Miji minne inayotoa kipaumbele kwa wasafiri wenye walemavu

Chanzo cha picha, Getty Images
Wasafiri walemavu huangalia nini wanapochagua jiji la kutembelea? Hili ni muhimu si tu kwa wenye ulemavu tu, bali pia kwa miji yenyewe inapotafuta kuingia katika soko kubwa la sekta ya usafiri linaloweza kufikiwa.
Kwa kuwa mtu mmoja kati ya sita anaishi na ulemavu, ni muhimu kuhakikisha kuwa miji yote ulimwenguni inafikiwa na watu wote. Lakini ni miji gani inayofanya vizuri zaidi, na kwa namna gani?
Singapore
Singapore imekuwa mahali pazuri pa kusafiri kwa watu wengi ikilinganishwa na sehemu kubwa ya Asia, kwa kiasi fulani kutokana na miundombinu bora na vistawishi bora, na kwa sababu Kiingereza ni lugha ya kawaida.
Lakini kama msafiri mlemavu, kuna kiwango cha juu cha ufikiaji kinachoifanya kuvutia zaidi.
Katika Singapore, swali sio, "Ni nini kinachoweza kupatikana?" lakini badala yake, "Ni nini hakiwezi kupatikana?"
Wengi wa waliojibu katika utafiti huo walichagua Singapore kwa sababu ya usafiri wake wa umma unaoweza kufikiwa, ambao hufanya kuzunguka jiji kuwa rahisi.
Tofauti na treni nyingi za chini ya ardhi, kuna kiwango cha ufikaji kwa kila gari kwenye usafiri wa reli Singapore, ambaoo huwapa watumiaji wa viti vya magurudumu na watu wenye ulemavu uhuru na heshima.
Zaidi ya hayo, zaidi ya 95% ya njia za waenda kwa miguu, vituo vya teksi na mabasi zinapatikana kwa watu wanaoishi na matatizo mbalimbali, na zaidi ya 85% ya mabasi ya umma yanafikiwa na viti vya magurudumu.
Kulingana na Nilesh Joshi, ambaye alihama kutoka Mumbai hadi Singapore miaka minane iliyopita, "Kwa mtu kama mimi, mwenye changamoto za ulemavu lakini bila [kutumia] kiti cha magurudumu, jiji linanipa urahisi mkubwa na kuniruhusu kuzunguka kwa uhuru kwa kutumia usafiri wa umma na kufurahia hduma za umma."
Watumiaji wa usafiri wa umma wenye matatizo ya kusikia pia wanahudumiwa vyema: kama mkazi Adrian Yap alivyosema, "Wakati wote kuna tangazo lolote kwenye treni, tunaweza kuona maagizo yaliyoandikwa kwenye klioo cha runinga." Yap pia alibainisha kuwa "maafisa wa treni wamefunzwa vyema kuwasiliana nawenye ulemavu wa kusikia", akisisitiza umuhimu wa mafunzo ya ufahamu wa ulemavu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mojawapo ya vivutio vikuu vya watalii vya Singapore, Gardens by the Bay, eneo la kipekee na la kuvutia la maonyesho ya bustani, linaweza kufikiwa kikamilifu na mtu anayetumia kiti cha magurudumu.
Kuna huduma ya usafiri ya bila malipo kwa watumiaji wa viti vya magurudumu na kukodisha viti vya magurudumu kwa dola 2 tu kwa siku - jambo linaloashiria ongezeko la umuhimu wa usafiri, hasa miongoni mwa jumii za Asia.
Kivutio kipya kabisa cha jiji, usanifu wa ajabu unaounganisha Jumba la Jiji la enzi za ukoloni na Mahakama ya Juu ya zamani ina mwongozo wa kina, unaoweza kupakua kwa maelekezo- ilitengenezwa na Chama cha Watu Wenye Ulemavu cha Singapore - ambao huruhusu wageni kupanga safari zao na kupata habari juu ya ufikiaji wa maonyesho au sherehe mahususi.
Las Vegas
Uchumi wa wageni - si tu utalii, lakini pia soko la thamani kubwa la MICE - ni muhimu sana kwa Las Vegas.
Utalii unachangia 20% ya Pato la Taifa la Las Vegas (ikilinganishwa na wastani wa kitaifa wa 6%) na 30% ya kazi (mara mbili ya wastani wa kitaifa).
Inashangaza, ni makazi ya hoteli 14 kati ya 25 kubwa zaidi duniani na, kulingana na mwanablogu mashuhuri mwenye ulemavu John Morris, ambaye hutoa taarifa katika wheelchairtravel.org na kutembelea jiji mara tatu au nne kwa mwaka, "Jiji lina mojawapo ya viwango vya juu zaidi. vyumba vya hoteli na vyumba vinavyoweza kufikiwa duniani, huku wamiliki wa hoteli wakiwa na shauku ya kuvutia dola za walemavu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Hoteli nyingi za Las Vegas pia zina mtaalamu maalum wa watu Wenye Ulemavu anayewasaidia wageni wenye ulemavu - na kuhakikisha kuwa hoteli hiyo haikosi mtaalamu katika nchi hii yenye kesi nyingi.
Kasino na vyumba vya maonyesho huhudumia vyema watumiaji wa viti vya magurudumu na wageni walio na matatizo mengine: wafanyakazi wanafundishwa kusaidia watu wenye matatizo ya kuona na kusikia kwenye meza za michezo ya kubahatisha.
Baadhi ya hoteli hata hutoa masomo ya michezo ya kubahatisha bila malipo na wakalimani wa lugha ya ishara.
Vivutio vingine vikuu vya jiji pia vinaweza kufikiwa, ikiwa ni pamoja na Gurudumu la High Roller Ferris (gurudumu refu zaidi la kuzunguka hewani), puto ya hewa moto na nyaya za kuteleza juu iliyopitiwa na Morris.

Chanzo cha picha, Getty Images
Sydney
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Julie Jones, msimamizi wa kikundi cha Facebook cha Accessible Sydney na mchapishaji wa Travel Without Limits, jarida pekee duniani lililobobea katika masuala ya safari , anaelezea kufurahishwa na urahisi wa kufikia sehemu mbalimbali katika jiji hilo la Australia.
Yeye na mwanawe Braeden ambaye anatumia kiti cha magurudumu "wanapenda kutembea Sydney na wanagundua kuwa jiji lenye ufikiaji mzuri".
Sehemu kubwa ya vivutio vikuu vya Sydney, ikiwa ni pamoja na majengo mengi ya Taasisi ya Kitaifa ya Jiji, yanaweza kufikiwa kwa watumiaji wa viti vya magurudumu.
Nyumba maarufu ya Opera ya Sydney ina vituo vyenye huduma kwa watu wenye mahitaji ya maalumu ya kufika hapo, ikiwa ni pamoja na burudani zinazopatikana na programu za wenye ulemavu.
Na baada ya miaka mingi ya kampeni, lifti ziliwekwa kwenye Daraja la Harbour miaka minne iliyopita.
Uwezo wa kutembea au kukimbia karibu na mandhari bora ya jiji ni raha, aliongeza Jones: "Sehemu kubwa ya mfumo wa usafiri wa umma ni rahisi kwa watumiaji wa viti vya magurudumu, ikiwa ni pamoja na vivuko vyetu vya Sydney, ambavyo hutoa mandhari bora ya bandari yetu nzuri.
Kuna kilomita kadhaa za njia za watu wenye ulemavu karibu na bandari inayounganisha Nyumba ya Opera na Darling Harbour na zaidi.
Uwezo wa kutembea au kukimbia karibu na mandhari bora ya jiji ni raha." Uzoefu wa Jones unakubaliana na wale wa washiriki wa uchunguzi huu, ambao walitaja jiji hilo.
Mtandao wa usafiri wa umma wa jiji, ambao ni pamoja na vivuko, mabasi, reli ya mwanga (trams) na reli, vinafikika kwa urahisi kabisa, ingawa mara nyingi inahitajika msaada kutoka kwa madereva.
"Hivi karibuni, mfumo wa reli wa Sydney umekuwa rahisi zaidi kwa watu wenye ulemavu usioweza kuonekana na sasa wafanyakazi wamepewa mafunzo ya kutambua na kujibu wasafiri wenyw ulemavu usioweza kuonekana," Jones alisema.

Chanzo cha picha, Getty Images
London
London pia ilipata alama za juu katika utafiti huo, huku 57% ya waliohojiwa wakiipendekeza kwa njia zake za usafiri zinazoweza kufikiwa, wakati karibu nusu walichagua mji mkuu huokwa sababu vivutio vyake vya kitamaduni vina usaidizi mzuri wa ufikiaji kwa watu wenye ulemavu na vifaa.
Makumbusho nyingi kubwa zimeweka mkazo mahususi katika ufikaji kwa watu wenye ulemavu, ikijumuisha Makumbusho ya Uingereza, Makumbusho ya Kisasa ya Tate na Makumbusho ya Historia Asilia.
Pia kuna habari nyingi zinazopatikana kwa watu wenye ulemavu kupanga likizo na matembezi.

Chanzo cha picha, Getty Images
London, kama ilivyo kwa jiji lolote kubwa, inaweza kuwa na changamoto ya kusafiri kama mtumiaji wa kiti cha magurudumu, lakini kuna mifumo bora ya ufikiaji sehemu.
Sambamba na majibu ya uchunguzi, aina nyingi za usafiri wa umma zinapatikana kwa urahisi, na mabasi yote yanaweza kufikiwa na viti vya magurudumu, kama vile vituo vyote vya mabasi ya umeme na vivuko vingi.
Hata hivyo ni karibu theluthi moja tu ya vituo vya chini ya ardhi vina fikika bila changamoto yeyote, kwa hivyo kupanga kwa uangalifu ni muhimu kabla ya kusafiri.
Kama mwanablogu asiyeona, Sassy Wyatt anasema London ni rahisi kuzunguka: "Ninaweza kufika kituo chochote cha chini ya ardhi na kutumia huduma ya kurejea na kwenda inayotolewa na Transport for London: mfanyakazi ataniongoza kupitia kituoni na kunipeleka kwenye mstari sahihi, mfanyakazi mwingine atakutana na mimi upande wa pili na kunisindikiza hadi njia ya kutoka, na kuniokoa na uchovu mwingi wa akili."











