Ni kwanini Marekani ina wasiwasi kuhusu usalama wa TikTok ?

Miito nchini Marekani ya kupiga marufuku mtandao wa TikTok imeibua mjadala duniani kuhusuhatari za usalama wa mtandao

Mkurugenzi Mkuu mtendaji wa TikTok anatarajiwa kuchukua msimamo katika kikao cha nchin Marekani huku miito ya kitaifa ya kupiga marufuku mtandao huo ambao baadhi wanahisi unatishia usalama wa taifa.

Kwa miezi kadhaa Shou Zi Chew amedai kuwa mtandao huo wa jukwaa la kushirikishana video ni salama licha ya wimbi la kupigwa marufuku na maafisa wa serikali katika nchi za Uingereza, Marekani, na Canada pamoja na mataifa mengi ya Ulaya ambao wamewazuia wafanyakazi kuutumia mtandao wao katika simu zao.

China imeishutumu Marekani kwa kwa kutia chumvi hofu za usalama wa kimtandao ili kuzima kuongezeka kwa kasi ya ukuaji wa kampuni lakini kuna ongezeko la shinikizo la kutaka iuzwe nchini Marekani au ipigwe marufuku marufuku kutokana na madai kwamba mtandao huo wa kijamii unaweza kutumiwa kama chombo cha ujasusi.

Mnamo mwaka 2020, TikTok iliponea chupuchupu wakati wa utawala wa Donald Trump, na kukabiliwa na maswali ya kila siku kuhusu hatari za usalama wa kimtandao unayosababishwa na TikTok.#

Kutokana na changamoto ngumu za kisheria, mjadala ulizimwa kwa kiasi kikubwa – na hatimaye ukatulia mwaka 2021, wakati Rais Joe Biden alipopinga pendekezo la Trump.

Ungeweza kusikia hali ya ahueni , kwa upande wa TikTok yenyewe na mamilioni ya washawishi wanaotegemea mtandao huo wa kijamii kupata pesa.

Lakini sasa, kutokana na shinikizo la hivi karibuni, tunarejea kule tulikoanzia.

Wakati pendekezo la Trump lilipotolewa miaka mitatu iliyopita, TikTok imekuwa ikipakua karibu video mara milioni 800 kote duniani. Kwa sasa imefikia video bilioni 3.5 zilizopakuliwa kulingana na mchambuzi wa kampuni ya TikTok, Sensor Tower.

Pamoja na kuongezeka kwa hali ya wasi wasi ya siasa za kijiografia iliyopo baina ya China na nchi za Magharibi, na ni wazi kuwa hali ya baadaye ya TikTok duniani imo hatarini kuliko wakati wowote ule.

Lakini je ni hofu gani tatu za usalama wa kimtandao kuihusu TikTok ambazo zinaendelea kujitokeza, na ni majibu gani yaliyotolewa na kampuni uhusu hofu hizo?

TikTok hukusanya kiasi cha data 'kupita kiasi'

Msemaji wa TikTok aliiambia BBC kwamba ukusanyaji wa data wa app hiyo "unawiana na utendaji katika sekta yake".

Mara kwa mara wakosoaji huishutumu TikTok kwa kuvuna kiwango kikubwa cha data kutoka kwa watumiaji. Ripoti ya usalam wa kimtandaoiliyochapishwa Julai , 2022 na watafiti katika Internet 2.0, kampuni ya mtandao ya Australia, mara kwa mara wamekuwa wakionyesha ushahidi.

Watafiti walichunguza chanzo cha alama ya siri ya app na waliripoti kuwa "uvunaji wa data wa kupita kiasi". Wachambuzi wanasema TikTok hukusanya taarifa kama vile eneo aliko mtumiaji, ni kifaa gani anachotumia na niprogramu(app) nyingine zipi, ambazo zipo katika kifaa

2. TikTok inaweza kutumiwa na serikali ya China kuwapeleleza watumiaji

Msemaji wa TikTok aliiambia BBC kwamba kampuni ni huru na "haijatoa data kwa serikali ya china, na hatujawahi kuombwa".

Ingawa inawakera wataalamu wa taarifa za kibinafsi, wengi wetu tunakubali kuwa kutoa dataza kibinafsi kwa mtandao huo wa kijamii.

Kwa kutupatia huduma zao bila malipo wanakusanya ujuzi kutuhusu na kuutumia kuuza matangazo ya kibiashara katika jukwaa lao, au kuuza data zetu kwa makampuni mengine yanayotaka kutangaza biashara kwetu kupitia mtandao

Suala la ukosoaji ambao TikTok inao ni kwamba inamilikiwa na kampuni kubwa ya kiteknolojia yenye kamao yake Beijing -ByteDance, na hivyo kuifanya kuwa kampuni ya kipekee ambayo sio ya Marekani inayotoa matangazo ya moja kwa moya ya mtandaoni . Facebook, Instagram, Snapchat na YouTube, kwa mfano, hukusanya kiasi sawa cha data lakini zote ni kampuni zilizoanzishwa na Marekani .

Kwa miaka mingi, mawakili wa Marekani , pamoja na maeneo mengine duniani wamekuwa wakiamini kwamba : data hizo zinazokusanywa na majukwaa haya hazitatumiwa kwa sababu za njama mbaya ambazo zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa.

Agizo la Rais Donald Trump la mwaka 2020 lilidai kkuwa ukusanyaji wa data za TikTok unaweza kuisaidia China "kufuatilia maeneo ya wafanyakazi wa shirikisho la Marekani na wajenzi, kujenga waraka wa taarifa za kibinafsi kwa ajili ya kuzitumia vibaya, na kufanya upelelezi wa makampuni

3. TikTok inaweza kutumiwa kama kifaa cha 'kuingiza mawazo kwa watumiaji'

Msemaji wa TikTok alisema: "Miongozo yetu ya watumiaji wa mtandao inazuia taarifa za upotoshaji ambazo zinaweza kusababisha madhara kwa watumiaji au kikundi cha umma , mkiwemo kujihusisha na uratibu wa tabia zisizoaminika."

Mwezi Novemba 2022, Christopher Wray, mkurugenzi wa Shirika la ujasusi la Marekani (FBI), aliwaambia wabunge wa Marekani: " Serikali ya China inaweza kudhibiti taarifa ambazo zinaweza kutumiwa kwa ajili ya operesheni za ushawishi ."

Hofu hizo zaidi zilichochewa na ukweli kwamba app nyingine ya TikTok, Douyin – ambayo inapatikana China pekee – imedhibitiwa sana na iliripotiwa kuwa iliwekwa kwa ajili ya ushawishi wa kielimu na taarifa zinazofaa kusambazwa zaidi mtandaoni.

Mitandao yote ya kijamii inadhibitiwa sana nchini China huku polisi wa mtandao wakifuta maudhi ambayo yanaikosoa serikali au yanayochochea vurugu.