Tetesi za Soka Ulaya Jumanne: Rashford tayari kupunguziwa mshahara kubaki Barcelona

Marcus Rashford is

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marcus Rashford anataka kusalia Barcelona
Muda wa kusoma: Dakika 2

Marcus Rashford, 28, hataki kurejea Manchester United mkataba wake wa mkopo Barcelona utakapokamilika na mshambuliaji huyo wa Uingereza yuko tayari kupunguziwa mshahara ili kusalia. (Mirror)

Kiungo wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso anatarajiwa kujumuishwa kwenye orodha ya wachezaji watatu wanaotarajiwa kuchukua nafasi ya Pep Guardiola huku tetesi zikiongezeka kwamba huu utakuwa msimu wa mwisho wa kocha huyo wa Manchester City. (Telegraph - usajili unahitajika)

Beki wa Ufaransa Dayot Upamecano, 27, anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Bayern Munich. (Fabrizio Romano)

Beki wa Manchester United Mholanzi Tyrell Malacia, 26, ameghadhabishwa na mkurugenzi wa kandanda wa klabu hiyo Jason Wilcox kwa kumzuia kuhama Old Trafford.( Mirror)

Malacia alikuwa karibu kukamilisha uhamisho wa kwenda Besiktas nchini Uturuki lakini Wilcox akamwambie beki huyo kwamba hana budi kusalia Manchester United. (Sportsport)

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Uingereza Raheem Sterling, 31, alipewa ofa ya kujiunga na klabu ya Bundesliga Union Berlin siku chache zilizopita lakini hakutilia maanani ombi hilo. (Florian Plettenberg)

Raheem Sterling akiichezea Chelsea

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Raheem Sterling akataa kuhamia Bundesliga

Mshambulizi wa Ufaransa Karim Benzema, 38, anatarajiwa kujiunga na klabu nyingine ya Saudi Pro League Al-Hilal . Benzema alijiunga na Al-Ittihad kwa mkataba wa miaka mitatu baada ya kuondoka Real Madrid msimu wa joto wa 2023. (The Athletic)

Tottenham haikufanikiwa kufikia mkataba na klabu ya Monaco kwa ajili ya Maghnes Akliouche, 23, lakini huenda wakamnunua kiungo huyo wa kati wa Ufaransa msimu wa joto. (Team talk)

Imetafsiriwa na Ambia Hirsi