Iran, Israel au Marekani, nani aliyeshinda vita?

Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, Kiongozi mkuu wa dini Iran Ali Ayatollah Khamenei na Rais Donald Trump wa Marekani.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, Kiongozi mkuu wa dini Iran Ali Ayatollah Khamenei na Rais Donald Trump wa Marekani.
Muda wa kusoma: Dakika 4

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Guo Jiaqun alisema katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 24 Juni kwamba Beijing "ina wasiwasi mkubwa" kuhusu yaliokuwa yakiendelea katika eneo la Mashariki ya kati kufuatia hatua ya Israel kuishambulia Iran."

Maoni hayo yalikuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza "kukomesha kabisa na kwa kina kwa uhasama huo."

Guo kwa mara nyingine alitoa wito kwa pande zinazohusika kurejea kwenye "njia sahihi ya suluhu la kisiasa" na kusisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kudumisha "amani na utulivu" katika Mashariki ya Kati.

Katika mtandao wa kijamii wa Kichina wa Weibo, watumiaji walikuwa na maoni zaidi au kidogo kwamba mabadiliko ya ghafla ya matukio na tangazo la usitishaji vita vilionyesha kuwa hakuna upande unaotaka vita vya muda mrefu na kwamba pande zote zinajaribu kujionyesha kuwa washindi.

Shen Yi, mchambuzi mashuhuri wa China mwenye msimamo mkali wa kitaifa, alisema si Trump wala Iran waliokuwa tayari kuendeleza vita. Jin Canrong, profesa na mchambuzi mwingine mashuhuri, alielezea shambulio la Iran kwenye kambi ya jeshi la Marekani kama "mwitikio wa ishara.

Qatar ilitangaza kuwa ilinasa makombora yote ya Iran mnamo Juni 23, na Trump aliishukuru Tehran kwa kutoa onyo la mapema ili kuzuia majeruhi.

Pia unaweza kusoma
.

Chanzo cha picha, AFP/GETTY

Hu Xijin, mhariri mkuu wa zamani wa gazeti la kitaifa, linaloendeshwa na serikali Global Times, pia alisema kuwa siku mbili za mwisho za mapigano zilikuwa kama "onyesho" ambalo liliruhusu pande zote kuonekana washindi.

Ho alisema licha ya pigo kubwa lililopata Iran, Tehran iliweza kudumisha taswira yake ya roho isiyoweza kushindwa, kuweka muundo wake wa kisiasa, na kumuweka madarakani Ali Khamenei, kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Aliongeza kuwa Trump sasa anaweza kudai "kumaliza vita" na "kuondoa tishio la nyuklia la Irani." Alisema Trump aliweza kupata "ushindi wa haraka" kwa kuepuka kuiingiza nchi katika vita vya machafuko.

Kuhusu Israel, Hu alisema ingawa nchi hiyo ilishindwa kuuangusha utawala wa Khamenei, ilitoa pigo kubwa kwa uwezo wa nyuklia wa Iran, ambao kwa mujibu wa uchambuzi wa Marekani, utachukua angalau miaka 8 hadi 10 kuujenga upya.

Hatahivyo, Han Peng, mkuu wa ofisi ya Amerika Kaskazini ya kikundi cha habari kinachomilikiwa na serikali ya China, aliandika kwenye Weibo kwamba nchi zote tatu zilishindwa katika vita hivi.

Amesema Iran ilipata uharibifu mkubwa zaidi, kutokana na uharibifu wa sehemu kubwa ya uwezo wake wa nyuklia hadi maafa ya binadamu ambayo yalikuwa mara kumi zaidi ya yale ya Israel.

Lakini kwa upande mwingine, alisema, mashambulizi ya Iran yalionyesha kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa Israel ulikuwa dhaifu.

Hahn ameongeza kuwa, Marekani pia ilionyesha udhaifu wake kwa ulimwengu kutokana na kupungua kwa uwepo wake wa kistratijia katika eneo hilo, na kwamba haikutaka kujihusisha zaidi na vita hivyo.

Trump hakulipiza kisasi baada ya Iran kushambulia kambi ya kijeshi ya Marekani, na aliishukuru Tehran kwa kumtaarifu mapema kuhusu mashambulizi yake.

Je, ni nani mshindi kulingana na China?

.

Chanzo cha picha, CCTV

Kwa upande wa China, Liu Menglong, mwanablogu anayehusishwa na chombo cha habari cha serikali cha Guangcha, alipinga wazo kwamba ushiriki wa Marekani katika vita vikuu inaweza kuwa na manufaa kwa China, akisema kuwa maendeleo ya China hayawezi kudumishwa katika ulimwengu wenye machafuko, uliojaa vita na kuambatana na kutengwa na mataifa makubwa.

Han Peng alikataa maoni kwamba China inaweza kupendelea upande mmoja katika mzozo huo, akisema Beijing inatafuta biashara tu, kwani China ni mshirika mkubwa wa kibiashara wa Iran, mshirika wa pili mkubwa wa kibiashara wa Israel, na mshirika wa tatu wa biashara wa Marekani.

Ameongeza kuwa: "Hakuna mshindi katika vita isipokuwa tu iwapo unaweza kumuondoa adui kwa hatua moja tu. Ushindi wa kweli unaweza kupatikana tu kwa maendeleo. Sio Marekani, wala Iran, wala Israel kwa sasa wenye uwezo wa kuuondoa kabisa upande wa pili, bali kila mmoja anataka kuonekana mshindi.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Seif Abdalla