitazama nasi.
Vita hivyo hasa humaanisha kuwahamasisha wafuatiliaji kuwatunza wachezaji Zawadi Zaidi,ambazo wanahitaji kushinda kila mzunguko wa dakika tano.
Mshindi ni mshawishi ambaye atapokea Zawadi Zaidi,huku aliyeshindwa akitarajiwa kumpongeza mshindani wake kwa kumtangaza kwamba Ukoo ule ndio wenye nguvu zaidi katika usiku ule.
Wakati mwingine tukio hilo hutangazwa mtandaoni kwa miezi kadhaa kabla ya kufanyika.
Washawishi, ambao mara nyingi huwa nchini Marekani na Ulaya, huonyeshwa moja kwa moja kabla ya mchezo kuanza, wakipaza sauti kwa umati.
Mwanzoni, wakati mwingine mijadala ikiendelea, lakini mazungumzo ya ndani ya mchezo huweza kuwa ya kawaida.
Shughuli huwa kati ya watu wanaochangia, wakijaribu kushindana kutoa zawadi.
Kuna lugha mpya,sarafu ya kidijitali na sheria nyingi zisizoeleweka ambazo ni sehemu ya mchezo,na kuongeza ubora wa hali ya juu kwa tukio hilo.
Tuliona baadhi ya vitu vya thamani ya juu Zaidi vikitolewa Zawadi kama vile ‘’Tiktok Universe’’ ambayo ina thamani ya Zaidi ya $500 (£385) ambayo sawa na karibu sarafu 50,000 za TikTok.
Gharama ikiwa nafuu kidogo kwa $400 (£308) na kipenzi cha mashabiki ni simba, ambaye hunguruma kwa sauti kubwa anapokimbia kwenye skrini. Au kuna nyangumi muungwana zaidi anaogelea kutoka chini ya maji.
Baadhi ya zawadi huweka nakshi kwenye uso wa anayeshawishiwa kama vile kofia ya ‘’cow boy’’ ,au bereti nyekundu.
Zara anasema alianza kucheza kwa sababu alitaka kutetea Fahari ya ukoo wake.
Ilikuwa "ya kusisimua" na "upande wangu ulishinda kila wakati", anakumbuka.
Lakini Zara alitumia zaidi ya dola 7,000, zilizokusudiwa kulipia ada yake ya chuo kikuu, kwenye michezo hiyo.
‘’Wazazi wangu wakigundua kwamba ninatumia pesa nyingi katika Tiktok,wangefadhaika - wasingefurahi - lakini kwa namna fulani ni kama uraibu."
Alijiuliza pia kwanini alitoa pesa zilizopatikana kwa tabu kwa kuwapatia washawishi ambao ni nadra walionesha shukrani zozote.
Lakini alipozama katika ulimwengu huu,aligundua kilikuwa kitu kibaya Zaidi.
Tumeona Ushahidi kwamba Mshawishi mwenye makao yake nchini Marekani amekuwa akitukana wanawake katika Tiktok na kuwatishia kuchapisha picha zao za ngono.
Zara anasema hutokea sana: "Hujua wewe ni nani, wanachukua picha za familia yako, picha yako, na wanasema, 'Nitazichapisha'.
Anasema mwanamume huyo mwenye ushawishi aliyeko Marekani alimfanyia hivyo,jambo lililomsababishia hofu na wasiwasi kwamba familia yake ingeona picha iliyotengenezwa ambayo alitishia kuchapisha mtandaoni , hakuweza kulala u…
Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Seif Abdalla