Nini kinachofanya wakati kwenda kwa kasi mwezini ikilinganishwa na duniani?

..

Chanzo cha picha, Getty Images

Mwezini, wakati huenda haraka kuliko duniani kwa sekunde 58.7 kila siku.

Hili huenda lisionekane kuwa jambo kubwa, lakini lina athari kubwa wakati wa kujaribu kusawazisha safari za vyombo vya anga kwenye satelaiti, haswa sasa kwa kuwa mbio za anga za juu sio tu kwa juhudi za kitaifa, lakini pia kwa ushindani kati ya kampuni za kibinafsi.

Ndiyo maana Ikulu ya Marekani na Shirika la Anga za Juu la Ulaya zinafanya kazi katika uundaji wa mfumo mpya wa wakati.

Kwa nini wakati mwezini hupita haraka?

Jambo la kwanza unahitaji kujua ni kwamba wakati unapita kwa njia tofauti katika sehemu tofauti za Ulimwengu.

Hakuna wakati wa kawaida wa ulimwengu kwa vile vyote viko anga za mbali, kwa njia sawa kwamba nguvu ya mvuto si sawa kwa vyote.

Ikilinganishwa na Dunia, "mvuto kwenye Mwezi ni dhaifu kidogo na saa hufanya kazi tofauti," kulingana na mwanaastronomia Catherine Heymans alizungumza kwenye kipindi cha cha BBC Radio 4.

Ikiwa utaweka saa hizo kwenye Mwezi, katika miaka 50, zitakuwa mbele kwa sekunde moja zaidi.

Leo, muda hupimwa Duniani kwa mamia ya saa za atomiki zilizo maeneo tofauti ya sayari yetu ambazo hufuatilia mabadiliko ya hali ya nishati ya atomi ili kurekodi muda hadi nanosecond.

Kevin Coggins, mwakilishi wa mawasiliano wa NASA, alielezea kuwa katika muktadha huo, "inaeleweka kwamba unapoenda kwenye sayarii nyingine, kama Mwezi au Mars, kila moja ina mpigo wake wa moyo."

Mvuto zaidi muda ukienda polepole

xx

Chanzo cha picha, Getty Images

Wazo kwamba wakati ni tofauti linatokana na nadharia ya Albert Einstein.

Maoni ni kwamba ambapo mvuto una nguvu zaidi, wakati hupita polepole zaidi.

Na mvuto huwa na nguvu kadiri ukubwa wa kitu unavyoongezeka.

Kwa mfano, chombo kilichojazwa kitu kizito, kama vile granite, kina wingi zaidi na kwa hivyo mvuto zaidi kuliko chombo sawa kilichojaa maji.

Katika anga, Mwezi una ukubwa mdogo kuliko Dunia, kwa hiyo nguvu ya mvuto ya Mwezi ni chini ya ile ya Dunia.

Hiyo inaelezea ni kwa nini mtu ana uzito mdogo kwenye Mwezi.

Nguvu hii ya uvutano hafifu ndiyo sababu tuna picha maarufu za wanaanga wa Apollo wakiruka kwenye uso wa Mwezi.

Kwa hiyo, uzito mkubwa wa mwili, mvuto wake mkubwa na wakati utapita polepole.

Kwenye Jupiter, kwa mfano, wakati hupita polepole zaidi kuliko Duniani kwa sababu mvuto ni mkubwa.

Lakini kwa Mwezi, wakati hupita haraka kwa sababu nguvu yake ya uvutano ni kidogo.

Athari za kuunda "saa ya mwezini"

Marekani inapendekeza uundaji wa " Wakati Ulioratibiwa wa Mwezini."

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Marekani inapendekeza kubuniwa kwa " Wakati Ulioratibiwa wa Mwezini."
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ikulu ya White House imelitaka Shirika la Anga za mbali la Marekani (NASA) kuunda saa mpya ya Mwezi.

Mpango wao ni kwamba ratiba hiyo mpya itawasaidia kuhakikisha kwamba juhudi za kitaifa na za kibinafsi kufikia Mwezi haziendi katika njia tofauti.

Hata hivyo, haitakuwa rahisi kwa nchi zote kukubaliana kuhusu mfumo huu mpya wa wakati unapaswa kuwa na ni shirika gani la kimataifa litakuwa na jukumu la kuuratibu.

Hivi sasa, kazi hii inafanywa na Ofisi ya Kimataifa ya Mizani na Vipimo kwa Hali ya Hewa Duniani (BIPM).

Kutoka hapo “Muda Ulioratibiwa wa Pamoja” unaotumiwa na Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu unasimamiwa.

Lakini kwa kuwa mbio za anga za juu zinalenga Mwezi, muda unaotumika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Anga hautakuwa mwafaka zaidi, kulingana na wataalamu.

Kipengele kingine ambacho nchi zitalazimika kuafikiana ni wapi muda mpya unaanza na urefu wake ni wa muda gani.

Je! nchi zinazoshindana kama vile Uchina, Urusi au Marekani zitaweza kukubaliana juu ya "wakati mpya wa mwezi?

Haionekani kuwa rahisi sana wakati wa mivutano ya kijiografia ambayo uhusiano wa kimataifa unakuwa ni sababu.

Lengo la mwaka 2026 na misheni ya mwanadamu

Wanaanga Eugene Cernan na Harrison Jack Schmitt

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wanaanga Eugene Cernan na Harrison Jack Schmitt walisafiri hadi Mwezini kwenye misheni ya Apollo 17 mnamo 1972.

Marekani inataka ratiba yake mpya ya wakati wa mwezi iwe tayari ifikapo 2026, kwa wakati muafaka kwa ajili ya misheni yake ya kuelekea Mwezini.

Artemis-3 itakuwa safari ya kwanza kurejea mwezini tangu Apollo 17 mwaka 1972. Imepangwa kutua kwenye ncha ya kusini ya mwezi, ambayo inaaminika kuwa na hifadhi kubwa ya barafu ya maji kwenye volkeno ambazo hazipati mwangaza wa jua.

Kutafuta na kuelekeza misheni hii kunahitaji usahihi wa hali ya juu hadi nanosekunde , kwa kuwa hitilafu yoyote ile inaweza kusababisha chombo kuingia kwenye njia zisizo sahihi na kugongana.

Ikiwa muda wa mwezi hautaratibiwa kati ya nchi na makampuni ya kibinafsi ambayo yanapanga kufanya safari Kwenda sayari hiyo, changamoto mpya zinaweza kutokea ambazo, pamoja na kupunguza uwezekano wa mafanikio ya misheni, changamoto katika kutuma data na mawasiliano kati ya chombo kinachofanya safari za anga, satelaiti na Dunia.