Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Man City wanamfikiria Gibbs

Chanzo cha picha, Getty Images
Kiungo wa kati wa Nottingham Forest na England Morgan Gibbs-White, 25, ni mojawapo ya chaguo ambalo Manchester City inamfikiria kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa Ubelgiji Kevin de Bruyne, 33. (Athletic)
Arsenal wako tayari kulipa euro 150m (£128m) kwa mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 27. (Fichajes)
Klabu ya Chelsea ipo tayari kuilipa Manchester United pauni za Uingereza milioni tano ili kuwezesha usajili wa kudumu wa kiungo wa pembeni raia wa Uingereza Jadon Sancho, 25, anayecheza Chelsea kwa mkopo.(Sun Club)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mshambuliaji wa Napoli na Nigeria Victor Osimhen, 26, anapendelea kuhamia Juventus au klabu ya Ligi ya Premia mara tu muda wake wa mkopo huko Galatasaray utakapomalizika. Chelsea, Arsenal na Manchester United wote wanavutiwa na mshambuliaji huyo, ambaye anapatikana kwa euro 65m (£55.7m). (ESPN)
Kiungo wa kati wa Brentford na Nigeria Frank Onyeka, 27, atarejea katika klabu hiyo mara baada ya muda wake wa mkopo katika klabu ya Augsburg ya Bundesliga kukamilika msimu huu wa joto. (Florian Plettenberg)
Bayern Munich na Ajax wametuma maskauti kumwangalia kiungo wa kati wa Manchester City na England chini ya umri wa miaka 18 Divine Mukasa, 17, ingawa City wanapanga kuongeza mkataba wake. (Fabrizio Romano)

Chanzo cha picha, Getty Images
Bosi Enzo Maresca anajipanga bila winga wa Ukraine Mykhailo Mudryk, 24, na fowadi wa Ufaransa Christopher Nkunku, 27, katika kikosi chake cha Chelsea msimu ujao. (Sun Club)
Arsenal wanatayarisha ofa yenye thamani ya euro 30m (£25.6m) kwa kiungo wa kati wa Real Madrid na Uturuki Arda Guler, 20, ambaye hajafurahishwa na muda wake mdogo wa kucheza. (Fichajes)
Mkufunzi wa Crystal Palace Oliver Glasner anashawishika kuihama klabu hiyo msimu huu wa joto ili kuchukua nafasi ya juu katika klabu ya RB Leipzig. (Football Insider)















