Kyiv yashambuliwa huku viongozi wa dunia wakikutana kwa mkutano wa G20

Urusi imefanya shambulizi katika mji mkuu wa Ukraine Kyiv, huku milipuko ikisikika na moshi ukionekana kupaa angani.

Majengo mawili ya makazi katika wilaya ya kati ya mji huo ni miongoni mwa maeneo yaliyopigwa, kulingana na meya Vitali Klitschko.

 Viongozi wa dunia kwa sasa wanakutana katika mkutano wa G20 nchini Indonesia ambako wamelaani vita dhidi ya Ukraine.

Makombora kadhaa ya Urusi yameweza kudunguliwa na wahudumu wa uokozi wamefika eneo la tukio, amesema Bw Klitschko.

 Tahadhari ya uvamizi huo wa anga pia ilikuwa imetolewa na Ukraine.

Vitaly Kimm, Meya wa Mykolayiv, amedai kuwa makombora ya Urusi yalikuwa yameshambulia katika makundi matatu.

Katika Chernihiv, Gavana Vyacheslav Chaus aliwatahadharisha watu kutafuta hifadhi, akisema kuwa "mashambulio ya makombora yanaendelea ".

Katika kipindi cha wiki iliyopita Urusi iliondoa vikosi vyake katika mji wa kusini mwa Ukraine wa Kherson - ikiwa ni hasara kubwa kwa urusi tangu ilipoivamia Ukraine.

Katika miezi iliyopita Urusi ilipoteza vibaya maeneo iliyokuwa imeyateka katika mashambulio ya ulipizaji yaliyofanywa na vikosi vya Ukraine.

Takriban makombora 70 yamepigwa nchini Ukraine, anasema mshauri wa masuala ya ulinzi wa Ukraine

“Hivi sasa tunavyoongea nimeona ripoti kwamba makombora ya Ballistic yamepigwa Ukraine ," Yuriy Sak anasema.

Baadhi ya maeneo ya mji wa kyiv hayana umeme, anasema meya wa mji, Andriy Sadovy.

Milipuko imesikika pia kaskazini – mashariki mwa Kharkiv

Tumeanza kupikea picha za wimbi la mashambulizi ya makombora ya Urusi kote nchini Ukraine.

Milipuko pia imesikika katika mji wa kaskazini -mashariki wa Kharkiv, kulingana na taarifa ya Interfax Ukraine , shirika la habari la Ukraine.

Meya wa Kharkiv, Igor Terekhov, alisema kuwa kumekuwa na "shambulio la kombora" katika mji huo na hakuna taarifa kuhusu vifo na majeruhi kwa sasa

Alisema kuwa kutokana na uharibifu, kuna matatizo ya umeme katika mji huo ambao umesitisha usafiri wa treni zinazotumia umeme- metro."Wahandishi wa umeme na wafanyakazi wa umma wa maeneo hayo wanafanya kila liwezekanalo kurejesha maisha ya kawaida katika mji wa Kharkiv haraka iwezekanavyo," alisema kwenye Telegram.

 Milipuko pia imeripotiwa katika mji wa Zhytomyr, kulingana na shirika la utangazaji la Ukraine, Suspilne.