Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 01.02.2024

.

Chanzo cha picha, REX features

Maelezo ya picha, Morgan Rodgers

Aston Villa imemsajili mshambuliaji Morgan Rogers kutoka Middlesbrough kwa mkataba unaoripotiwa kuwa wa takriban £15m.

Rogers, 21, amefunga mabao saba na kutoa asisti tisa katika michezo 33 aliyoichezea klabu hiyo ya Championship msimu huu.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza chini ya miaka 20 alihamia Riverside Stadium kutoka Manchester City kwa £1.5m kwa mkataba wa miaka minne Julai iliyopita.

Middlesbrough ilikataa ofa tatu kutoka kwa Aston Villa kabla ya kukubaliana juu ya bei ya Rogers.

Mmiliki Steve Gibson alidhamiria kutomruhusu mchezaji huyo kuondoka kwa chini ya hesabu yake - iliyofikiriwa kuwa karibu £12m.

Manchester City pia walifanya mazungumzo ya ada ya mauzo ya 25% kutoka kwa faida ya mpango huo kwa Rogers, ambaye anacheza kama winga.

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Fulham wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Chelsea na Albania Armando Broja, 22 kwa uhamisho wa dakika za lala salama (Evening Standard)

Chelsea wanataka pauni milioni 50 kwa Broja - bei ambayo Cottagers wanasita kuilipa (Mail)

Tottenham hawana uwezekano wa kufikia bei inayotakiwa na Chelsea ya pauni milioni 50 kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Conor Gallagher na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 anatazamiwa kusalia na The Blues kwa muda wote uliosalia.(Talksport)

Spurs wanavutiwa na mchezaji wa kimataifa wa Uswidi mwenye umri wa miaka 17 Lucas Bergvall, anayechezea Djurgardens .(Football London)

TH
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Jose Mourinho, ambaye hivi majuzi alitimuliwa kama mkufunzi wa Roma , angetamani kurejea Manchester United kama meneja wa klabu hiyo ya Old Trafford iwapo nafasi hiyo itatokea.. (Mail)

Mkufunzi wa Bournemouth Andoni Iraola hatarajii mshambuliaji wa Uingereza Dominic Solanke kuondoka katika klabu hiyo mwezi Januari, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kuhusishwa na Tottenham. (Evening Standard)

Aston Villa wamekubali dili la kumsaini beki wa pembeni wa England chini ya miaka 19 Lino Sousa, 19, kutoka Arsenal . (Fabrizio Romano)

Wolves wako kwenye mazungumzo juu ya uhamisho wa mkopo kwa mshambuliaji wa Corinthians na Brazil Yuri Alberto , 22 . (Telegraph - usajili unahitajika)

Brighton wako kwenye mazungumzo ya kumleta winga wa Uhispania Bryan Gil, 22, kwa klabu hiyo kwa mkopo kutoka Tottenham. (Evening Standard)

Stuttgart wanashinikiza kumsajili kiungo wa kati wa Ujerumani Mahmoud Dahoud, 28, kutoka Brighton. (Sky Germany)

TH

Chanzo cha picha, Getty Images

Sheffield United wamewasiliana na Leicester City kuhusu uhamisho wa mlinzi wao raia wa Australia Harry Souttar, 25, huku Blades wakijaribu kuimarisha safu yao ya ulinzi. (Football Insider)

Everton pia wanamtazama Souttar, ambaye yuko na kikosi cha Australia kinachoshiriki Kombe la Asia nchini Qatar.. (Football League World)

Crystal Palace wanafikiria kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 27 Maxwel Cornet, ambaye anaweza kuruhusiwa kuondoka West Ham. (Telegraph - usajili unahitajika)

Aberdeen wanawezakumteua Neil Warnock mwenye umri wa miaka 75 kama meneja hadi mwisho wa msimu huu kufuatia klabu hiyo kumfukuza kazi Barry Robson (The Press and Journal)

Imetafsiriwa na Yusuf Jumah