Tetesi za soka Ulaya: Vilabu 7 vinamtaka Raheem Sterling

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 2

Wawakilishi wa winga wa England Raheem Sterling, 31, ambaye aliondoka Chelsea kwa makubaliano ya pande zote mapema wiki hii, wako kwenye mazungumzo na vilabu saba vya kiwango cha Ligi ya Mabingwa Ulaya vinavyotaka kumsajili. (Sky Sports)

Tottenham wanaangalia kwa umakini uwezekano wa kumsajili Sterling, ambaye sasa ni mchezaji huru, na kocha Thomas Frank yuko tayari na anaunga mkono uhamisho huo. (Teamtalk)

Burnley, pamoja na vilabu vya Italia vya Serie A Juventus na Napoli, pia vina nia ya kumsajili Sterling. (Mail)

Manchester United hawatamsajili kiungo wa Chelsea Cole Palmer, 23, msimu huu wa joto, kwani viongozi wa klabu wanajua kuwa mchezaji huyo wa England yuko nje ya uwezo wao wa kifedha. (Mirror)

s

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea wanapanga kutumia euro milioni 150 (£129m) kumsajili kiungo wa Real Madrid na England Jude Bellingham, 22, msimu huu wa joto. (Fichajes)

Ajax wako tayari kumsajili kiungo wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 29, ambaye yuko kwa mkopo Nottingham Forest kutoka Arsenal, kwa uhamisho wa kudumu wa takriban euro milioni 1.5 (£1.3m), pamoja na ziada endapo klabu hiyo ya Uholanzi itafuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya. (Fabrizio Romano)

Kocha wa Aston Villa, Unai Emery, yupo kwenye orodha ya Real Madrid ya makocha wanaoweza kuchukua nafasi ya kuwa kocha mpya msimu huu wa joto. (Sky Germany)

Chelsea bado wako kwenye mazungumzo na Rennes kumsajili beki wa kati wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20, Jeremy Jacquet, kabla ya dirisha la usajili la Januari kufungwa. (Givemesport)

Real Madrid wanataka kumsajili beki wa pembeni wa Manchester United na Ureno Diogo Dalot, 26, kutokana na udhaifu wao katika safu ya ulinzi. (Fichajes)

Manchester City wamekubali kumpeleka beki kinda wa England mwenye umri wa miaka 17, Stephen Mfuni, kwa mkopo Watford hadi mwisho wa msimu. (Fabrizio Romano)