Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Je, Israel "itatengwa" kimataifa kwa sababu ya vita vya Gaza? - Magazeti ya Israel
Tunaanza kuangazia magazeti ya Israel na gazeti la "Times of Israel", ambalo lilichapisha makala ya mwandishi Yossi Klein Halevi, ambaye alionesha wasiwasi wake kuhusu "kutengwa" kwa watu wa serikali ya Kiyahudi, akitaja kile Wayahudi walivyokuwa wakikabiliwa na mikono ya Wanazi, inayojulikana kama Holocaust. Nakala hiyo ilionya juu ya uwezekano wa Israel kurudi kwenye kutengwa tena.
Mwandishi aliamini kwamba "labda jeraha kubwa zaidi ambalo bado tunaugua kama matokeo ya Holocaust ni kumbukumbu ya kutengwa wakati ulimwengu ulisimama bila kuingiliwa wakati mateso yalipogeuka kuwa mauaji ya kimbari."
Alidokeza kwamba Israel inakabiliwa na kutengwa na jumuiya ya kimataifa wakati inajaribu kushinda jaribu la Oktoba 7, "na inakabiliwa na wimbi la chuki dhidi ya Wayahudi" ambalo limezua hofu ambayo imeleta mshtuko.
"Mwezi mmoja baada ya Oktoba 7, kumbukumbu ya siku hii imefifia katika ghasia," Halevy alisema, akinukuu taarifa za Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye alisema kwamba shambulio la Hamas "halikutokea tu bila sababu." akirejelea miongo kadhaa ya mateso, chini ya uvamizi wa Israel.
Pia alisema kuwa Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama alizitaka pande zote mbili kuwajibika kwa kile kilichotokea, na akasema kwamba tunapaswa "kuzingatia ukweli kuhusu mzozo."
Mwandishi huyo alisema: "Mgogoro huo unapita zaidi ya ule ulinganifu wa mzozo kati ya Israel na Hamas. Wengi katika nchi za Magharibi wameona kwamba kuna tofauti kubwa kati yao ambayo inaonekana Hamas inawakilisha wema huku Israel ikiwakilisha uovu."
Licha ya hofu iliyooneshwa na mwandishi huyo kuhusu uwezekano wa kujitenga na ulimwengu tena, alielezea nia yake ya kukubali kila kitu ambacho kinaweza kutokea kutokana na msimamo wa Israel wa kukataa usitishaji wa mapigano na kuingia katika hali ya kutengwa na ulimwengu wote hatua ambayo ingefanikisha malengo ya nchi yake.
"Ushindi mbaya wa kidiplomasia"
Tunageukia gazeti la Israel la Yedioth Ahronoth, ambalo lilichapisha makala inayokosoa njia za kisiasa na kidiplomasia ambazo serikali ya Israel inashughulikia mzozo wa Gaza, tishio lake kwa taswira ya Israel duniani kote, na uwezekano wa “kuwafanya wapiganaji wa Hamas kuwa mashujaa mbele ya ulimwengu .”
Mwandishi Avi Azikrov alisema: "Licha ya kile kinachosambazwa kuhusu hasara zaidi kati ya safu za IDF wakati wa operesheni za ardhini katika Ukanda wa Gaza, ni lazima kusisitizwa kuwa kushindwa zaidi kwa vikosi vya Israel kunageuka kuwa mafanikio ya kawaida ya operesheni za ardhini, ambazo. huongeza imani katika uwezo wa jeshi.” Kutoa pigo chungu kwa Hamas.”
Alisema pamoja na hayo yote, "karibu dunia nzima inatuona sisi kuwa magaidi huku wao wakimchukulia Yahya Sinwar na wenzake kuwa ni watetezi wa uhuru na kuwasifu duniani kote, ikiwa ni pamoja na maoni ya umma wa Marekani na Uingereza, na bila shaka katika nchi za kiarabu.
Alisema uvamizi wa ardhini katika Ukanda wa Gaza uko njiani kufikia lengo lake, ambalo ni "kuondoa udhibiti wa Gaza kutoka mikononi mwa Hamas," baada ya vikosi vya Israeli kufunga "hospitali" katikati mwa Gaza, ngome ya Hamas huko, pamoja na "kuwashinda wapiganaji wa Hamas ambao "Walikuwa wakijaribu kuzuia majeshi ya Israel kuingia mjini."
Mwandishi huyo alisema: "Ofisi za serikali ya Hamas zimeacha kabisa kufanya kazi huku viongozi wa vuguvugu la kigaidi wakiwa wamejificha kwenye mahandaki na mashimo chini ya Ukanda huo. Ni vigumu kutabiri kwa sasa siku wataliona tena jua. "
Mwandishi huyo alidokeza kuwa licha ya mafanikio hayo ya kijeshi, mitaa ya Marekani na Ulaya bado inapokea maelfu ya waandamanaji wanaodai "ukombozi wa Palestina" na kusitishwa kwa vita huko Gaza.
Mkutano wa kilele wa Waarabu na Kiislamu pia ulifanyika katika mji mkuu wa Saudi, Riyadh, Jumapili iliyopita, ambao ulitangaza kukataa ukiukaji wote wa kibinadamu na kutaka kusitishwa kwa mapigano.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pia alijiunga na kambi hiyo akitaka kusitishwa kwa mapigano.
Kwa sababu hizo, mwandishi aliona kwamba kinachotokea kwa kushirikiana na hatua za kijeshi za Israeli ni "anguko kubwa zaidi la kisiasa, la umma na la kidiplomasia" ambalo ameona katika maisha yake kwa kuzingatia jinsi vita hivyo vilivyoanza.
Mwandishi anaamini kuwa aliyehusika na kushindwa huku ni Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu.
Alisema kuwa Hamas huenda wasiwe madarakani tena huko Gaza, lakini "tunapozungumzia siku inayokuja baada ya hapo, Netanyahu atakuwa sehemu ya tatizo kuliko sehemu ya suluhu."
Imetafsiriwa na Lizzy Masinga na kuhaririwa na Seif Dzungu