Mtu ambaye alikwenda kina cha chini zaidi ya bahari

.

Chanzo cha picha, SUE FLOOD

Mgunduzi wa bahari Kapteni Don Walsh amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Aliweza kuzama hadi kwenye kina kirefu zaidi cha bahari miaka 60 iliyopita.

Sehemu hii, inayoitwa Mfereji wa Mariana, iko kilomita kumi na moja katika kina cha bahari.

Fuatilia simulizi ya kipekee ya mtu aliyekwenda kina cha chini zaidi ya bahari.

Katika miaka ya 1960, shauku ya wanaanga ilienea ulimwenguni ya kutimiza ndoto yao ya safari ya kwanza kwenye anga la mbali.

Lakini nahodha wa miaka 28 Don Walsh aliangazia zaidi kilindi.

Alikwenda sehemu ya chini kabisa ambayo mguu wa mwanadamu haujawahi kufikia.

Wakati huo, Jeshi la Wanamaji la Marekani lilikuwa na manowari mpya Triste.

Na, Dunn, Luteni mtaalamu wa nyambizi, akajitolea kujiunga na mradi huo.

Alipojiunga na operesheni hiyo, kina kirefu zaidi alichowahi kufika kilikuwa mita 100 tu.

Alishtuka baada ya kujua jinsi atakavyoingia ndani zaidi ya bahari. Kina ambacho jeshi la wanamaji walitaka aende kilikuwa mara 100 zaidi.

Mradi huo ulikuwa ni kwenda kwenye sehemu ya kina cha chini zaidi katika sayari.

Sehemu ya chini kabisa ya Mfereji wa Mariana, ambalo ni bonde jembamba chini ya Bahari ya Pasifiki na liko nje kidogo ya Ghuba ya Guam.

.

Chanzo cha picha, NAVAL HISTORICAL FOUNDATION

Nilichosema cha kwanza ilikuwa, 'Nini?'" Dunn alisema katika mahojiano ya 2011. Kwa nini hawakuniambia haya kabla sijajitolea?"

"Kisha nikajiambia: Nafahamu fika kwamba angalau kwa nadharia inaweza kufanywa na kuna njia ya kuifanya ifanye kazi."

Mnamo Januari 23, 1960, Dan na Jacques Picard, mtaalamu wa bahari wa Uswisi ambaye alikuwa ameunda manowari ya Triste kwa msaada wa baba yake, Ott Picard, walianza operesheni yao na kuvuka mawimbi na kuelekea kwenye kina kirefu cha bahari.

Walijiweka ndani ya chumba kilichokuwa na ukuta mnene wa chuma.

Don alisema kuwa nafasi waliyokuwa nayo ni saizi ya jokofu kubwa la nyumbani. Hewa ndani ilikuwa baridi kama friji.

Wapelelezi wawili walizama polepole gizani. Shinikizo la eneo linalozunguka, liliongezeka huku manowari ikifanya kelele.

.

Chanzo cha picha, NOAA

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Chombo hicho kilijengwa kwa namna ambayo inaweza kuhimili shinikizo mara 1000 zaidi ya shinikizo kwenye uso wa maji, lakini haijawahi kujaribiwa kuthibitisha uwezo wake wa juu wa kuhimili kina hicho.

Mwanzoni mwa kushuka, kila kitu kilikuwa kikienda vizuri, lakini walipofika kina cha mita 9,000, manowari ghafla ilitoa mshindo mkubwa, ambao ulikuwa wa kutisha.

"Ilikuwa sauti isiyo ya kawaida," Don alisema baadaye. Hatujawahi kusikia sauti kama hiyo hapo kabla."

Ilikuwa ni sauti kama kitu kikubwa kimepasuka. Don na Jacques walikagua kwa uangalifu data kutoka kwa vifaa walivyokuwa navyo. Kila kitu kilionekana kuwa sawa. Ndio maana waliamua kwenda chini zaidi.

Baada ya saa tano, kipimo cha kina kilionyesha mita 10,000, lakini bado hapakuwa na dalili ya sakafu ya bahari.

Walishangaa ni kwa kiasi gani walipaswa kwenda chini.

Lakini mwishowe, kuakisiwa kwa taa za utafutaji za manowari kuliweza kufichua jambo fulani. Don na Jacques walikuwa wamefaulu: kwa kina cha kilomita 11, walikuwa wamefika chini ya Mfereji wa Mariana.

"Tulipoketi kwenye sakafu ya bahari, kulikuwa na nyenzo nyingi zilizotawanyika," Dunn alisema. Nyenzo zinazounda sakafu ya bahari zilikuwa nusu-kioevu.

"Ilikuwa kama kuangalia bakuli la maziwa. Ndio maana hatukupiga picha sehemu hii ya kina kabisa ya chini ya bahari."

Mwishoni mwa mteremko huu hadi mahali pa kina zaidi ulimwenguni na rekodi iliyopatikana, hakukuwa na kupiga makofi wala mbwembwe.

"Kulikuwa na ukimya wa muda mfupi," Dunn anakumbuka.

Walikaa chini ya bahari kwa dakika 2. Walipokuwa wakiichunguza manowari hiyo, waligundua sauti ya kishindo waliyosikia hapo awali ilitoka kwa nini.

Moja ya madirisha ilipata ufa. Kwa bahati nzuri, haikuwa imepata shinikizo kwa sababu kama ingekuwa hivyo, ingeweza kusababisha manowari kulipuka mara moja.

Waliweza kurudi kwa salama wa salmin hadi kwenye uso wa maji.

Timu yao ya watu wawili iliweza kuweka historia. Walipokea Nishani ya Ubora kutoka kwa Rais Dwight D. Eisenhower na pia walitiwa moyo na medali na tuzo nyingine nyingi walizopata baadaye.

.
Maelezo ya picha, Dunn alishirikiana na mkurugenzi wa filamu James Cameron

Safari ya kwenda katika kina cha chini zaidi ya bahari kwa namna fulani iliathiri maisha yote ya Don na ikawa sehemu ya utu wake. Alitania kwamba alitumia maisha yake yote kula chakula cha jioni na watu wengine akizungumzia hilo.

Wale kama mimi ambao wamevutiwa na bahari na wametumia maisha yao yote kujifunza juu yake, wana hamu ya kusikia juu ya uzoefu wake wa mahali pa kushangaza zaidi duniani alipokwenda.

Don alikuwa mtu mkarimu, mcheshi na mnyenyekevu ambaye siku zote alipenda kuzungumza juu ya uzoefu wake wa kipekee.

Lakini Don hakuwa mfungwa wa maisha yake ya zamani, alifanya zaidi ya uzoefu huo.

Kwenda kwake kwenye kina kirefu cha bahari ilikuwa mwanzo tu wa miaka ya kazi ya kusaidia ugunduzi wa baharini na wale ambao walitaka kuchunguza na kujifunza juu ya bahari.

Alionya kuhusu mkasa uliotokea kwa manowari ya Titan. Manowari hiyo iliyokuwa ikielekea upande wa kushoto wa meli ya Titanic, ililipuka ikiwa njiani na kuwaua wote sita waliokuwa ndani yake.

Miaka mingi kabla ya hapo, alikuwa amemwandikia Mkurugenzi Mtendaji wa watengenezaji wa Titan, akionya kwamba kushindwa kufanya majaribio ya manowari kunaweza kuwa na matokeo mabaya.

Baada ya Dunn kufaulu kupiga mbizi hadi mahali hapo mnamo 1960, alifikiria mtu mwingine angetaka kurudi baada ya miaka miwili.

Kwa kweli, ilichukua miaka 50 kwa safari hii kurudiwa tena.

.

Chanzo cha picha, REEVE JOLLIFFE

Imefasiriwa na Asha Juma