Kifahamu kisiwa kidogo cha Ujerumani chenye watu 16

l;

Chanzo cha picha, Getty Images

Muda wa kusoma: Dakika 3

Oland ni kisiwa kidogo ambacho kinatumia reli nyembamba kuungana na bara. Kisiwa hicho kinakisiwa kina idadi ya watu 16. Mnara mdogo zaidi wa taa nchini Ujerumani upo hapa, ukiwa pia ndio pekee wenye paa la nyasi.

Watu wameishi katika eneo hili tangu Enzi za Kati, Oland ya leo ilikuwa imeungana na eneo la Hallig Langene hadi mafuriko ya Burchardi 1634. Hallig ikawa ndogo kutokana na mawimbi mengi ya dhoruba kwa karne nyingi.

Tangu 1927, Oland na Hallig Langene zinaunganishwa kwa reli nyembamba. Zaidi ya hayo, Oland ina bandari ndogo. Boti ndogo zinaweza kuingia bandarini baada ya maji mengi kujaa.

Halligen, ni mkusanyiko wa visiwa vilivyo karibu na pwani ya kaskazini mwa Ujerumani, visiwa hivi ni muhimu kwa Ujerumani kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Mabadiliko ya Tabianchi

Mabadiliko ya tabianchi ni tishio kubwa kwa visiwa vya Halligen katika Bahari ya Wadden kaskazini mwa Ujerumani, vitaathiriwa sana na kasi inayotarajiwa ya kupanda kwa usawa wa bahari.

Watu wa Hallig lazima walindwe kutokana na kupanda kwa bahari. Eneo hili hukumbwa na mafuriko ya mara kwa mara kutoka baharini. Kupanda kwa kasi kwa viwango vya bahari kunawakilisha hatari kwa watu na asili.

Ndege wa Halligen katika Bahari ya Wadden kaskazini mwa Ujerumani (Schleswig-Holstein) ni wa kipekee duniani. Mshairi Theodor Storm aliwahi kuwaita ndge "wanao ogelea". Watu chini ya 300 wanaishi pamoja na ndege wa pwani wapatao 60,000 wanaozaliana katika visiwa hivi vidogo katika Bahari ya Wadden.

Ndege wengi aina ya oystercatcher, terns, na shakwe huzaliana huko kwa wingi kwenye takriban hekta 2,000 za vinamasi vya chumvi. Makumi ya maelfu ya ndege wengine wanaotembea majini na ndege wa majini hupumzika hapa, kama vile bata bukini.

Ulinzi dhidi ya maji

l

Chanzo cha picha, Getty Images

Nyumba za watu wa Halligen zimesimama kwenye vilima vya makazi vilivyozungukwa na Hifadhi ya Kitaifa ya Bahari ya Wadden na Eneo la Urithi wa Dunia. Vilima vidogo ambavyo nyumba hizo zinalindwa kutokana na mafuriko.

Ni kwa sababu Halligland hufurika mara kadhaa kwa mwaka wakati wa mafuriko ya dhoruba. Kuwalinda watu kutokana na mafuriko ya dhoruba ni lengo muhimu sana la vilima hivi.

Mabadiliko ya tabianchi na kasi ya kupanda kwa usawa wa bahari katika siku zijazo ni tishio kubwa kwa visiwa hivi. Viota vya ndege wa pwani pia viko katika hatari ya kuwa waathiriwa wa mafuriko ya mara kwa mara.

Ili kuiokoa Halligen, ulinzi wa mazingira unahitajika zaidi ya yote, lakini pia hatua za ziada za kukabiliana na athari za tabia nchi.